Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Anza Kuiua Biashara Yako Wewe Mwenyewe….

By | June 18, 2017

Ukweli ni kwamba, watu wamekuwa wanaua biashara zao wao wenyewe, bila ya kujua kama wanafanya hivyo. Na hili linakuwa changamoto kwao kwa sababu wanakuja kustuka mambo yakiwa yameshaharibika sana. Wateja wameshaondoka, hasara imeshakuwa kubwa na hakuna namna ya kuiokoa tena biashara ile. Mimi ninachotaka kukuambia leo ni uanze kuiua biashara (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UPO TAYARI KWA MIAKA MITANO?

By | June 18, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Hii ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tunakwenda kutafakari kuhusu (more…)

UKURASA WA 900; Maisha Yako Ni Kazi Inayoendelea….

By | June 18, 2017

Kabla hujapata chochote ambacho unakitaka sana, huwa unafikiri ukishakipata basi ndiyo umemaliza kila kitu. Lakini unapokipata ndiyo unagundua kumbe ni mwanzo kabisa wa maisha kuwa bora kwako. Mfano kabla hujamaliza masomo, unaona ukimaliza masomo basi ndiyo umemalizana na changamoto. Lakini unapomaliza ndiyo unagundua unahitaji kujifunza zaidi hata ya ulivyokuwa unajifunza (more…)

BIASHARA LEO; Urahisi Wa Biashara Na Thamani Ya Biashara…

By | June 17, 2017

Biashara rahisi kufanya, thamani yake ni ndogo, na biashara ngumu kufanya, thamani yake ni kubwa. Kwa maneno mengine, biashara rahisi kufanya faida yake ni kidogo, na biashara ngumu kufanya faida yake ni kubwa. Watu wengi wamekuwa wakikimbilia kutafuta biashara rahisi kufanya, biashara ambayo haitawapa stress, biashara ambayo wana uhakika wa (more…)

UKURASA WA 899; Endesha Maisha Yako Kama Biashara….

By | June 17, 2017

Msingi mkuu wa biashara ni huu; FAIDA = MAUZO – MANUNUZI NA MATUMIZI. Biashara inapata faida, na hivyo kuendelea pale inapotengeneza faida, na faida inapatikana pale mauzo yanapokuwa makubwa kuliko manunuzi na gharama za biashara. Kadhalika kwenye maisha yako, ili uweze kuwa na maisha bora yenye uhuru wa kifedha, mapato (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Viwili Vinavyojenga Biashara Yenye Mafanikio.

By | June 16, 2017

Biashara zote zenye mafanikio, zinajengwa kwenye vitu viwili vikuu; Bidhaa au huduma nzuri. Wateja wanaojirudia. Unahitaji kuwa na bidhaa au huduma nzuri, siyo nzuri kwa sura, bali nzuri kwa uhitaji wa watu. Kile unachouza lazima kiwe kinatatua tatizo au kutimiza mahitaji ya wateja wako. Kiwe na thamani kwao inayowafanya kuwa (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MUDA UPO WA KUTOSHA….

By | June 16, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Ni kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MUDA (more…)

Njia Tano (05) Bora Za Kutoa Mafunzo Kwa Wafanyakazi Wa Biashara Yako.

By | June 16, 2017

Huwezi kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa wewe peke yako. Unahitaji msaada wa watu wengine wengi ambao watafanyia kazi majukumu muhimu kwenye biashara yako. Hivyo kuajiri ni kitu ambacho kila mfanyabiashara akifikirie hata kama biashara ni ndogo kabisa. Lakini pia kuajiri pekee hakutoshi kukuletea mafanikio kwenye biashara yako. Bali unahitaji kutoa (more…)

UKURASA WA 898; Kutoroka Siyo Suluhisho….

By | June 16, 2017

Kuna wakati tunakutana na changamoto au matatizo ambayo yanaomekana ni makubwa kuliko uwezo wetu. Kila tukiyaangalia tunaona hakuna namna tunaweza kupambana nayo. Sasa kwa kuwa akili yetu haipendi tuteseke, inachofanya ni kutafuta njia ya kutoroka. Na hapo tunaona mengi ya kufanya, lakini siyo kulikabili tatizo. Tunaanza kuangalia nani kasababisha mpaka (more…)

UKURASA WA 897; Hamasa Inapatikana Hapa….

By | June 15, 2017

Ili kufanikiwa, lazima tufanye mambo ambayo wengine hawapo tayari kufanya, na hata sisi wenyewe, hatujawahi kufanya hapo awali. Mambo haya siyo rahisi, na ndiyo maana wengi hawafanyi. Hivyo kuweza kufanya mambo haya magumu na makubwa, tunahitaji sana hamasa. Lazima tuwe na hamasa ya kuweza kufanya hata pale ambapo hatuoni urahisi (more…)