Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; SULUHISHO LA MUDA MFUPI…

By | September 16, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, ambapo tunakwenda kufanya makubwa na kuweza kupata makubwa leo na kila (more…)

UKURASA WA 990; Raha Na Furaha Ipo Kwenye Mchakato Na Siyo Matokeo…

By | September 16, 2017

Moja ya kazi kubwa ambazo nimekuwa najitahidi kufanya ni kupindua kila uongo ambao jamii imetujaza na kutufanya tuamini kuhusu maisha. Na kwa kujua na kupindua uongo huo, tunaujua ukweli na ukweli unatuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio. Leo nataka tuangalie uongo ambao kila mtu alishapandikizwa na tunaendelea kupandikizwa (more…)

Jinsi ya kujijengea udhibiti binafsi (self-control).

By | September 16, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 45 – 55 Jinsi ya kujijengea udhibiti binafsi (self-control). Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, watu wenye udhibiti binafsi wanakuwa na maisha bora na yenye mafanikio kuliko wale wanaokosa udhibiti binafsi. Wanafalsafa wa (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Mfumo Wa Biashara Moja Kusimama Kabla Hujaenda Nyingine…

By | September 15, 2017

Tunaishi kwenye dunia ya wingi, kila mtu anapenda kuwa na vitu vingi. Kwa sababu dunia inachanganya wingi na mafanikio. Kwamba mwenye vingi ndiye aliyefanikiwa, asiyekuwa na vingi basi ameshindwa. Hii ni falsafa mbovu sana kwenye kila eneo la maisha. Lakini inakuwa mbovu zaidi inapoingia kwenye biashara. Wapo watu wanapima mafanikio (more…)

UKURASA WA 989; Weka Nguvu Zako Kwenye Kile Unachoweza Vizuri…

By | September 15, 2017

Unapoanza kufanya kitu chochote kwenye maisha, na kikatoa majibu mazuri, hutakosa watu wa kukushauri ni namna gani unaweza kuboresha zaidi. Watu watakupa mbinu na njia za kuweza kufanya zaidi. Sasa ushauri na njia nyingi unazopewa huwa zinakuondoa kwenye kusudi lako la mwanzo. Wengi wanaokuwa wanakushauri wanafanya hivyo kwa kuangalia vitu (more…)

HALI YETU YA UDHIBITI JUU YA MAMBO YANAYOTUTOKEA.

By | September 15, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 33 – 45. HALI YETU YA UDHIBITI JUU YA MAMBO YANAYOTUTOKEA. Mambo yote yanayotokea kwenye maisha yetu tunaweza kuyagawa katika makundi mawili. 1. Mambo ambayo yapo chini ya udhibiti wetu, haya (more…)

BIASHARA LEO; Jua Eneo Hili La Biashara Yako Linalokurudisha Nyuma.

By | September 14, 2017

Biashara yenye mafanikio inaendeshwa kwa mfumo. Mfumo wa biashara unakuwa na vipengele mbalimbali kama mauzo, masoko, uzalishaji, usimamizi na kadhalika. Kwa njia hii ya mfumo, mmiliki wa biashara anaweza kuiendesha vizuri biashara yake na kwa mafanikio makubwa sana. Lakini mifumo yote ina changamoto kubwa moja, eneo moja likiwa na changamoto, (more…)

#KURASA_KUMI; Nini maana ya maisha mazuri?

By | September 14, 2017

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO. KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems. Kurasa 21 – 31. Nini maana ya maisha mazuri? Swali moja ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kuhusu maana ya maisha mazuri. Kumekuwepo mijadala mingi kuhusu nini maana ya maisha mazuri na (more…)