Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 896; Acha Kutorokea Kwenye Vitabu…

By | June 14, 2017

Kusoma vitabu, au kujifunza ni hitaji la msingi kabisa la mafanikio yetu. Hatuwezi kufanikiwa kama tunafanya mambo yale yale na kwa uelewa ule ule. Tunahitaji kujifunza mambo mapya na njia bora wanazotumia wengine kuwa bora zaidi. Na hapa ndipo umuhimu wa vitabu unapokuja. Ni muhimu sana kusoma vitabu, vya aina (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; TATUA TATIZO….

By | June 13, 2017

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo rafiki. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTATUA TATIZO…. Dunia ina matatizo, Watu wana (more…)

UKURASA WA 895; Uhakika Wa Asilimia 100…

By | June 13, 2017

Hakuna jambo lolote kwenye maisha yetu ambalo tuna uhakika nalo kwa silimia mia moja, hivyo kwa kila tunachofanya, kuna nafasi ya kupata kile tunachotaka kupata, na nafasi ya kukosa. Japo unaweza kuwa unataka sana kitu fulani kitokee, na ukafanya kila ambacho unapaswa kufanya, bado matokeo yanaweza kuwa tofauti na usiweze (more…)

UKURASA WA 894; Kushindana Na Watu Bilioni Saba…

By | June 12, 2017

Unahitaji kuwa bora zaidi kwenye kile ambacho unakifanya, bora kabisa duniani, kwa kuweza kukifanya kwa namna ambavyo hakijawahi kufanywa na yeyote duniani. Lakini changamoto ni kwamba, dunia ina watu zaidi ya bilioni saba, na karibu wote wanakazana kufanya vitu vile vile ambavyo vinafanana. Hili linapelekea ushindani kuwa mkali, watu bilioni (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NEXT MOVE…

By | June 11, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NEXT MOVE, au tukio linalofuata. Iko (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Dawa Ya Msongo Wa Mawazo Ni Hii.

By | June 11, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunajifunza mbinu za kifalsafa za kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi, yenye mafanikio na furaha. hakuna popote tunapofundishwa falsafa ya aina hii, hivyo inabidi tuitengeneze wenyewe na kuweza kuiishi ili maisha yetu yaende (more…)

UKURASA WA 893; Kama Huwezi Kubadili Unachofanya, Badili Hichi…

By | June 11, 2017

Katika safari ya maisha ya mafanikio, kile unachofanya, kinahusika sana kwenye mafanikio yako. Na wengi wamekwama kufanikiwa kwa sababu kile wanachofanya kinawazuia. Kile wanachofanya, iwe ni kazi, biashara au chochote, kinakuwa kikwazo kwao kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao. Na sababu kuu ni kwamba wengi huona kama wanapita tu. Huwa (more…)