Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

2529; Mrefu halafu mfupi.

By | December 3, 2021

2529; Mrefu halafu mfupi. Kwenye ukurasa uliopita (2528), tumejifunza tamaa ya kutaka vingi kwa pamoja inavyokuwa kikwazo kwa wengi kufanya maamuzi. Watu wanachelewa kufanya maamuzi kwa sababu hawataki kukosa fursa nzuri zinazoweza kujitokeza baadaye na hilo linakuwa kikwazo kwao. Huo ni upande mmoja ambao watu wamekuwa wanatumia kukwepa kufanya maamuzi. (more…)

#SheriaYaLeo (33/366); Anachohitaji Menta.

By | December 3, 2021

#SheriaYaLeo (33/366); Anachohitaji Menta. Ili kujifunza kwa vitendo na uhalisia, unahitaji mtu ambaye tayari ameshafanikiwa kwenye kile unachotaka kufanikiwa ili awe menta wako. Ni kupitia menta huyo ndiyo utajifunza kwa uzoefu ambao yeye ameupitia mpaka kufika alipofika. Atakusaidia kuepuka makosa ambayo yeye alifanya ili usijicheleweshe. Ni muhimu sana kumpata aliyefanikiwa (more…)

2528; Kutaka vingi kwa pamoja.

By | December 2, 2021

2528; Kutaka vingi kwa pamoja. Hadithi tulizokuwa tunajifunza utotoni zilikuwa na masomo makubwa sana kuhusu maisha. Lakini kwa bahati mbaya sana tumekuwa hatuzipi uzito na hivyo kufanya makosa ambayo hadithi hizo zilikuwa zinatuasa tuyaepuke. Chukua hadithi ya sungura kualikwa kwenye sherehe mbili. Kwa ulafi wake akapanga asikose vyote. Hivyo akawa (more…)

#SheriaYaLeo (32/366); Jifunze kwa kufanya.

By | December 2, 2021

#SheriaYaLeo (32/366); Jifunze kwa kufanya. Ulipokuwa mdogo, wazazi na jamii ilikufundisha mambo mengi kuhusu maisha kupitia maelekezo na mifano. Ulipoenda shule ukafundishwa mambo mengine mengi kuhusu kazi na biashara kupitia maelekezo na mifano. Unapoingia kwenye dunia ya uhalisia, katika kuyaishi maisha na kufanya kazi au biashara, ndiyo unagundua yale uliyojifunza (more…)

2527; Kila suluhisho ni tatizo.

By | December 1, 2021

2527; Kila suluhisho ni tatizo. Kwenye maisha huwa tunapitia matatizo na changamoto mbalimbali. Hilo hutusukuna kutafuta suluhisho ili maisha yetu yaweze kwenda vile tunavyotaka. Tunachosahau au ambacho tunakuwa hatujui wakati tunatafuta suluhisho ni kwamba kila suluhisho huwa lina tatizo ndani yake. Ndiyo ni suluhisho la tatizo ambalo unalo, lakini ndani (more…)

#SheriaYaLeo (31/366); Chanzo cha nguvu zote.

By | December 1, 2021

#SheriaYaLeo (31/366); Chanzo cha nguvu zote. Usijaribu kuikwepa kazi ya kugundua kusudi na wajibu wa maisha yako kwa kudhani vitakuja kwako vyenyewe. Japo inaweza kutokea hivyo kwa baadhi ya watu, kuweza kujua kusudi na wajibu wa maisha yao mapema na kwa matukio ya kipekee, kwa wengj wetu hilo linahitaji kazi (more…)

2526; Mtego wa mateso.

By | November 30, 2021

2526; Mtego wa mateso. Haya maisha huwa yana mitego ya mateso ambayo usipoijua utaishi maisha ya kuteseka sana. Mitego hii haijaanza sasa, wanafalsafa wa kale waliielewa sana na wakawa na mafunzo ya kuwatahadharisha watu. Kuna mifano mikubwa miwili ya mafunzo ya kale yanayoonyesha mitego hii. Wa kwanza ni Promethus ambaye (more…)

#SheriaYaLeo (30/366); Amini kwenye mchakato.

By | November 30, 2021

#SheriaYaLeo (30/366); Amini kwenye mchakato. Unapoanza kufanya kitu chochote kile kipya kwako, unakutana na ugumu mkubwa. Unakua hujui mambo mengi kuhusu kitu hicho na hivyo unasumbuka sana mwanzoni. Unaweza kukata tamaa kwa kuona vitu ni vingi na vigumu, huwezi kupambana navyo. Kama utakata tamaa, utakuwa umeishia hapo na kushindwa kufikia (more…)

ONGEA NA KOCHA; Wewe Ni Mshindi, Third Door na Ernest Paschal.

By | November 29, 2021

Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi cha juma cha ONGEA NA KOCHA. Kwenye kipindi hiki unakwenda kupata yafuatayo; Moja ni somo la wewe ni mshindi, ambapo nimekushirikisha kwa kina namna ya kufikiri kama mshindi, kufuta kabisa mbadala na kupambana mpaka ufanikiwe. Mbili ni uchambuzi wa kitabu cha Third Door ambapo mwandishi ameshirikisha (more…)

2525; Mbadala Ndiyo Unaokuponza.

By | November 29, 2021

2525; Mbadala Ndiyo Unaokuponza. Kadiri unavyokuwa na machaguo mengi, ndivyo inavyokuwa vigumu kwako kuchukua hatua. Pale unapokuwa na mbadala wa chochote unachofanya, ukikutana na ugumu utakimbilia kwenye mbadala huo. Hiki ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya wengi, kuwa na mbadala kunawafanya wasikomae na kitu kimoja mpaka wakapata matokeo makubwa. Kujua (more…)