Jinsi ya kujijengea udhibiti binafsi (self-control).

By | September 16, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 45 – 55 Jinsi ya kujijengea udhibiti binafsi (self-control). Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, watu wenye udhibiti binafsi wanakuwa na maisha bora na yenye mafanikio kuliko wale wanaokosa udhibiti binafsi. Wanafalsafa wa (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Mfumo Wa Biashara Moja Kusimama Kabla Hujaenda Nyingine…

By | September 15, 2017

Tunaishi kwenye dunia ya wingi, kila mtu anapenda kuwa na vitu vingi. Kwa sababu dunia inachanganya wingi na mafanikio. Kwamba mwenye vingi ndiye aliyefanikiwa, asiyekuwa na vingi basi ameshindwa. Hii ni falsafa mbovu sana kwenye kila eneo la maisha. Lakini inakuwa mbovu zaidi inapoingia kwenye biashara. Wapo watu wanapima mafanikio (more…)

UKURASA WA 989; Weka Nguvu Zako Kwenye Kile Unachoweza Vizuri…

By | September 15, 2017

Unapoanza kufanya kitu chochote kwenye maisha, na kikatoa majibu mazuri, hutakosa watu wa kukushauri ni namna gani unaweza kuboresha zaidi. Watu watakupa mbinu na njia za kuweza kufanya zaidi. Sasa ushauri na njia nyingi unazopewa huwa zinakuondoa kwenye kusudi lako la mwanzo. Wengi wanaokuwa wanakushauri wanafanya hivyo kwa kuangalia vitu (more…)

HALI YETU YA UDHIBITI JUU YA MAMBO YANAYOTUTOKEA.

By | September 15, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 33 – 45. HALI YETU YA UDHIBITI JUU YA MAMBO YANAYOTUTOKEA. Mambo yote yanayotokea kwenye maisha yetu tunaweza kuyagawa katika makundi mawili. 1. Mambo ambayo yapo chini ya udhibiti wetu, haya (more…)

BIASHARA LEO; Jua Eneo Hili La Biashara Yako Linalokurudisha Nyuma.

By | September 14, 2017

Biashara yenye mafanikio inaendeshwa kwa mfumo. Mfumo wa biashara unakuwa na vipengele mbalimbali kama mauzo, masoko, uzalishaji, usimamizi na kadhalika. Kwa njia hii ya mfumo, mmiliki wa biashara anaweza kuiendesha vizuri biashara yake na kwa mafanikio makubwa sana. Lakini mifumo yote ina changamoto kubwa moja, eneo moja likiwa na changamoto, (more…)

#KURASA_KUMI; Nini maana ya maisha mazuri?

By | September 14, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 21 – 31. Nini maana ya maisha mazuri? Swali moja ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kuhusu maana ya maisha mazuri. Kumekuwepo mijadala mingi kuhusu nini maana ya maisha mazuri na (more…)

UKURASA WA 988; Kabla Hujazama, Elewa Misingi…

By | September 14, 2017

Hakuna watu hatari kama waliozama na kubobea kwenye jambo lolote kabla hawajaielewa misingi. Kwa sababu uzamivu wao, hugeuka kuwa hatari kwao na kwa wengine kuliko unavyokuwa faida, hata kama ni kwa jambo zuri. Chukua mfano wa fedha, kila mtu anapenda fedha, kila mtu anakazana kupata fedha, lakini mtu anapozama kutafuta (more…)

#TAFAKARI YA LEO; THAMANI IPO KWENYE KUPOTEZA…

By | September 13, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi (more…)