#TAFAKARI YA LEO; KIPIMO NI WINGI WA WANAOFANYA…

By | April 11, 2021

Kipimo rahisi kabisa unachoweza kutumia kuamua kitu gani ufanye ni kuangalia wingi wa wale wanaokifanya kitu hicho. Ukiona kitu kinafanywa na watu wengi, jua hicho siyo sahihi kwako kufanya. Kwa sababu watu wengi wanapenda kufanya vitu rahisi na vilivyo rahisi huwa havina thamani kubwa. Wewe unapaswa kufanya vitu vyenye thamani (more…)

2292; Rahisi ni hatari…

By | April 10, 2021

2292; Rahisi ni hatari… Ukiona kila unachofanya ni rahisi kwako, hukutani na ugumu wala changamoto, ogopa sana, kwa sehemu kubwa uko eneo hatari na hutaweza kufanya makubwa. Japo huwa tunapenda mambo yawe rahisi, lakini iko wazi, hakuna mafanilio yamewahi kutokana na kufanya vitu rahisi. Tukirudi kwenye asili, ambayo ina kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO, HAKUNA KINACHOPOTEA…

By | April 10, 2021

Kuna wakati utaweka juhudi na muda kwenye kile unachofanyia kazi, lakini matokeo unayopata yasiwe sahihi. Ni rahisi kuona juhudi na muda ulioweka vimepotea. Kama upo kwenye mchakato sahihi, basi jua hakuna kinachopotea, hata kama matokeo unayopata siyo uliyotaka, jua juhudi na muda ulioweka havijapotea, badala yake ni uwekezaji ambao baadaye (more…)

2291; Mchakato wa mafanikio…

By | April 9, 2021

2291; Mchakato wa mafanikio… Mafanikio ni mchakato, ambao unahitaji juhudi na muda wa kutosha mpaka uweze kuyafikia. Mchakato huo una vipengele kadhaa, ambavyo unapaswa kuvifuata bila kuacha hata kimoja. Kipengele cha kwanza ni kujua kile hasa unachotaka kupata au kufikia. Lazima ujue mafanikio kwako yana maana gani. Kama hujui unakotaka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TOA ILI UPATE…

By | April 9, 2021

Watu wengi wanakwama kwenye maisha kwa sababu wanataka kupata kwanza kabla hawajatoa. Mtu anataka kazi imlipe vizuri ndiyo aweke juhudi au biashara impe faida kubwa ndiyo aweke umakini wake mkubwa. Kinachotokea ni hawapati kile wanachotaka. Ili kupata unachotaka, anza kutoa kwanza. Anza kuweka juhudi kubwa kwenye kazi na biashara yako (more…)

2290; Endelea kukaa kimya…

By | April 8, 2021

2290; Endelea kukaa kimya… Kama mtu alitumia mamlaka yake kukukandamiza au kukuumiza na wewe ukachagua kukaa kimya kwa kuyaogopa mamlaka yake, hupaswi kuanza kulalamika pale mtu huyo anapokuwa hayupo au hana tena mamlaka yale aliyotumia kukuumiza nayo. Kuja kusema baadaye kwamba mtu alikuumiza, alikosea au hakuwa anafaa baada ya mtu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HESHIMA NI BORA KULIKO KIKI…

By | April 8, 2021

Watu wanaotaka mafanikio kwa njia za mkato, huwa wanakimbilia kutumia kiki. Kufanya mambo ya kijinga ambayo yanawapa umaarufu wa haraka, lakini usio na heshima. Umaarufu wa aina hiyo huwa haudumu muda mrefu na huacha madhara makubwa. Wewe jenga mafanikio na umaarufu wako kupitia heshima na heshima inajengwa kupitia kutoa thamani (more…)

2289; Ulichozaliwa nacho, hupaswi kukiomba…

By | April 7, 2021

2289; Ulichozaliwa nacho, hupaswi kukiomba… Jamii huwa haipendi uwe huru kuwa vile unavyotaka. Na ili kukunyima uhuru wako, inahakikisha inakujengea aina fulani ya utegemezi ambapo utajiona bila jamii hiyo maisha yako hayawezi kwenda. Ukianza na uhuru wenyewe, ulizaliwa ukiwa huru kabisa, lakini mamlaka mbalimbali zinajihamishia uhuru huo na kukufanya uzione (more…)

#TAFAKARI YA LEO; RAHA IPO KWENYE KUFANYA…

By | April 7, 2021

Watu wengi hutegemea kupata raha au furaha baada ya kukamilisha kufanya kitu. Lakini ukweli ni kwamba raha inapatikana wakati wa kukifanya kitu, siyo baada ya kumaliza kukifanya. Na ili uipate raha hiyo, lazima uwe umechagua na kuridhia kukifanya na wakati wa kukifanya unaweka umakini wako wote hapo. Usihangaike kutafuta raha (more…)

2288; Watoze watu wakikukatisha kwenye hiki…

By | April 6, 2021

2288; Watoze watu wakikukatisha kwenye hiki… Joe Girard, aliyekuwa muuzaji mkubwa wa magari amewahi kusema kitu anachopenda zaidi ni kulala, hivyo kama mtu anakatisha usingizi wake, lazima awatoze. Kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza hapa, kuhusu kuweka vipaumbele kwenye maisha yako. Tumeshajifunza umuhimu wa kufanya kile unachopenda na kuangalia namna (more…)