Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; MATATU YANAYOKUKWAMISHA…

By | March 13, 2021

Kutokujua hasa kile unachotaka, kutokujitoa hasa kupata unachotaka na kuwa na mbadala ni vikwazo vikubwa vitatu kwa mafanikio yako. Kama hujui kile unachotaka, kila mara utayumbishwa na wanayofanya wengine, ukiona wanafanya hiki na wewe unajaribu, wakifanya kile unajaribu pia. Mwisho wa siku unakuta muda umeenda na hakuna cha tofauti umepata. (more…)

2263; Kuwaangalia Wengine Ndiyo Kunakupoteza…

By | March 12, 2021

Mwekezaji bilionea Warren Buffett amewahi kusema kinachopelekea maanguko ya uchumi ni tabia ya watu kufuata kundi. Anasema watu wengi huwa hawawezi kutulia pale wanapoona kundi kubwa la watu likifanya kitu, huwa hawataki wapitwe, hivyo hukimbilia kufanya na kuishia kuanguka. Ndiyo maana watu wengi hununua hisa wakati zinapanda bei na kuziuza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUNA GHARAMA KUSIMAMIA UNACHOAMINI…

By | March 12, 2021

Mafanikio makubwa siyo rahisi kwa wengi kwa sababu yanahitaji msimamo. Na msimamo una gharama kubwa ambayo mtu anapaswa kuwa tayari kulipa. Je wewe upo tayari kulipa gharama kiasi gani ili kusimamia unachoamini? Maana dunia itatumia kila aina ya ushawishi na mateso kuhakikisha inakuangusha. Lazima uwe umejitoa kweli kweli kama unataka (more…)

2262; Mtu Asiye Na Madhaifu…

By | March 11, 2021

Kila mtu huwa ana madhaifu yake, ni wale wanaoyatambua na kuhakikisha hayawi kikwazo kwao ndiyo hufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Wale wanaoyakataa madhaifu yao huwa ni kiburi tu walichonacho au ujinga wa kutokujitambua, lakini huwa hawafanikiwi. Kwa sababu hata wapate fursa nzuri kiasi gani, madhaifu yao huwa kikwazo. Kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MPAKA MWISHO…

By | March 11, 2021

Mafanikio huwa hayaji kwa kuanza kufanya vitu na kuishia njiani, bali huja kwa kufanya vitu mpaka mwisho. Japo haitakuwa rahisi, japo utakutana na vikwazo na changamoto, huwezi kufanikiwa kama utaishia njiani. Chochote unachochagua kufanya, amua kukifanya mpaka mwisho wake, kamwe usikubali kuishia njiani, pambana kwa kila namna uendelee kufanya. Moja (more…)

2261; Tumia Thamani Badala Ya Uhaba…

By | March 10, 2021

Utajiri wa zamani ulijengwa kwenye misingi ya uhaba, kwamba rasilimali muhimu ni chache, wachache wanazihodhi na kunufaika kwa kiwango kikubwa. Hivyo ndivyo zama za kilimo zilivyofanya kazi, wachache walimiliki mashamba na wengi kuwa wafanyakazi au watumwa kwenye mashamba hayo. Kadhalika zama za viwanda zikarithi hilo, kumiliki kiwanda ilihitaji mtaji mkubwa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIPO UNACHOWEZA KUFANYA…

By | March 10, 2021

Haijalishi unapitia hali gani, kuna kitu unachoweza kufanya. Usikate tamaa na kukosa matumaini kwamba hakuna unachoweza kufanya. Martin Luther King amewahi kusema kama huwezi kuruka kimbia, kama huwezi kukimbia tembea na kama huwezi kutembea tamaa, fanya chochote kuhakikisha unasonga mbele. Hivyo ndivyo unapaswa kukabili kila linalokuja kwenye maisha yako, kwa (more…)

2260; Kutaka Fedha Kusikupe Upofu…

By | March 9, 2021

Uliwahi kufanyika utafiti kwa wale wanaofanya utapeli. Utafiti huo ulitaka kujua iwapo watu wanaofanya hivyo hawasutwi nafsi zao kwa kuwaibia na kuwatapeli wengine. Mmoja wa watu waliohojiwa kwenye utafiti huo alitoa jibu ambalo liliwafanya watafiti wapate mtazamo ambao hawakuwa nao awali. Mtu huyo aliwaambia ni kweli tabia ya utapeli inamuumiza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; LINDA UTULIVU WA AKILI YAKO…

By | March 9, 2021

Watu wakitaka kuyavuruga maisha yako, wanaanza kwa kuvuruga akili yako. Watu wakitaka kukuibia au kukutapeli, wanaanza kwa kuivuruga akili yako. Na hata wale wanaotaka kukutumia kwa manufaa yao, wanahakikisha wamevuruga akili yako kwanza. Akili yako ni rasilimali muhimu na yenye nguvu kubwa ndiyo maana ni kitu cha kwanza kushambuliwa. Kila (more…)

2259; Linda Juhudi Unazoweka Sasa Unufaike Nazo Baadaye…

By | March 8, 2021

Asili ina kanuni zake nyingi, huwezi kupanda mbegu na kuivuna hapo hapo ukaila. Lazima uwe na subira, lazima uipe mbegu hiyo muda, ikue, izae mbegu nyingi zaidi ndipo uvune na kuweza kula. Sasa pata picha umekuwa unaona shamba liko mahali, lina rutuba nzuri na hakuna anayelilima. Unaona unaweza kutumia shamba (more…)