UKURASA WA 1117; Watu Hawa Walikuja Baada Ya Ndoto Zako…

By | January 21, 2018

Ni jambo la kushangaza namna gani watu wapo tayari kuacha ndoto zao kwa sababu ya maoni au mtazamo wa watu wengine. Au mtu anaacha kufanyia kazi ndoto zake kubwa alizokuwa nazo, kwa sababu ya watu ambao wanamhitaji afanyie kazi vitu vingine. Cha kushangaza ni kwamba, watu wengi ambao watu wanawakubalia (more…)

UKURASA WA 1116; Vitu Vitatu Vya Kujijengea Uwezo Ili Kuwa Na Maisha Ya Uhuru Na Mafanikio.

By | January 20, 2018

Tunadanganyika kwamba uhuru ni kuweza kupata kila unachokitaka kwa namna unavyotaka wewe. Na mafanikio ni kuwa na kila unachokitaka kwa namna unavyotaka wewe. Yote hayo mawili ni uongo kwa sababu hakuna yeyote anayeweza kupata kila anachokitaka kwa wakati anaotaka na namna anavyotaka yeye. Kuna wewe kutaka na kuna dunia kutoa. (more…)

UKURASA WA 1115; Ni Urafiki Na Mapenzi Ndiyo Vinajenga Wateja Wazuri…

By | January 19, 2018

Kitu kimoja ambacho huwa napenda kuwakumbusha wafanyabiashara mara kwa mara ni kwamba wateja wananunua kwa sababu zao binafsi na siyo kwa sababu zako. Mteja hanunui kwa sababu wewe unauza, ila ananunua kwa sababu anahitaji kununua. Na kama ambavyo tunajua, sisi binadamu ni wabinafsi, tunajali mambo yetu zaidi kuliko kitu kingine (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAISHA HAYAKUSUBIRI WEWE…

By | January 19, 2018

While we are postponing, life speeds by. – Lucius Annaeus Seneca Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo tunakwenda kuishi kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana. Pia kwa TATUA, AMUA NA (more…)

UKURASA WA 1114; Jikumbushe Kila Siku…

By | January 18, 2018

Kitu kimoja ambacho sisi binadamu tunacho ni kusahau, tunasahau mambo haraka sana. Na hili siyo baya, bali ni jambo zuri kwa sababu yapo mambo ambayo kama siyo kusahau basi maisha yetu yatakuwa hovyo. Kuna mambo makubwa, magumu na mabaya tunakutana nayo kwenye maisha yetu ambayo kama siyo kusahau, tunaweza kukata (more…)

UKURASA WA 1113; Orodha Ya Vitu Vya Kufikiria…

By | January 17, 2018

Muda tulionao kwenye siku yetu ni masaa 24 pekee, haujawahi kuongezeka na hakuna dalili kwamba muda huu utaongezeka siku za hivi karibuni. Lakini mambo ya kufanya yanazidi kuwa mengi, tunazidi kuwa na majukumu mengi katika muda mfupi tulionao. Kama hiyo haitoshi, kiasi cha taarifa na maarifa tunayoyapata kwenye siku yetu (more…)

UKURASA WA 1112; Muunganiko Na Wengine, Utengano Na Wewe Mwenyewe…

By | January 16, 2018

Zama za taarifa, zama za teknolojia ambazo tumeungana kwa masaa 24. Sasa hizi, kwa masaa 24 ya siku unaweza kupata taarifa yoyote unayotaka, unaweza kuwasiliana na yeyote unayetaka. Muunganiko huu unaweza kuwa kitu kizuri, na unaweza kiwa kitu kibaya pia, kama hutaweza kuutumia vizuri. Kwa mfano, kadiri watu wanavyounganika na (more…)