Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1549; Sauti Hasi Iliyopo Ndani Yetu…

By | March 29, 2019

Kila mtu ana sauti hasi ambayo ipo ndani yake. Hii ni sauti ambayo kila mara inamkumbusha madhaifu yake, makosa yake, na jinsi ambavyo hawezi kufanya makubwa kama alivyopanga. Weka mipango yoyote mikubwa na kuna kisauti ndani yako kitaanza kukusumbua, kitakuambia huwezi, kitakuonesha wengine ambao walijaribu wakashindwa. Kuna wakati kisauti hiki (more…)

1548; Kazi, Maisha Na Burudani…

By | March 28, 2019

Mtu mmoja amewahi kumuuliza Mjasiriamali na Bilionea Richard Branson ambaye anamiliki makampuni zaidi ya 400 kwamba anawezaje kuwa na mlinganyo wa kazi, maisha na burudani, anatengaje muda wa kazi, muda wa maisha na hata muda wa burudani? Richard Branson kwa mshangao aliuliza, kwani vitu hivyo vimetenganishwa? Si vinapaswa kuwa kitu (more…)

1547; Unahitaji Muda Au Unajificha?

By | March 27, 2019

Waswahili wanasema mambo mazuri hayahitaji haraka na pia wanaendelea kusisitiza haraka haraka haina baraka. Ni kweli misemo hii miwili ina ukweli mkubwa ndani yake, kwamba ili upate mambo mazuri, lazima uwe na subira. Vitu vizuri kwenye maisha vinahitaji muda zaidi. Kuna vitu hata kama una uwezo wa kuvifanya kwa haraka, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; LIPIA KITU KULINGANA NA THAMANI YAKE…

By | March 27, 2019

“Diogenes of Sinope said we sell things of great value for things of very little, and vice versa.” —DIOGENES LAERTIUS, LIVES OF THE EMINENT PHILOSOPHERS, 6.2.35b Ni siki nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora (more…)

1546; Kitu Kikubwa Kinachokusukuma Zaidi…

By | March 26, 2019

Kikwazo cha kwanza cha mafanikio ya mtu kinaanzia ndani yake. Siyo kwenye mazingira, hali ya uchumi, kazi au biashara mtu anayopata ndiyo kikwazo, bali kikwazo kipo ndani ya mtu mwenyewe. Watu wengi wamekwama pale walipo sasa, kwa sababu kwa ndani wameshakubaliana na hali hiyo na hawaoni picha kubwa na nzuri (more…)

1545; Kuwa Huru Na Kufikiri Upo Huru…

By | March 25, 2019

Kuwa huru na kufikiri upo huru ni vitu viwili tofauti kabisa. Watu wengi wanaojiona wapo huru, ni kufikiri kwao kwamba wapo huru ndiyo kunawapa matumaini. Lakini kwa uhalisia hawapo huru, na hawajui kama hawapo huru, kitu kinachofanya hali yao izidi kuwa mbaya zaidi. Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuhalalisha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UHURU NI BURE…

By | March 25, 2019

“. . . freedom isn’t secured by filling up on your heart’s desire but by removing your desire.” —EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.175 Ni siku nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu. Tumepata nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU (more…)