#TAFAKARI YA LEO; USIWE MPUMBAVU…

By | May 8, 2018

“Intelligent individuals learn from every thing and every one; average people, from their experiences. The stupid already have all the answers.” — Socrates Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni fursa nzuri na ya kipekee kwetu, kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. (more…)

UKURASA WA 1223; Lisha Unachotaka, Siyo Unachokwepa…

By | May 7, 2018

Iwapo timu mbili zitaingia uwanjani, moja ikaenda kwa lengo la kushindwa na nyingine ikaenda kwa lengo la kutokushindwa, timu yenye nafasi kubwa ya kushinda ni ile inayoenda na lengo la kushinda. Hata kwa wanaoangalia mchezo huo, watakaoburudika zaidi ni wale wanaoangalia mchezo wa timu inayokwenda kwa lengo la kushinda, na (more…)

UKURASA WA 1222; Jinsi Ya Kujua Tabia Halisi Ya Mtu Kwenye Ufanyaji…

By | May 6, 2018

Ni vigumu sana kuzijua tabia za binadamu, kwa sababu kinachotutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine, ni uwezo wetu wa kuhadaa wengine. Tunaweza kuwatega wanyama wakali kama simba na chui kwa sababu wanatabirika. Lakini kumtega binadamu ni kugumu kwa sababu hatabiriki, na anaweza kuhadaa. Hivyo unapojifanya unatafuta kujua tabia ya mtu, (more…)

DARASA LA WIKI; FALSAFA YA USTOA NA MATUMIZI YAKE KWENYE ZAMA TUNAZOISHI.

By | May 6, 2018

UTANGULIZI KUHUSU FALSAFA. Tangu enzi na enzi kumekuwepo na falsafa mbalimbali hapa duniani. Falsafa imekuwa ni njia ambayo wanadamu wamekuwa wakiitumia kuielewa dunia, kuyaelewa maisha na kujua kwa nini wapo hapa duniani. Maisha yetu sisi binadamu ndiyo maisha ya viumbe ambao hawajaandaliwa kuendana na mazingira tunayoishi, hivyo inatuhitaji sisi kutumia (more…)

UKURASA WA 1221; Njia Mbili Za Kukabiliana Na Mabaya Yanayotokea Kwenye Maisha…

By | May 5, 2018

Kuna mabaya, majanga mbalimbali yanayotokea kwenye maisha yetu ya kila siku. Ni mambo ambayo hatukutegemea yatokee, lakini pia hatuwezi kuyazuia yasitokee. Mfano ukame, mafuriko, magonjwa ya mlipuko na kadhalika. Yapo mabaya na majanga mengi ambayo tumewahi kukutana nayo na tutaendelea kukutana nayo. Unaweza kuomba sana usikutane na mabaya hayo, lakini (more…)

UKURASA WA 1220; Jinsi Ya Kumshinda Goliath Wako…

By | May 4, 2018

Hadithi ya Daudi na Goliath ni hadithi ambayo kwa namna tofauti imefundishwa kwenye kila jamii, kuhusu mtu mdogo anayepindua mtu mkubwa na kuleta mabadiliko. Kila mmoja wetu ni Daudi kwenye eneo fulani, na kuna Goliath ambaye anamsumbua, ambaye ni mkubwa na anatumia ukubwa wake kuwakandamiza wengine. Iwe ni kwenye kazi, (more…)

UKURASA WA 1219; Kutaka Kila Mtu Akubaliane Na Wewe…

By | May 3, 2018

Fanya chochote unachotaka kufanya na wapo watakaosema unakosea, hata kama unaona unafanya kitu sahihi kiasi gani. Hata kama utachukua fedha zako na kwa roho yako moja ukaamua kugawa kwa wengine, wapo watakaokuambia bora ungefanya nazo kitu kuliko kugawa. Hivyo basi, kutaka kila mtu akubaliane na wewe, ni moja ya mambo (more…)