Category Archives: ONGEA NA COACH MAKIRITA

Kupitia makala hizi unaongea moja kw amoja na kocha wako MAKIRITA AMANI. Hapa unapata mambo mazuri kwa ajili yako ili uweze kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.

Swali moja muhimu sana ninalojiuliza kila siku asubuhi.

By | November 24, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini upo vizuri sana na maisha yako yanaendelea kuwa bora kadiri siku zinavyokwenda. Vizuri na hongera sana kwa hilo. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya mazuri na muhimu sana, ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio na kuwa na maisha bora. Leo nitakushirikisha swali moja muhimu sana (more…)

Hivi Ndivyo Waajiriwa Wanavyopoteza Uhuru Wao Wenyewe, Na Jinsi Ya Kuudai Tena.

By | November 19, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini unaendelea vyema sana na majukumu yako ya kila siku. Na nina imani kabisa ya kwamba kama unafanyia kazi haya ambayo tunashirikishana hapa basi mambo yako yatakuwa yanabadilika kadiri siku zinavyokwenda. Naomba nikukumbushe pia ya kwamba mabadiliko hayaji mara moja kama mvua, bali yanakuja kidogo kidogo (more…)

Kuwa Chanya, Inalipa Sana Kuliko Kuwa Hasi.

By | November 12, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Karibu tena kwenye mazungumzo yetu mazuri haya ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali kwa ajili ya mafanikio. Kama uliandika email kupata nafasi kwenye program mpya ya ukocha, email bado zinafanyiwa kazi ili kuchagua ni watu gani nitafanya nao kazi. Niwashukuru na kuwapongeza sana wote ambao mmeitaka program (more…)

Maneno Mazuri Ya Ushindi Kutoka Kwa Rafiki Yetu.

By | November 5, 2015

Habari za leo rafiki? Nina imani unaendelea vyema sana na kufanyia kazi malengo na mipango yako. hongera sana kwa hilo na nikukaribishe kwenye mazungumzo yetu ya siku hii nzuri ya leo. Kwenye mazungumzo yetu ya leo mimi nitakaa pembeni kidogo na kwa pamoja tutamsikiliza na kujifunza kutoka kwa rafiki yetu (more…)

Ndio, hakuna jipya, lakini bado unahitaji kujifunza “KILA SIKU”.

By | November 3, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini uko poa sana, rafiki yako niko vizuri sana. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya muhimu sana kama marafiki. Karibu tushirikishane yale muhimu katika safari yetu hii tuliyochagua, safari ya kuwa tofauti na kuwa bora sana kila siku. Leo nataka tushirikishane jambo moja muhimu ambalo limekuwa (more…)

Watu wanakua, watu wanabadili mawazo.

By | October 27, 2015

Habari za leo rafiki? Unaendeleaje? Nina imani harakati zako za kuboresha maisha yako na ya wale ambao wanakuzunguka zinaendelea vizuri sana. Hongera kwa hilo. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya ya leo, tuendelee kupeana maarifa na mbinu za kuboresha maisha yetu. Kumbuka hakuna kilele cha ubora, kila siku kwenye maisha (more…)

Hiki Ni Kitu Kimoja Nakuhakikishia Utakutana Nacho Mara Kwa Mara.

By | October 15, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Naamini uko vizuri sana, mimi pia nipo vizuri. Karibu tena leo kwenye mazungumzo yetu haya muhimu, ambapo mimi na wewe tunazungumza kama marafiki. Leo nataka nikuambie kitu kimoja ambacho nakuhakikishia utakutana nacho mara kwa mara. Na siku utakayoacha kukutana nacho, ni siku utakapoondoka kwenye dunia (more…)

Usikubali mtu yeyote awe mzigo kwako.

By | October 13, 2015

Habari rafiki? Naamini unaendelea vizuri sana, hongera kwa hilo. Karibu tena kwenye mazungumzo haya baina yangu mimi na wewe rafiki yangu wa karibu. Sisi wote tuna lengo kubwa la kuwa na maisha bora kwetu na wanaotuzunguka. Kwa kufanyia kazi malengo na mipango tuliyojiwekeza. Kupitia mazungumzo haya tunashirikishana mambo muhimu sana (more…)

Hivi Ndivyo Unavyoua Ndoto Zako Kubwa Za Mafanikio.

By | September 9, 2015

Habari za leo rafiki? Karibu kwenye mazungumzo yetu ya leo kama ulivyo utaratibu wetu kila siku ya jumanne na alhamisi. Naamini unaendelea vizuri, na unafanyia kazi yale yote ambayo unajifunza. Vizuri sana kwa hilo. Leo nataka tuzungumzie kitu kimoja ambacho nimekuwa nakiona kwa watu wengi ninaofanya nao kazi. Watu wengi (more…)

Kwani mafanikio ni nini hasa?

By | September 9, 2015

Heus amicus/amica! Quid agis? Hapo ni habari rafiki, unaendeleaje? Kwa kilatini, unakumbuka nilikuambia mwezi huu nitajifunza kilatini? Ndio mambo yameanza, nipigie makofi kidogo. Kama wewe ni mwanaume salamu hiyo ya kwanza ingekuwa heus amicus na kama wewe ni mwanamke salamu hiyo ingekuwa amica. Kilatini kina maneno yanayotumika kwa wanaume(masculini generis), (more…)