Mambo muhimu ya kufanya pale mauzo yanaposhuka.

By | March 23, 2015

Wewe kama mjasiriamali kipato chako kinategemea mauzo ya bidhaa au huduma unayotoa. Hii ni sawa na kusema kwmaba kama huuzi basi huna biashara na kama huna biashara maana yake upo kwenye hali mbaya sana kifedha. Vile vile katika ujasiriamali, kipato hakilingani siku zote, kuna wakati ambao utakuwa na kipato kikubwa (more…)

KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

By | March 23, 2015

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia. Jambo moja (more…)

NENO LA LEO; Huu Ndio Ufunguo Wa Maisha, Na Sio Elimu.

By | March 23, 2015

“The key to life is accepting challenges. Once someone stops doing this, he’s dead.” ― Bette Davis Ufunguo wa maisha ni kuzikubali changamoto. Mtu atakapoacha kuzikubali changamoto, amekufa. Hakuna maisha ambayo hayana changamoto, kwa kifupi hakuna mtu ambaye hana matatizo. Ukiwa huna fedha unakuwa na matatizo, ukiwa na fedha unakuwa (more…)

KITABU; SHERIA 48 ZA NGUVU KATIKA UONGOZI.

By | March 22, 2015

Katika moja ya matatizo yanayoisumbua nchi yetu na hata bara la Africa kwa ujumla ni ukosefu wa uongozi mzuri. Tunao viongozi ambao wamepewa nafasi za kuongoza ila hawajapata mafunzo mazuri ya uongozi. Kuongoza kwa utashi kila mtu anaweza, lakini hakumwezeshi kiongozi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali za zama hizi. Kwa (more…)

UKURASA WA 81; Achana Na Ubishi, Hautakusaidia Lolote.

By | March 22, 2015

Ukishaamua ni kitu gani ambacho unataka kufanya kwenye maisha yako, basi hapo ndio unafunga mjadala. Usijiingize kwenye ubishi kuhusiana na kile unachofanya. Kama umeshaamua kwamba wewe utakuwa mjasiriamali, anza kufanya ujasiriamali, jua kabisa mpaka unakufa wewe utakuwa mjasiriamali. Kuanza kuingia kwenye ubishi kama mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa hakutakusaidia lolote. Kuanza (more…)

NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Nguvu Zako.

By | March 22, 2015

“Look well into thyself; there is a source of strength which will always spring up if thou wilt always look.” ― Marcus Aurelius Angalia vizuri ndani ya nafsi yako na utaona chanzo kikubwa cha nguvu ambacho kitaendelea kububujika kama utaendele  kukitumia. Kama unafikiri huna nguvu, kama unafikiri huna ujasiri basi (more…)

UKURASA WA 80; Utabiri Mzuri Wa Kesho.

By | March 21, 2015

Je unahitaji mtu wa kukusaidia kuitabiri vizuri kesho yako? Huna haja ya kwenda kwa wapiga ramli au watabiri wa nyota, kwani mtabiri bora kabisa tayari upo nae hapo ulipo. Mtabiri huyo ni wewe mwenyewe. Unafikiria kama biashara unayofanya itakuletea mafanikio makubwa baadae? Unafikiria kama kazi unayofanya utadumu nayo kwa muda (more…)

NENO LA LEO; Umuhimu Wa Kuchukua Hatari.

By | March 21, 2015

“Risk anything! Care no more for the opinion of others … Do the hardest thing on earth for you. Act for yourself. Face the truth." ― Katherine Mansfield, Kuchukua hatari ndio kila kitu. Usijali maoni ya wengine… Fanya vitu ambavyo ni vigumu sana kwako. Fanya mambo yako. Ukabili ukweli. Kuna (more…)

TAFAKARI YA LEO; Urefu Wa Muda Sio Mrefu.

By | March 20, 2015

Utaanza lini kutekeleza mipango mizuri uliyoweka? Muda sio mrefu. Karibu kila mmoja wetu ameshaingia kwenye mtego huu, wa kufikiria muda sio mrefu. Lakini swali la msingi ni urefu wa muda sio mrefu ni upi? Yaani unaposema muda sio mrefu, kiuhalisia unamaanisha nini? Kesho? Wiki ijayo? Mwezi ujao? Mwaka ujao? Kulingana (more…)

UKURASA WA 79; Usitegemee Nyundo Tu, Kuna Zana Nyingine Pia.

By | March 20, 2015

Wenye busara walipata kusema maneno haya mazuri sana; Kama zana pekee uliyonayo ni nyundo, basi kila kinachokuja mbele yako kitaonekana kama msumari. Umeielewa vizuri kauli hiyo? Kama hujaielewa tafuta mtoto mdogo halafu mpe nyundo akae nayo tu na uone atakuwa anafanya nini. Atagonga kila kitu. SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa (more…)