Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Huuzi Tu Biashara, Unajiuza Na Wewe Pia.

By | September 25, 2017

Katika kununua, watu wanaendeshwa na hisia zaidi ya fikra. Huwa tunafikiri kwamba watu watakuwa ‘logical’ katika kufanya maamuzi ya kununua, lakini huo siyo ukweli. Watu huwa wanaendeshwa na hisia zaidi katika kufanya maamuzi kuliko kufikiri kwa kina. Na hapo ndipo wengi wanapokosea, kwa kuamini watu watanunua kile wanachouza, kwa sababu (more…)

BIASHARA LEO; Kazi Yako Siyo Kuwaambia Watu Kipi Wanataka, Bali Kuwasikiliza Nini Wanataka.

By | September 22, 2017

Mapinduzi makubwa sana yameshafanyika kwenye biashara kwa ujio wa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Sasa hivi nguvu kubwa ipo kwa wateja na siyo wafanyabiashara. Siku za nyuma ilikuwa kampuni inaamua izalishe nini, kisha inatengeneza matangazo yenye kuvutia sana na kuwashawishi watu mpaka wapokee ile bidhaa inayotolewa. Lakini sasa (more…)

BIASHARA LEO; Watu Hawapendi Kuuziwa, Bali Wanapenda Kununua.

By | September 21, 2017

Hii ni dhana ambayo itakusaidia sana kubadili mtazamo wako kibiashara, hasa pale unapokutana na mteja wako. Japokuwa upo kwenye biashara kuuza bidhaa na huduma unazotoa, kumbuka kwamba mteja haji kwako kwa sababu wewe unauza. Bali mteja anakuja kwako kwa sababu ana shida au changamoto, na ana amini ya kwamba wewe (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Mmoja Asikufanye Ubadili Biashara Yako Yote…

By | September 19, 2017

Wakati unapoanza biashara yoyote, huwa unakuwa na mawazo yako juu ya biashara hiyo. Huwa unakuwa na mipango mikubwa juu ya biashara yako na wateja unaowalenga pia. Lakini unapoingia kwenye biashara hasa, mambo huwa tofauti na ulivyotegemea. Wakati mwingine kitu ulichofikiri wateja wanakitaka kweli kinakuwa siyo kitu chenyewe. Hili linakufanya ubadili (more…)

BIASHARA LEO; Mahitaji Binafsi Na Mahitaji Ya Wengine Kwenye Biashara…

By | September 18, 2017

Zipo biashara ambazo huwa zinaanza kwa hamasa na nguvu kubwa. Biashara hizo zinakua kwa kasi sana, watu wanapata mahitaji yao na wanaridhishwa sana. Lakini baada ya muda, biashara hizi zinaacha kuwapendeza watu, zinatoa huduma mbovu na watu kuzikimbia. Yapo mengi yanayoweza kusababisha hali ya aina hii kwenye biashara, lakini kubwa (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Mfumo Wa Biashara Moja Kusimama Kabla Hujaenda Nyingine…

By | September 15, 2017

Tunaishi kwenye dunia ya wingi, kila mtu anapenda kuwa na vitu vingi. Kwa sababu dunia inachanganya wingi na mafanikio. Kwamba mwenye vingi ndiye aliyefanikiwa, asiyekuwa na vingi basi ameshindwa. Hii ni falsafa mbovu sana kwenye kila eneo la maisha. Lakini inakuwa mbovu zaidi inapoingia kwenye biashara. Wapo watu wanapima mafanikio (more…)

BIASHARA LEO; Jua Eneo Hili La Biashara Yako Linalokurudisha Nyuma.

By | September 14, 2017

Biashara yenye mafanikio inaendeshwa kwa mfumo. Mfumo wa biashara unakuwa na vipengele mbalimbali kama mauzo, masoko, uzalishaji, usimamizi na kadhalika. Kwa njia hii ya mfumo, mmiliki wa biashara anaweza kuiendesha vizuri biashara yake na kwa mafanikio makubwa sana. Lakini mifumo yote ina changamoto kubwa moja, eneo moja likiwa na changamoto, (more…)

BIASHARA LEO; Hebu Tukumbushane Tena Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Biashara…

By | September 13, 2017

Nimekua nakuambia hili mara kwa mara, na leo nakukumbusha tena kwamba siyo lazima kila mtu ajiajiri na kuwa na biashara. Lakini kila mtu anapaswa kuwa na mifereji mingi ya kipato, hasa kwa walioajiriwa. Kutegemea mshahara pekee kama njia kuu ya kipato, ni hatari mno, kama ambavyo kila mtu amekuwa anaona (more…)

BIASHARA LEO; Usiogope Kuwasumbua Wateja…

By | September 11, 2017

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanatumia sababu za ajabu sana kuendesha biashara zao kwa uzembe. Moja ya sababu hizo ni kuogopa kuwasumbua wateja. Wapo wafanyabiashara ambao wamekuwa wanapoteza wateja kwenye biashara zao, kwa sababu wanaogopa kuwasumbua. Labda ni kumkumbusha mteja kuja tena kwenye biashara, wengi huona wakifanya hivyo mteja ataona ni kama (more…)