UKURASA WA 1073; Darasa La Kushindwa Kwako….

By | December 8, 2017

Mwandishi Brian Tracy kwenye kitabu chake cha THE PSYCHOLOGY OF SUCCESS anasema kwamba watu ambao hawajafanikiwa wana tatizo kubwa sana. Wakipata kitu wanaona ni bahati, na wakishindwa au kukosa kitu basi wanaona ni bahati mbaya au kisirani kwao. Kwa njia hiyo, hawajifunzi na wala hawapati mbinu bora za kupata kile (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ZUNGUKWA NA WANAOKUVUTA KWENDA JUU…..

By | December 8, 2017

The key is to keep company only with people who uplift you, whose presence calls forth your best. – Epictetus Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku ya leo, nafasi nyingine nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa. Kama kuna chochote ambacho jana ulisema utafanya kesho, (more…)

UKURASA WA 1072; Usiangalie Kipato Pekee, Angalia Maisha Unayotengeneza Pia…

By | December 7, 2017

Watu wengi wanapochagua kazi au biashara ya kufanya, huanza kuangalia ni kiasi gani cha fedha wanaweza kupata. Na kama kuna machaguo mengi ya vitu wanaweza kufanya, wengi huchagua kile wanachoona kitawalipa zaidi. Wapo wengine wanasema wazi kabisa kwamba wapo tayari kufanya chochote kama kinawaingizia fedha. Hali kama hii ni kawaida (more…)

UKURASA WA 1071; Acha Kujitengenezea Mateso…

By | December 6, 2017

Kusudi la maisha halijawahi kuteseka, Ni kweli changamoto na vikwazo vingi vipo kwenye safari ya maisha, lakini havipaswi kuwa chanzo cha mateso. Ukiiangalia dunia jinsi ilivyo, hakuna namna yoyote imejipanga kuwatesa watu. Lakini watu wanateseka kila siku, kwa sababu wanachagua kujitengenezea mateso wao wenyewe. Yaani ni sawa na kuwe na (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ishi Maisha Yako Na Waruhusu Wengine Kuishi Maisha Yao.

By | December 5, 2017

KITABU; Meditations / Marcus Aurelius. UKURASA; 38 – 47. Ni tabia yetu binadamu kutaka watu wawe kama tunavyotaka kuwa sisi. Kutaka wafanye kile tunachotaka wafanye na hata kufikiri vile tunavyotaka sisi wafikiri. Marcus anatuambia huku ni kupoteza muda wetu, kwa sababu hatuwezi kuwafanya wengine wawe kama tunavyotaka siai. Wala hatupaswi (more…)

UKURASA WA 1070; Kupata Fedha Kwa Muda Mrefu Ni Zao La Maono Makubwa…

By | December 5, 2017

Tuongee jambo moja muhimu sana, ambalo naona wengi tunalisahau hasa kwenye zama hizi za utitiri wa fursa ambazo zinaonekana kuwawezesha watu kupata fedha. Kuna kupata fedha mara moja, au mara chache na kuna kupata fedha kwa muda mrefu. Yaani haya mawili ni sawa na mtu unakinga maji kwa mvua inayonyesha (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Muda Wa Maisha Yetu, Kifo Na Kilicho Muhimu Zaidi Kwetu.

By | December 4, 2017

KITABU ; Meditations / Marcus Aurelius. UKURASA; 29 – 38. Muda wa maisha yetu hapa duniani ni mfupi sana. Muda huu una ukomo, hivyo chochote ambacho mtu unapanga kufanya, ni vyema ukakifanya kwa muda ulionao sasa. Kuahirisha mambo na uvivu mwingine wowote wa kusema nitafanya, ni kujaribu kupoteza muda huu (more…)