Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1074; Kwa Nini Bado Kuna Fursa Kubwa Kwenye Kila Aina Ya Kazi Au Biashara…

By | December 9, 2017

Tabia ya binadamu ni moja, ukiwa kwenye kazi fulani, unaona kama kazi hiyo haina fursa na kazi za wengine ndiyo zina fursa zaidi na manufaa zaidi. Kadhalika kwenye biashara, mtu anaweza kuwa kwenye biashara fulani, lakini akiwaangalia wengine ambao wapo kwenye biashara nyingine, anaona wana manufaa zaidi kuliko yeye. Lakini (more…)

UKURASA WA 1073; Darasa La Kushindwa Kwako….

By | December 8, 2017

Mwandishi Brian Tracy kwenye kitabu chake cha THE PSYCHOLOGY OF SUCCESS anasema kwamba watu ambao hawajafanikiwa wana tatizo kubwa sana. Wakipata kitu wanaona ni bahati, na wakishindwa au kukosa kitu basi wanaona ni bahati mbaya au kisirani kwao. Kwa njia hiyo, hawajifunzi na wala hawapati mbinu bora za kupata kile (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ZUNGUKWA NA WANAOKUVUTA KWENDA JUU…..

By | December 8, 2017

The key is to keep company only with people who uplift you, whose presence calls forth your best. – Epictetus Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku ya leo, nafasi nyingine nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa. Kama kuna chochote ambacho jana ulisema utafanya kesho, (more…)

UKURASA WA 1072; Usiangalie Kipato Pekee, Angalia Maisha Unayotengeneza Pia…

By | December 7, 2017

Watu wengi wanapochagua kazi au biashara ya kufanya, huanza kuangalia ni kiasi gani cha fedha wanaweza kupata. Na kama kuna machaguo mengi ya vitu wanaweza kufanya, wengi huchagua kile wanachoona kitawalipa zaidi. Wapo wengine wanasema wazi kabisa kwamba wapo tayari kufanya chochote kama kinawaingizia fedha. Hali kama hii ni kawaida (more…)

UKURASA WA 1071; Acha Kujitengenezea Mateso…

By | December 6, 2017

Kusudi la maisha halijawahi kuteseka, Ni kweli changamoto na vikwazo vingi vipo kwenye safari ya maisha, lakini havipaswi kuwa chanzo cha mateso. Ukiiangalia dunia jinsi ilivyo, hakuna namna yoyote imejipanga kuwatesa watu. Lakini watu wanateseka kila siku, kwa sababu wanachagua kujitengenezea mateso wao wenyewe. Yaani ni sawa na kuwe na (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ishi Maisha Yako Na Waruhusu Wengine Kuishi Maisha Yao.

By | December 5, 2017

KITABU; Meditations / Marcus Aurelius. UKURASA; 38 – 47. Ni tabia yetu binadamu kutaka watu wawe kama tunavyotaka kuwa sisi. Kutaka wafanye kile tunachotaka wafanye na hata kufikiri vile tunavyotaka sisi wafikiri. Marcus anatuambia huku ni kupoteza muda wetu, kwa sababu hatuwezi kuwafanya wengine wawe kama tunavyotaka siai. Wala hatupaswi (more…)