#TAFAKARI YA LEO; SIYO RAHISI LAKINI INAWEZEKANA…

By | April 16, 2021

Kufikia mafanikio makubwa siyo kazi rahisi, lakini ni kitu kinachowezekana kwa sababu wapo ambao wameweza kuyafikia. Hivyo wajibu wetu kama tunataka kuyafikia, ni kujitoa kweli kweli na kuwa tayari kupambana kwa kila namna ili kuyapata. Tunapotaka kukata tamaa tujikumbushe haya mawili, kwamba wapo walioweza kufikia mafanikio hayo makubwa na wapo (more…)

2297; Misimu Ya Maisha…

By | April 15, 2021

2297; Misimu Ya Maisha… Kila kitu kwenye asili, huwa kinaenda kwa misimu. Na hiyo ni kwa sababu kwenye asili hakuna kilichosimama, kila kitu kipo kwenye mwendo. Maisha yetu pia yana misimu mbalombali, lakini wengi hatulijui hilo. Tunachofikiri ni maisha kama safari ya njia iliyonyooka, kuanzia kuzaliwa mpaka kufa. Lakini hivyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUWEZI KUELEWEKA NA WOTE…

By | April 15, 2021

Kueleweka au kukubalika na watu wote ni kitu ambacho hakiwezi kutokea. Hata kama unafanya jambo lenye manufaa kiasi gani, kuna ambao wataona ni bora ungefanya jambo jingine wanaloona lina manufaa zaidi. Hivyo msingi wako kwenye yale unayofanya haupaswi kuwa kukubalika na kila mtu, badala yake unapaswa kuwa ni kufanya kilicho (more…)

2296; Ukiweka Sifa Pembeni, Utafanya Makubwa.

By | April 14, 2021

2296; Ukiweka Sifa Pembeni, Utafanya Makubwa. Sisi kama binadamu tunasukumwa sana na sifa katika mengi tunayofanya. Tunapojua kuna fursa ya wengine kutukubali na kutusifia kwa kile tunachofanya, tunasukumwa zaidi kukifanya. Lakini ubaya wa kufanya kwa sifa ni unaweza kujikuta unafanya hata yasiyokuwa na manufaa kwa sababu tu unataka sifa. Ipo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIDHARAU HATUA NDOGO NDOGO…

By | April 14, 2021

Hakuna kitu unachofanya kisiache madhara kwenye maisha yako. Kila hatua unayochukua, hata kama ni ndogo kiasi gani, inaacha alama kwenye maisha yako na unavyorudia kufanya inajenga au kubomoa tabia fulani ndani yako. Pia kile unachofanya, kinageuka kuwa mazoea na baadaye unajikuta unafanya bila hata ya kufikiri. Kuwa makini sana na (more…)

2295; Zaidi na Kidogo…

By | April 13, 2021

2295; Zaidi na Kidogo… Tengeneza zaidi, tumia kidogo. Ongoza zaidi, fuata kidogo. Sikiliza zaidi, ongea kidogo. Changia zaidi, chukua kidogo. Vumilia zaidi, harakisha kidogo. Shirikiana zaidi, jitenge kidogo. Andika zaidi, angalia kidogo. Soma vitabu zaidi, mitandao kidogo. Kuwa na matumaini zaidi, kukata tamaa kidogo. Kocha. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WINGI HAUBADILI USAHIHI…

By | April 13, 2021

Huwa tunapenda kupima usahihi wa kitu kwa kuangalia wingi wa wanaokifanya. Kama wengi wanafanya au kukubaliana na kitu, tunaamini kitu hicho ni sahihi na hata kama siyo sahihi basi tunaamini kifo cha wengi ni harusi. Tatizo ni huwezi kufanikiwa kwa kuhangaika na yasiyo sahihi na kama unapima usahihi wa kitu (more…)

2294; Tatizo la wataalamu…

By | April 12, 2021

2294; Tatizo la wataalamu… Tafiti nyingi ambazo zimefanywa kwenye ubashiri, kwa kulinganisha wataalamu wa eneo husika na watu wa kawaida, watu wa kawaida wamekuwa wanafanya vizuri kuliko wataalamu. Pia mambo mengi ambayo wataalamu hukadiria au kushauri huwa hayaendi kwa namna walivyoeleza kwa utaalamu wao. Tatizo la wataalamu ni kuwa na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; EPUKA KAULI HII YA KITAPELI…

By | April 12, 2021

Utapeli huwa hautofautiani sana, ukiwa na akili kidogo tu na ukaitumia, utaona wazi viashiria vya utapeli. Na matapeli wanajua kuna viashiria vilivyo wazi na pale unapouliza kuhusu hilo tayari wana majibu. Watakuambia hii ni tofauti na nyingine ambazo utakuwa umefananisha nazo. Na kama utaendelea kuuliza zaidi watakuonesha wengine ambao tayari (more…)