Category Archives: SIKU 30 ZA MAFANIKIO

SIKU YA 11; Jinsi Ya Kuanza Safari Yako Ya Mafanikio.

By | September 11, 2014

Kwa kuwa sasa umeshaamua kujiajiri mwenyewe au kufanya biashara kuna mambo ya msingi unahitaji kuyajua au kuyakamilisha ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Jiulize kama kuwa bosi wako mwenyewe ni kitu muhimu sana kwako, jiulize kama ni mtu ambaye unaweza kufikia mafanikio ukiwa unajifanyia kazi yako. Jiulize ni yapi madhaifu yako (more…)

SIKU YA 10; Ijue Siri Ya Kuelekea Kwenye Utajiri.

By | September 10, 2014

Tajiri mmoja wa kihindi aliulizwa aeleze ni kitu gani kimoja ambacho kimumwezesha kufikia mafanikio makubwa sana na kuweza kuwa tajiri sana kupitia biashara anayofanya? Alijibu “mimi ndio nguvu kubwa ya mafanikio yangu, kumfanyia kazi mtu mwingine unarudishwa nyuma au kulazimishwa kufanya kazi chini ya kiwango chako” Nafikiri kila mmoja wetu (more…)

SIKU YA 9; Siri Ya Utajiri, Mafanikio na Furaha.

By | September 9, 2014

Ni mara ngapi umewahi kutamani muujiza utokee na mara moja uwe tajiri mkubwa, na uwe na mafanikio na furaha tele? Hii ni ndoto ambayo inawatokea watu wengi katika maisha yao. Hijalishi hali uliyonayo sasa, iwe umeshapata mafanikio ya kukuridhisha au unasukuma maisha kiubishi, unapenda kuwa zaidia ya hapo ulipo sasa. (more…)

SIKU YA 8; Mtazamo Wako Ndio Unatawala Maisha Yako.

By | September 8, 2014

Mtazamo chanya na tabia nzuri zitakuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Fikra zako zinazotokana na mtazamo wako ndizo zitakazokufanya uweze kufanikiwa au ushindwe kufanikiwa. Fikiria mambo madogo na utakuwa mtu mdogo, fikiria mambo makubwa na utakuwa mtu mkubwa kama ukitenda yale unayofikiri. Mtu mwenye mtizamo sahihi haonyeshi tu kufanikiwa bali hufikia mafanikio (more…)

SIKU YA 7; Tiba Rahisi Kwa Walioacha Shule, Walioacha Kazi na Walioacha Maisha.

By | September 7, 2014

Kumbuka kwamba kila mmoja wetu ana hitaji kubwa la kukubalika kwa kile anachofanya au kile alichofanya. Kama hitaji hili la kukubalika lisipotimizwa, mtu hupata hisia za kutokuaminika, hofu ya kutokuweza na hatimaye kushindwa. Ni hisia hizi ambazo humfanya mtu kuamua kuacha kile anachofanya iwe ni elimu, kazi au hata maisha (more…)

SIKU YA 6; Epuka Mawazo Yenye Sumu.

By | September 6, 2014

Kuna watu wengi duniani ambao ni wagonjwa wa mawazo kuliko walivyo wagonjwa wa mwili. Magonjwa haya ya mawazo yanasababishwa na ukosefu wa virutubisho muhimu kwa akili. Virutubisho muhimu kwa akili ni mawazo mazuri na yenye kujenga. Watu wenye ugonjwa wa mawazo ni watu ambao mara zote wanaingiza mawazo yenye sumu (more…)

SIKU YA 5; Imani Imara Kwamba Unaweza Kufanikiwa.

By | September 5, 2014

Katika watu wote waliofikia mafanikio makubwa, kuna kitu kimoja ambacho kinapatikana kwa kila mmoja. Kitu hicho ni imani imara kwamba wanaweza kufikia mafanikio makubwa sana kwenye kile wanachofanya. Hijalishi ni kitu gani umechagua kufanya au kupata, unaweza kufanya au kupata chochote unachotaka. Lakini ni lazima ufanye mambo haya matatu; 1. (more…)

SIKU YA 4; Nguvu Ya Kuamini.

By | September 4, 2014

Kuna nguvu moja inayokuwezesha kufanikiwa na kupata chochote unachotaka. Nguvu hii inaweza kushinda vikwazo, changamoto na hata kushindwa. Nguvu hii ni NGUVU YA KUAMINI. Bila nguvu ya kuamini una uhakika wa kushindwa kwenye jambo lolote unalofanya. Kwa kuwa nayo kufanikiwa ni uhakika. Nguvu ya kuamini inaweza kukupatia mambo haya matatu; (more…)

SIKU YA 3; Jinsi Ya Kuondo Kabisa Hofu Ya Kushindwa.

By | September 3, 2014

Ili uweze kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako ni lazima uweze kuishinda hofu ya kushindwa. Kupata furaha, mapenzi, mafanikio, utajiri, ushawishi, umaarufu na hata chochote unachotaka hatua ya kwanza ni kuishinda hofu ya kushindwa. Hatua ya kwanza ya kushinda hofu ya kushindwa ni kuelewa kwamba kushindwa ni kitu ambacho kinatokea (more…)

SIKU YA 2; Neno Moja Litakaloleta Maajabu Maishani Mwako.

By | September 2, 2014

Kuna neno moja ambalo linaweza kuleta maajabu makubwa sana kwenye maisha yako. Neno hili la maajabu ni siri ya kuwafanya wengine wafanye kile unachotaka. Neno hili la maajabu ni siri ya kupata chochote unachotaka. Neno hili la maajabu linafundishwa katika dini zote na linatumika katika kada zote za elimu, matibabu, (more…)