BIASHARA LEO; Kazi Kubwa Iliyopo Kwenye Mwanzo Wa Biashara Yako…

By | September 6, 2018

Ni kutengeneza wateja wa biashara hiyo. Kutengeneza sifa ambayo wateja wako wanakuwa nayo kuhusu wewe. Huwezi kwenda kununua kitu kwenye biashara mara moja na ukatoka hapo ukawaambia watu ile ni sehemu nzuri. Utaenda na kupata huduma nzuri, utashawishika tena kurudi na utapata huduma nzuri, mara ya tatu ukipata tena huduma (more…)

UKURASA WA 1345; Acha Ushahidi Uongee Wenyewe…

By | September 6, 2018

Ni rahisi sana kudanganya kwa maneno, ni vigumu mno kudanganya kwa vitendo. Hivyo kama unataka kuujua ukweli, usisikilize watu wanasema nini, bali angalia watu wanafanya nini. Ushahidi huwa unaongea wenyewe hata kama umechelewa. Tumia hili kwa pande mbili. Upande wa kwanza, pale unapotaka kujua ukweli kuhusu wengine, angalia zaidi wamefanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; RUDIA RUDIA…

By | September 6, 2018

Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ambayo tumeipata leo. Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa na kupata matokeo bora kabisa. Orodhesha yote unayokwenda kufanya leo, na hakikisha unafanya kweli. Usiruhusu kujiambia utafanya kesho, maana hakuna kesho, leo ndiyo muhimu kwako. Msingi wetu wa maisha ya (more…)

BIASHARA LEO; Hadithi Zinauza Kuliko Kelele…

By | September 5, 2018

Kuna njia mbili za kuuza chochote unachouza. Njia hizo ni kelele na hadithi. Kwenye kelele, mtu anapaza sauti kwa njia mbalimbali ili kuwafikia wengi wajue kwamba yupo na anauza nini. Matangazo ya vyombo vya habari, matangazo kwenye mitandao ya kijamii ni moja ya aina za kelele za kutangaza na kujaribu (more…)

UKURASA WA 1344; Kwenye Zama Za Taarifa, Wewe Ndiye Habari…

By | September 5, 2018

Kwenye zama tunazoishi sasa, zama za taarifa, taarifa ni nyingi kuliko uwezo wa mtu yeyote kuzipata zote. Hivyo hili linawaweka wengi kwenye hofu ya kupitwa, kitu kinachowapelekea kupoteza muda mwingi kukimbizana na vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa kwao. Njia pekee ya kuondokana na hali hii ya kukimbizana na kila aina (more…)

BIASHARA LEO; Matumizi Bora Ya Fedha Ya Matangazo Kwenye Biashara Yako…

By | September 4, 2018

Nimekutana na dhana hii ambayo nimeona ni nzuri sana kuijaribu kwenye biashara. Kama una biashara ambayo unahitaji kutangaza ili kuwafikia wengi, badala ya kutumia fedha kwenye matangazo, tumia fedha hiyo kwenye bidhaa au huduma ambazo unatoa kwa watu. Yaani ukishajua kiasi cha fedha unayopaswa kulipa kwenye matangazo ni kiasi gani, (more…)

UKURASA WA 1343; Ukishafanikiwa, Sheria Hazibadiliki…

By | September 4, 2018

Watu hushangazwa sana pale wanapoona baadhi ya watu waliofanikiwa wakianguka. Wanawaona watu ambao wametoka chini, wamejitahidi na kupata mafanikio, lakini wanaanguka na kurudi chini kabisa. Kinachotokea ni hiki; wengi wanapoanza wanaweka juhudi kubwa sana, wanajituma mno, hawachagui kazi, wanafanya kazi kwa muda wa ziada, wanakuwa tayari kuumia, wanakuwa wavumilivu hasa (more…)