UKURASA WA 1128; Kuepuka Kukosolewa…

By | February 1, 2018

Meli inakuwa salama sana inapokuwa imetia nanga bandarini, ndege inakuwa salama kabisa ikiwa imetua kwenye uwanja wa ndege. Ni mpaka pale meli inapotoa nanga na kuanza kuelea, au ndege inaondoka uwanjani na kuanza kupaa ndipo hatari zinaweza kujitokeza. Kwa meli kukubwa na dhoruba na kuzama au ndege kukutana na hali (more…)

UKURASA WA 1127; Unaanza Na Mtu Mmoja…

By | January 31, 2018

Kuanza jambo lolote jipya, huwa ni kugumu. Hii ni kwa sababu wengi huwa tunafikiria makubwa. Kwamba mtu anapotaka kuanza kitu, anawaangalia wale ambao tayari wameshafanya kwa muda mrefu na kufika juu kabisa. Kwa mfano kama unataka kuanza biashara, halafu unaowaangalia ni wakina Mengi au Bakhresa, utaona kwamba wako mbali sana, (more…)

UKURASA WA 1126; Upendo Na Wema…

By | January 30, 2018

Ukisikie neno Msamaria mwema unapata picha gani? Kwa wengi ni mtu ambaye anajitoa kuhakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora zaidi, hata kama hakuna anachonufaika nacho moja kwa moja kwa kufanya hivyo. Sasa zipo zawadi kuu mbili ambazo kila mmoja wetu anazo, lakini namna tunavyozitumia tunatofautiana. Zawadi ya kwanza ni upendo. (more…)

UKURASA WA 1125; Kama Ni Kazi, Tayari Imeshakushinda…

By | January 29, 2018

Tunapokutana na kitu kigumu kwenye maisha, tunasema ni kazi kweli kweli. Hii inaonesha ni kwa namna gani tunaitafsiri kazi kwenye akili zetu, kwamba ni kitu chochote ambacho ni kigumu na ambacho hatupo tayari. Sasa kama chochote unachofanya kwenye maisha yako kinakuwa kazi, unakuwa umeshashindwa kabla hata hujaanza. Ukiangalia watu wa (more…)

UKURASA WA 1124; Hapo Unawapa Watu Nafasi Ya Kukutawala…

By | January 28, 2018

Kuna kutawaliwa kwa nguvu, halafu kuna kutawaliwa kwa hisia. Kutawaliwa kwa nguvu au mabavu kunaweza kuumiza, lakini kunafanyika na mtu mwingine, hivyo angalau unaweza kuwa na mtu wa kumlaumu na hata kupambana kupata uhuru wako. Lakini kutawaliwa kwa hisia, kunaumiza zaidi, ila ubaya ni kwamba, unakuwa umejiweka wewe mwenyewe kwenye (more…)

UKURASA WA 1123; Matatizo Magumu Kutatua Ni Tunayotengeneza Wenyewe…

By | January 27, 2018

Asili, yaani ulimwengu kwa ujumla wake, huwa inawaandaa viumbe hai wote kwenye kuendana na mazingira ambayo viumbe hawa wanajikuta. Kwa mfano, mmea ambao unaota kwenye eneo la jangwa, huwa na majani madogo na membamba, wakati mwingine miiba kabisa. Hii inapunguza mmea huo kupoteza maji mengi kwenye mazingira hayo ya jangwa. (more…)