UKURASA WA 714; Hofu Kama Rafiki…

By | December 14, 2016

Kuna mambo mengi ambayo umekuwa unapanga na kupenda kufanya kwenye maisha yako, ila unashindwa kufanya kwa sababu ya hofu. Unakuwa na mipango mizuri, lakini inapofikia utekelezaji hofu inabisha hodi, vipi kama nikishindwa, vipi kama sitaweza, wengine watanichukuliaje na mengine mengi. Watu wengi wamekuwa wanasikiliza hofu hizi na kushindwa kabisa kuchukua (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UNAMWANGALIA NANI?

By | December 13, 2016

Hongera kwa siku nyingine nzuri sana ya leo rafiki. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa zaidi ili kupata matokeo bora zaidi. Tumia muda wa leo vizuri kwa sababu ukishapita hautorudi tena. Asubuhi ya leo tutafakari ni mtu gani ambaye unamwangalia. Japokuwa unahitaji kuishi maisha yako, na kupanga (more…)

UKURASA WA 713; Jiambukize Mafanikio…

By | December 13, 2016

Mafanikio yanaambukizwa, na ndiyo maana kukaa karibu na watu waliofanikiwa, au kujifunza kupitia wao, unajiweka kwenye nafasi ya wewe kufanikiwa pia. Na kama ukikaa karibu na watu walioshindwa, au kujifunza kupitia wao, pamoja na kuwasikiliza, basi utaambukizwa kushindwa. Pamoja na kwamba tunaambukizwa mafanikio kutoka kwa wengine, pia sisi wenyewe tunaweza (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; SELFISHNESS…

By | December 12, 2016

Hongera rafiki yangu kwa nafasi hii nzuri sana ya leo. Na siku nyingine nzuri ambapo tumepata nafasi ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tulichochagua kufanya. Tutumie nafasi hii ya leo vizuri rafiki. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu SELFISHNESS yaani UBINAFSI. Ili tuweze kuendelea, na ili tuweze kuwasaidia (more…)

UKURASA WA 712; Biashara Katika Maneno Matatu…

By | December 12, 2016

Moja ya hatua muhimu unazopaswa kupiga kila siku ili kufanikiwa ni kuchukua jukumu kubwa na kuligawa kwenye majukumu madogo madogo. Kitu chochote kikubwa, huwa kinawatisha watu kufanya, kama ukiambiwa umle tembo, ni vigumu, lakini ukimkatakata tembo katika vipande vidogo vidogo unaweza kumla. Tukija kwenye biashara, kuiangalia biashara kama biashara ni (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Unapimaje Ushindi Kwenye Maisha Yako?

By | December 11, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo tunashirikishana misingi muhimu ya kuweza kujenga maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa. Tupo hapa tulipo sasa kwa sababu sisi ni washindi. Jamii nzima ya binadamu inasonga mbele kupitia ushindani. Kwa sababu (more…)

UKURASA WA 711; Njia Ya Uhakika Ya Kujiongezea Kujiamini…

By | December 11, 2016

Watu wana mawazo mazuri sana, ambayo kama wakiyafanyia kazi basi yanaweza kuleta mapinduzi makubwa mno. Watu wana ubunifu mkubwa sana ambao upo ndani yao, na kama wakiutumia basi wanaweza kufanya makubwa. Lakini cha kushangaza, wengi hawatoi zawadi hizi kubwa ambazo zipo ndani yao. Mwandishi mmoja aliwahi kusema, wengi wanakufa na (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; GO WITH THE FLOW….

By | December 10, 2016

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tulichopanga kufanya ili tuweze kupata matokeo makubwa zaidi. Tutumie muda wetu wa leo vizuri rafiki kwa sababu ukishapita hauwezinkurudi tena. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KWENDA NA HALI (more…)

UKURASA WA 710; Vitu Viwili Muhimu Vitakavyowawezesha Watu Kukuelewa Na Kukuamini…

By | December 10, 2016

Moja ya eneo gumu sana kwenye maisha yetu ya kila siku, ni watu kutuelewa na hatimaye kutuamini. Kuaminiana ndiyo kunaendesha kila kitu, kuanzia biashara, kazi na hata familia. Na ili watu wakuamini ni lazima kwanza wakuelewe kwa kile unachofanya au unachosema. Lazima watu wakuelewe kwa aina ya biashara unayofanya na (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; FURSA MPYA…

By | December 9, 2016

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu? Ni matumaini yangu kwamba uko vizuri na unakwenda kuianza siku hii ya kipekee ukiwa na hamasa ya hali ya juu. Najua leo utakwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya. Na nina uhakika utafanya makubwa leo. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu FURSA MPYA…. Kama (more…)