Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 879; Tofauti Ni Falsafa…

By | May 28, 2017

Watu waliofanikiwa wana masaa 24 kwenye siku yao, muda ambao hata wengine pia wanao kwenye siku zao. Watu waliofanikiwa wanafanya kazi na biashara ambazo wapo wengine wengi pia wanaozifanya, lakini wengi hawajafanikiwa. Je kuna nini hapa, kipi kimejificha? Tumekuwa tunaona mengi, kama kuweka juhudi kwenye kazi, kuwa na maono makubwa (more…)

UKURASA WA 878; Wape Watu Suluhisho…

By | May 27, 2017

Bill Cosby amewahi kunukuliwa akisema; hajui ufunguo wa mafanikio, ila anajua ufunguo wa kushindwa ambao ni kujaribu kumridhisha kila mtu. Watu wengi wamekuwa wanapenda kuwaridhisha wengine, ili waonekane wema, wakijua kufanya hivyo ndiyo watakubalika zaidi na kuweza kufanikiwa kwenye lolote wanalotaka. Huo siyo ukweli hata kidogo. Kujaribu kumridhisha kila mtu, (more…)

UKURASA WA 877; Dunia Inaendeshwa Kwa Hisia…

By | May 26, 2017

Japokuwa tafiti nyingi zinafanywa na data kupatikana kujua vitu gani vinawafanya watu kuchukua maamuzi fulani, labda kununua au kukubali kitu fulani, kipo kitu kimoja ambacho kinaongoza maamuzi ya watu wengi duniani. Kitu hicho ni hisia. Hisia zinaendesha dunia, na ndiyo maana utaona vitu kama mapenzi, chuki na wivu vinatawala maamuzi (more…)

💥 #GHAHAWA ☕ ☕; UNA UHAKIKA HULINGANISHI?

By | May 25, 2017

Habari za siku yako ya leo rafiki? Je yapi makubwa uliyofanya leo? Na zipi changamoto zimekufanya ujifunze zaidi? Usisahau kupitia haya kabla hujamaliza siku hii nzuri. Karibu kwenye #GHAHAWA ☕ ☕ jioni ya leo, Kupitia ghahawa tunachangamsha akili zetu ili kuweza kufikiri sawasawa na kuacha kufanya makosa yanayotugharimu. Leo nianze (more…)

Mambo 31 Niliyojifunza Kwenye Miaka 31 Ya Forbes Kufuatilia Mabilionea.

By | May 25, 2017

Jarida la Forbes limejizolea umaarufu kwa utaratibu wake wa kutoa orodha ya mabilionea wa dunia kila mwaka. Mwaka huu 2017 limetoa orodha ya mabilionea ambapo kwa sasa wapo mabilionea 2,043 ambapo ni ongezeko la asilimia 13 kutoka idadi ya mabilionea mwaka 2016 ambao walikuwa 1,810. Utajiri wa mabilionea hao kwa (more…)

UKURASA WA 876; Kuhusu Kupambana, Kushindana Na Kubishana…

By | May 25, 2017

Dunia haitakuacha ufanye chochote unachotaka bila ya kukusumbia, hivyo kuna wakati unahitaji kupambana, kushindana na kubishana. Mapambano hayo inabidi yawe kwenye kile unachofanya, na siyo kwa watu. Kwa sababu, kupambana, kushindana na kubishana na watu, kunakuwa na madhara makubwa kwako wewe mwenyewe, hata kama utashinda. Lakini watu hawatakuacha hivi hivi, (more…)

💥 #GHAHAWA ☕ ☕; MAMLAKA ZINAWEZA KUKUPOTOSHA…

By | May 24, 2017

Hongera kwa siku hii nzuri ya leo rafiki. Umeshinda mengi na kujifunza mengi siku ya leo. Hakikisha unakwenda kuyafanyia yale uliyojifunza ili uweze kuwa bora zaidi. Karibu kwenye #GHAHAWA ☕ ☕ jioni ya leo, tuchangamshe akili zetu kwa kutikisa fikra zetu kidogo. Yapo maamuzi mengi ambayo tumekuwa tunafanya bila ya (more…)

UKURASA WA 875; Neno Linalofuata Baada Ya Lakini, Linapinga Lililotangulia Lakini…

By | May 24, 2017

Mimi siyo mnafiki lakini…… maelezo yanayofuata hapo ni ya unafiki mtupu. Au mimi siyo mbaguzi lakini…. sentensi itakayofuata hapo ni ya kibaguzi. Nafikiri unapata picha, kama vile, sitaki kupinga lakini…… unajua kinachofuata hapo. Matumizi yatu ya lugha na maneno yanatuwezesha watu kutusoma wazi, na kujua kile ambacho tunaficha kusema. Na (more…)

💥 #GHAHAWA ☕ ☕; UNAONA UNACHOTAKA KUONA…

By | May 23, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Nina imani umeshinda mengi leo, na kujifunza mengi pia. Kwa yale uliyoshindwa, hujashindwa bado kama umejifunza kitu, na hivyo kesho nenda kaweke juhudi zaidi. Karibu kwenye #GHAHAWA yetu jioni ya leo ambapo tunapeana chakula cha fikra ili kuweza kuweka (more…)

UKURASA WA 874; Busara Kwa Mpumbavu…

By | May 23, 2017

Mpumbavu hajali chochote kuhusu busara, kama ilivyo mtu mwenye ugonjwa wa akili asivyojali kuhusu yale anayofanya. Hii ni kwa sababu watu hawa hawajui hicho ambacho wewe unashangaa kwa nini hawajali. Ni sawa na kumshangaa kipofu kwa nini haoni kitu unachotaka aone, ataonaje na hana macho? Hivyo mtu anapofanya jambo ambalo (more…)