Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1079; Huwezi Kumfundisha Yeyote Somo, Siyo Kwa Namna Unayofikiri Wewe…

By | December 14, 2017

Wanasema kwamba njia bora ya kulipa kisasi kwa watu waliokusumbua au kukukwamisha kwa namna yoyote ile, ni kuwa na mafanikio makubwa sana. Tumekuwa tunafikiri hivi kwamba kama kuna mtu anatusumbua, amewahi kutunyanyasa kwa namna yoyote ile, basi tukikazana na kufanikiwa tutamfundisha somo. Tutamwonesha kwamba alikosea sana kutufanyia kile alichofanya. Lakini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKATILI NI ZAO LA UDHAIFU…

By | December 14, 2017

All cruelty springs from weakness. – Lucius Annaeus Seneca Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda (more…)

UKURASA WA 1078; Uwezo Wa Kufikia Maamuzi Unazidi Kuwa Adimu…

By | December 13, 2017

Kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo uwezo wa watu kufikia maamuzi yao wenyewe unavyozidi kuwa mgumu. Hii inatokana na wingi wa machaguo, wingi wa maarifa na taarifa na pia wingi wa ushauri ambao mtu anaweza kupata juu ya jambo lolote lile. Unapotaka kufanya jambo lolote na ukaanza kutafuta taarifa na maarifa, utayapata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ZAWADI YA LEO….

By | December 13, 2017

Each day provides its own gifts. – Marcus Aurelius Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Ni siku nyingine nzuri sana kwetu ambapo tumepata nafasi ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa (more…)

UKURASA WA 1077; Mambo Madogo Yasiyo Na Hatia Yanapoanza Kuzalisha Hatia Kubwa…

By | December 12, 2017

Kuna mambo madogo madogo ambayo tunayafanya kila siku, ambayo hayana hatia kabisa, yaani ni mambo ya kawaida mno, ambayo haitujii kwenye akili zetu kwamba yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye maisha yetu. Kwa mfano kuianza siku yako kila siku kwa kusikiliza habari na matukio mbalimbali ambapo nyingi huwa ni hasi. (more…)

UKURASA WA 1076; Mafanikio Ni Magumu, Lakini Umasikini Ni Mgumu Zaidi…

By | December 11, 2017

Ukweli ni kwamba, mafanikio ni magumu, kuyatafuta mafanikio ni safari ngumu ambayo imejaa vikwazo na kukatishwa tamaa kwenye mambo mengi. Lakini hata unapoyapata mafanikio, siyo kwamba mambo yanakuwa rahisi, badala yake yanazidi kuwa magumu zaidi. Changamoto ndiyo zinazidi kuwa kubwa, na hatari ya kupoteza chochote ulichonacho inazidi kuwa kubwa. Kwa (more…)

UKURASA WA 1075; Siyo Namba, Ni Watu…

By | December 10, 2017

Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kitu kinapimwa kwa namba. Kuanzia fedha, kiwango cha kazi tunachofanya na hata idadi ya watu tunaowahudumia au kuwauzia. Kipimo kikubwa sasa kimekuwa ni namba, na kadiri namba inavyokuwa kubwa, ndivyo tunavyoona tumefanikiwa. Kadiri kiasi cha fedha kinavyokuwa kikubwa, ndivyo tunavyoona tumefanikiwa. Kadiri idadi ya watu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAJENGEE MISINGI, SIYO KUWAPA FEDHA PEKEE…

By | December 10, 2017

Be careful to leave your sons well instructed rather than rich, for the hopes of the instructed are better than the wealth of the ignorant. – Epictetus Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri na ya kipekee sana ya leo. Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza (more…)