Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

💥#TAFAKARI IANZE SIKU KWA SALAMU CHANYA.

By | June 2, 2017

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio, Hongera kwa siku hii nzuri sana ya leo. Leo ni siku ya kipekee sana kwetu, tunayo nafasi ya kwenda kufanya makubwa na tutegemee kupaga matokeo bora kutokana na juhudi kubwa tulizoweka. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kuianza siku na maneno chanya. Tunaishi kwenye jamii (more…)

UKURASA WA 883; Kushindwa Ni Ushindi…

By | June 1, 2017

Hakuna ushindi mkubwa kwenye maisha, kama kushindwa. Najua unaweza kuuliza hilo linawezekanaje, inawezekanaje kushindwa kwako kuwe ushindi, au ni kujidanganya na kujibembeleza? Na mimi nitakujibu kwa sababu zifuatazo; Unaposhindwa, maana yake umejaribu kitu, umefanya kabisa na siyo kwamba umekaa na kupanga tu. Pamoja na hofu zote, umekaa chini na kufanya (more…)

UKURASA WA 882; Wewe Ni Kazi Ya Sanaa…

By | May 31, 2017

Kwenye ukurasa wa 881 jana nilikuambia kitu kimoja, kwamba kabla hujawa bora kwenye jambo lolote unalofikiria, iwe ni kazi, biashara au uongozi, unahitaji kuwa bora wewe kwanza. Leo nakwenda kukupa sehemu nyingine muhimu ya hilo la kuwa bora wewe kwanza, ambalo ni wewe ni kazi ya sanaa. Kabla sijaendelea kwanza (more…)

NG’ANG’ANA NA KATAA; Njia Pekee Ya Kuweza Kufanya Makubwa Kwenye Zama Hizi Za Usumbufu Wa Hali Ya Juu.

By | May 30, 2017

Hakuna ambaye hapendi kufanya mambo makubwa kwenye maisha yake. Na kuonesha ni namna gani tumejitoa kufanya makubwa, tunapanga kabisa kila tunachotaka kufanya na kuona wapi tunapotaka kufika. Lakini hii ni sehemu rahisi ya kufika tunakotaka, tunaweza kusema ni asilimia moja pekee. Sehemu kubwa, ile asilimia 99, inatokana na juhudi tunazoweka (more…)

UKURASA WA 881; Anza Kuwa Bora Wewe Kwanza…

By | May 30, 2017

Kila mtu kuna vitu ambavyo anataka kuwa bora kwenye maisha yake na shughuli zake. Labda unataka kuwa baba/mama bora kwa watoto wako. Au unataka kuwa mke/mume bora kwa mwenza wako. Huenda unataka kuwa mwajiriwa bora kwa mwajiri wako, au mwajiri bora kwa wafanyakazi wako. Huenda unataka kuwa mfanyabiashara bora kwa (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Usichanganye Falsafa, Chagua Moja Na Itumie Vizuri.

By | May 28, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu nyingine ya falsafa mpya ya maisha ambapo tunajenga falsafa mpya ya maisha yetu ili kuweza kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Kwenye jamii zetu, huwa kuna pande mbili ambazo mara zote zinakinzana, na tunaweza kusema ni sheria ya (more…)