Tag Archives: HUDUMA KWA WATEJA

BIASHARA LEO; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.

By | June 12, 2015

Biashara ni uaminifu, kama hakuna uaminifu hakuna biashara. Kama bado unafanya biashara kwa mazoea yale ya zamani kwamba biashara ni kuwaibia watu, usiendelee kusoma makala hii maana tutakavyojadili hapa hutavielewa. Badala yake fungua makala za nyuma kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO na uanze kujifunza yale muhimu kwanza. Sasa twende (more…)

BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara.

By | June 11, 2015

BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara. Jana nilikuwa kwenye ofisi moja, mama mmoja akatoka kwenda kutoa fedha kwa njia ya simu na kununua vocha pia. Baada ya muda alirudi akiwa amekamilisha zoezi lake na kutaka kuingiza vocha kwenye simu. Alipoangalia akakuta amepewa vocha mara mbili ya alizoagiza. Alinunua (more…)

BIASHARA LEO; Sehemu Mbili Anazokwenda Mteja Wako Unazotakiwa Kuzijua.

By | June 10, 2015

Unapokuwa kwenye biashara, jukumu lako kubwa ni kumjua mteja wako kuliko hata anavyojijua wewe mwenyewe. Labda sio, lakini cha msingi lazima umjue mteja wako vizuri. Changamoto nyingi za biashara zinaanza pale mfanyabiashara anaposhindwa kumjua mteja wake vizuri na hivyo anashindwa kwenda naye vizuri kwenye biashara yake. Kama unasema huna haja (more…)

Jinsi ya kutumia wateja wako kama sehemu ya kutangaza biashara yako.

By | June 8, 2015

Linapokuja swala la kutangaza biashara, watu hufikiria matangazo kwenye vyombo vikubwa vya habari, kupata tangazo wakati wa taarifa ya habari, ambapo watu wengi wanaangalia. Au kudhamini michezo inayofuatiliwa na wengi. Au kuweka bango kubwa kwenye eneo ambalo watu wengi wanapita. Hizi zote ni njia nzuri za kutangaza biashara yako, ila (more…)

BIASHARA LEO; Sahau Kuhusu Kuongeza Faida Na Fanyia Kazi Kitu Hiki Kimoja Kwanza.

By | May 21, 2015

Lengo la biashara sio kutengeneza faida. Kama utakataa sentensi hiyo na una biashara fanya jaribio. Endesha biashara yako kwa lengo moja tu, kupata faida. Na hivyo tumia njia yoyote unayoona itakuwezesha kukuletea faida. Utaipata faida hii kwa muda mfupi lakini biashara haitokua, itakufa. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa makala (more…)

BIASHARA LEO; Kama Biashara Yako Isingekuwepo….

By | May 19, 2015

Leo kaa chini na ujiulize na kupata jibu la swali lifuatalo; Kama biashara yako isingekuwepo, je watu wanaokuzunguka wangekuwa katika hali gani? Je dunia ingekuwa kwenye hali gani? Kama jibu ni hakuna tofauti kati ya kuwepo au kutokuwepo kwa biashara yako, basi huna biashara, yaani upo tu unasukuma siku. SOMA; (more…)

BIASHARA LEO; Unawachukia Wateja Wasionunua Kwako?

By | May 14, 2015

Nakumbuka zamani kidogo, ulikuwa kama umezoea kununua vitu kwenye duka moja, na siku kitu ulichokuwa unataka hukukipata, ukaenda kwenye duka jingine ambapo mfanyabiashara anajua huwa unanunua wapi, angeweza kukataa kukuuzia. Anaweza kukuambia kwamba kila siku unapita pale na kwenda kununua kwingine kwa nini leo uende kununua kwake. Mwingine anaweza kukataa (more…)

BIASHARA LEO; Usianze Biashara Upya Kila Siku…

By | May 13, 2015

Moja ya changamoto zinazowasumbua watu wengi kwenye biashara ni kuanza upya biashara kila siku na kila mara. Hali hii imefanya biashara zionekane ni ngumu sana kuliko ugumu wenyewe. Mtu anaanzaje biashara upya kila siku? Sio kwamba mtu anafunga biashara yake na kuanza upya, ila uendeshaji wake wa biashara unakua ni (more…)

BIASHARA LEO; Upya Wa Biashara Mpya Na Unavyoweza Kuutumia Vizuri…

By | May 12, 2015

Biashara mpya zimekuwa na mambo mengi sana. Kuna biashara ambazo huwa zinaanza kwa wateja wachache sana na kuna nyingine zinaanza na wateja wengi sana. Biashara zinazoanza na wateja wachache tulishajadili hapa na hatua gani za kuchukua. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile isome hapa; Aina Tatu Za Wateja Na (more…)

BIASHARA LEO; Njia Kumi Rahisi Za Kufukuza Wateja…

By | May 11, 2015

Mara nyingi huwa tunafanya mambo kwa mazoea. Na kutokana na mazoea hayo tunasahau kwamba matokeo ya kile tunachofanya yanaweza kuwa mabaya sana kwenye biashara zetu. Kuna njia uliyozoea kufanya biashara yako ambapo kwa njia hiyo unafukuza wateja wengi zaidi ya wale ambao unawakaribisha. Na hii imekuwa inaumiza biashara yako kidogo (more…)