UKURASA WA 1218; Tukumbushane Jinsi Ya Kusikiliza…

By | May 2, 2018

Mtu akikuambia anataka umlipe hela ili akufundishe jinsi ya kusikiliza utamcheka, au siyo? Kwa sababu utaona ni kitu cha ajabu mno. Yaani ufundishwe jinsi ya kusikiliza, kwamba huna masikio au una matatizo gani? Lakini ukweli ni kwamba, kila mmoja wetu ana mengi ya kujifunza kuhusu kusikiliza. Na kwenye zama hizi (more…)

UKURASA WA 1217; Matatizo Yanakuja Yenyewe, Suluhisho Linahitaji Kazi…

By | May 1, 2018

Ukiacha shamba lenye rutuba bila ya kulifanyia chochote, magugu yataota na kustawi vizuri sana. Lakini magugu siyo kitu unachotaka kwenye shamba lako, ila yamejiotea yenyewe. Ukitaka kusafisha shamba hilo, utahitaji kuweka kazi, tena siyo ndogo. Hutakuta shamba lenye magugu limejisafisha lenyewe, lakini shamba safi utalikuta lina magugu lenyewe. Kwa asili, (more…)

UKURASA WA 1216; Raha Leo Maumivu Kesho…

By | April 30, 2018

Ni asili ya binadamu kupenda raha, kupenda kile kinacholeta manufaa ya haraka kuliko kile ambacho manufaa yake yanachelewa. Lakini sheria ya asili ni hii, chochote kinachokupa raha leo, kesho kitakupa maumivu. Ni sheria ya asili, ambayo huwezi kubishana nayo na wala huwezi kuikwepa. Jaribu kuangalia mifano kwenye kila eneo la (more…)

UKURASA WA 1215; Maamuzi Unayofanya Kwa Hekima…

By | April 29, 2018

Hatua ngumu kwenye maisha na mafanikio ni kufanya maamuzi. Kwa sababu unapofanya maamuzi, maana yake unakubali kuachana na mengine yote na kufanya kile ulichochagua kufanya au kufuata. Watu wengi hukwepa kufanya maamuzi kwa sababu wanaona kuacha mengine ni hatari kubwa. Kwa mfano kuingia kwenye biashara fulani ni maamuzi magumu kufanya (more…)

UKURASA WA 1214; Mipango Isiyo Ya Kawaida, Isiyowezekana Kwa Uhalisia…

By | April 28, 2018

Uhalisia ni kifo cha mafanikio, pale unapopanga kitu na kuanza kujiuliza kama kinaendana na uhalisia au la, ndiyo mwisho wako wa kwenda mbali zaidi. Huwa tunapenda kuweka mipango ya kawaida, mipango inayoendana na kile tulichozoea, mipango inayowezekana na inayoendana na uhalisia. Mtu mmoja amewahi kusema, watu wa kawaida huwa wanaenda (more…)

UKURASA WA 1213; Zingatia Vitu Hivi Viwili Na Mara Zote Utakuwa Mbele Ya Wengine…

By | April 27, 2018

Ushindani ni mkali sana zama hizi, chochote unachofanya, wapo wengine ambao wanakifanya pia. Na hata ukiamua kuwa mbunifu na ukaanzisha kitu chako mwenyewe, watu wakishaona kinafanya kazi watakuiga, huna njia ya kujimilikisha chochote unachofanya, hata kama umekibuni mwenyewe. Hivyo ili kuepuka ushindani na wale ambao wanafanya kile unachofanya, vipo vitu (more…)