Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1594; Siku Haitengenezi Hali, Bali Hali Ndiyo Inatengeneza Siku…

By | May 13, 2019

Rafiki yangu mpendwa, Imekuwa ni mazoea kwa wengi kusingizia siku kwamba ndiyo zinatengeneza hali ambazo wanazo. Labda ni jumatatu ambayo mtu anajisikia vibaya kwenye kazi zake na hapo kusingizia kwamba jumatatu siyo nzuri, na kuipa majina kama ‘blue monday’ na mengineyo. Au ni ijumaa ambayo mtu anajisikia vizuri sana kwa (more…)

1593; Ijue Nguvu Ya Maneno Unayoyatumia Kila Siku…

By | May 12, 2019

Tumekuwa tunatumia maneno kwa mazoea na huwa hatuchukui hata sekunde chache kupima nguvu ya maneno hayo. Kinachotokea ni kwamba baadhi ya maneno ambayo tumekuwa tunayatumia yamekuwa kikwazo kwetu kupiga hatua. Kwa kutumia baadhi ya maneno, tumekuwa tunajiwekea ukomo wenyewe. Na baadhi ya maneno yanatupa hamasa ya kupiga hatua zaidi, yanatuonesha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WEMA NI JIBU SAHIHI MARA ZOTE….

By | May 12, 2019

“Kindness is invincible, but only when it’s sincere, with no hypocrisy or faking. For what can even the most malicious person do if you keep showing kindness and, if given the chance, you gently point out where they went wrong—right as they are trying to harm you?” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, (more…)

1592; Hatua Ya Kwanza Ya Kuikabili Hofu Ni Hii…

By | May 11, 2019

Hofu imekuwa kikwazo kwa wengi kupiga hatua kwenye maisha yao na kufanikiwa zaidi. Japo wengi hawatakiri kwamba kinachowazuia ni hofu, lakini kwa hakika hofu ndiyo kikwazo kwa wengi, na hata kwako pia. Fikiria vitu vyote vikubwa ambavyo umewahi kupanga kufanya na hukufanya, fikiria malengo yote makubwa ambayo umewahi kujiwekea na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HATIA NI MBAYA KULIKO GEREZA…

By | May 11, 2019

“The greatest portion of peace of mind is doing nothing wrong. Those who lack self-control live disoriented and disturbed lives.” —SENECA, MORAL LETTERS, 105.7 Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu. Tumeipata fursa nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora (more…)

1591; Chochote Kinachokusumbua Umekitengeneza Wewe Mwenyewe…

By | May 10, 2019

Tuseme labda kuna mahali unataka kuwahi, umeshachelewa na hivyo upo kwenye haraka ya kufika ndani ya muda, unasumbuka sana kuhakikisha unawahi. Unafikiri nani ametengeneza tatizo hilo? Vipi kama ungewahi mapema zaidi je ungekuwa kwenye masumbuko hayo? Au pata picha una kazi ambayo inabidi uikamilishe kwa haraka, huna muda kabisa na (more…)

1590; Hakuna Tatizo Linaloondoka Kwa Kulikimbia…

By | May 9, 2019

Mbuni anapokutana na tatizo ambalo hawezi kulikabili, huwa anafukia kichwa chake kwenye mchanga. Kama vile asipoliona tatizo basi litaondoka lenyewe. Japokuwa sisi binadamu tuna uwezo mkubwa kuliko mbuni, lakini inapokuja kwenye matatizo makubwa, hatutofautiani sana na ndege hao. Watu wengi wanapokutana na matatizo makubwa, huwa wanajaribu kuyakimbia au kujificha, wakiamini (more…)