Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 501; Njia Mbili Za Kuwa Mbele Ya Wengine…

By | May 17, 2016

Katika jambo lolote ambalo unachagua kufanya, kuna wengine wengi ambao nao pia wanalifanya. Inawezekana umeanza kufanya kwa sababu uliona wengine wanafanya au wengine wamekuona wewe unafanya na wao wakaanza kufanya. Hivyo ushindani ni kitu ambacho huwezi kukikimbia. Kama unavyojua, kushindana moja kwa moja ni kitu ambacho sikushauri ufanye kwa sababu (more…)

Vitu vinne vinavyochangia thamani na kipato cha biashara yako.

By | May 16, 2016

Kujua thamani ya biashara yako na kipato unachoweza kuingiza kupitia biashara hiyo ni moja ya vitu muhimu unavyotakiwa kuzingatia. Na kama ukiweza kufanya hivi kabla hujaanza biashara yako unaweza kuianza ukiwa na mpango bora wa kutoa thamani kubwa na kutengeneza kipato kizuri.  Watu wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara na kufanya (more…)

UKURASA WA 500; Maua Yatakayochanua Kesho…

By | May 16, 2016

Maua yatakayochanua kesho, ni yale ambayo yamepandwa leo. Na hivyo kama jana hakuna maua uliyopanda, usitegemee maua yachanue leo. Muhimu zaidi ni kwamba kulalamika na kujuta kwamba kwa nini hukupanda maua jana, hakutasaidia maua yachanue kesho. Njia pekee ya kuhakikisha hilo ni kupanda maua leo. Huu ni ujumbe maalumu kwa (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Chanzo Kikuu Cha Mafanikio Na Furaha Kwenye Maisha Yako.

By | May 15, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye kipengele chetu hiki cha FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunajijengea falsafa ambayo itatuwezesha kuwa na maisha bora yenye mafanikio na furaha. Tumeshajifunza sana kuhusu mafanikio na mbinu za kufikia mafanikio. Na pia tumeshajifunza sana kuhusu furaha na vyanzo vya furaha kwenye maisha yetu. (more…)

UKURASA WA 499; Dawa Ya Usumbufu Wa Mitandao…

By | May 15, 2016

Tunaishi kwenye wakati ambao kuna usumbufu mkubwa sana. Ni vigumu kuweza kupata utulivu wa kuweza kufanya kazi zako kwa ufanisi. Na usumbufu huu unaanza na sisi wenyewe kutokana na vifaa vya kiteknolojia tunavyotumia. Simu za mkononi za kisasa zina uwezo wa kufanya mambo mengi na hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha (more…)

UKURASA WA 498; Siyo Kila Mtu, Lakini Kwa Nini Usiwe Wewe?

By | May 14, 2016

Kuna majibu ambayo watu wakikupa pale unapowaambia kitu unaona ni jinsi gani ambavyo wanajizuia wao wenyewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Unamwambia mtu aweke juhudi ili kufikia utajiri, anakuambia siyo kila mtu anaweza kuwa tajiri. Ni sawa siyo kila mtu anaweza, lakini kuna ambao wanaweza, sasa kwa nini wewe (more…)

UKURASA WA 497; Watu Ambao Hawawezi Kukuelewa….

By | May 13, 2016

Mtoto mdogo wa miaka mitatu, ambaye ndiyo kwanza amejua kuongea, akiangalia unachofanya na kukuambia huwezi kufanya kitu hiko au utashindwa unamchukuliaje? Hutampa uzito sana, kwa sababu unajua bado ni mtoto na hajui lile analolisema. Utamchukulia ni mtu ambaye hajui hata kitu chenyewe kinafanywaje ila amejisikia tu kusema hivyo. Kauli hiyo (more…)

UKURASA WA 495; Mafanikio Ni Matone, Siyo Mafuriko…

By | May 11, 2016

Tunapoona mafanikio ya wengine, huwa tunaona mafuriko. Tunaona jinsi mambo makubwa yanavyotokea kwao huku wakionekana hawaweki juhudi kubwa sana. Na sisi tunafikiria kwenye mlengo huo huo kwamba kama na sisi tutaweza kutengeneza mafuriko kama ya hao wengine, basi mambo yetu yatakuwa vizuri sana. Ambacho hatuoni ni kwamba watu hawa hawakuanza (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; THE 50TH LAW (Mbinu Za Kuondokana Na Hofu)

By | May 11, 2016

The 50th law ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi Robert Green ambapo amefuatilia maisha ya mwanamuziki 50 Cent ambaye ameweza kufanikiwa sana kwenye muziki. Mwandishi alifuatilia kwa makini maisha ya mwanamuziki huyu ambaye amepitia maisha magumu sana lakini bado akaweza kufikia mafanikio makubwa. katika uchambuzi wake, mwandishi aliweza kuona falsafa moja (more…)