Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1589; Usiuze Maisha Yako, Unayapata Mara Moja Pekee…

By | May 8, 2019

Maisha ni kitu ambacho kila mtu anakipata mara moja, baada ya miaka michache yanayeyuka na hakuna mwenye uhakika nini kinatokea baada ya maisha haya kuwa yameisha. Dini na falsafa zina nadharia tofauti, lakini kwa kuwa hakuna aliyewahi kwenda akarudi, tunabaki gizani kwamba nini kinatokea baada ya kuwa tumeondoka kwenye haya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UZURI NA UBAYA UPO KWENYE MAAMUZI YAKO…

By | May 8, 2019

“Where is Good? In our reasoned choices. Where is Evil? In our reasoned choices. Where is that which is neither Good nor Evil? In the things outside of our own reasoned choice.” —EPICTETUS, DISCOURSES, 2.16.1 Hongera sana rafiki yangu mpendwa kwa nafasi hii nyingine ambayo umeipata leo. Ni nafasi ya (more…)

1588; Mipango Ni Mwongozo Na Siyo Msaafu….

By | May 7, 2019

Ili kufika kule unakotaka kufika kwenye maisha yako, unahitaji kuwa na mipango ya kukufikisha pale. Mipango ni muhimu sana, kwa sababu hakuna chochote kinachotokea kama muujiza. Lazima kifanyiwe kazi kwa mpango unaoeleweka. Lakini mipango imekuwa kikwazo kwa wengi kupata kile wanachotaka. Kwa sababu wanapoweka mipango, wanataka kila kitu kiende kama (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JINSI YA KUWA NA SIKU BORA…

By | May 7, 2019

“God laid down this law, saying: if you want some good, get it from yourself.” —EPICTETUS, DISCOURSES, 1.29.4 Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu. Tumeipata nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA (more…)

1587; Mchezo Wa Maisha Ni Kugeuza Kila Kitu Kuwa Zawadi…

By | May 6, 2019

Unaweza kuyaishi maisha yako kwa mitazamo miwili, Moja kila kitu ni kibaya kwako, na hapa kila kinachotokea utaona ubaya ndani yake. Ukifukuzwa kazi unaona kuna wabaya wako wamefanya ufukuzwe. Mahusiano uliyonayo yakivunjika unaona upande wa pili ulikuwa na matatizo. Ukianzisha biashara na ikafa unaona uchumi ni mgumu au huna bahati (more…)

1585; Ufunguo Na Kufuli…

By | May 4, 2019

Inapokuja kwenye mawazo ya kuanza biashara au ujasiriamali, watu hukabili hilo kwa mitazamo miwili, ambayo inaendana na ufunguo na kufuli. Wapo ambao wanaanza kutengeneza ufunguo, kisha wanazunguka kutafuta kufuli ambalo litakubali kufunguliwa na ufunguo huo. Hili ni zoezi gumu sana, kwa sababu hata ufunguo uwe mzuri kiasi gani, itakuchukua muda (more…)