BIASHARA LEO; Mteja Wa Mfano Wa Biashara Yako…

By | August 7, 2018

Kosa moja wanalofanya wafanyabiashara wengi ni kuanzisha biashara zao kwa kujifikiria wao wenyewe, au kuangalia wafanyabiashara wengine wanafanya nini. Biashara yoyote inayoanzishwa na mtu kwa sababu anafikiria ananufaikaje na biashara hiyo pekee, au kwa kuwaangalia wengine wanaofanya biashara hiyo na kujiambia inalipa ndiyo maana wapo, lazima biashara hiyo ishindwe. Biashara (more…)

UKURASA WA 1315; Kwa Nini Ni Vigumu Sana Kuwa Wewe?

By | August 7, 2018

Kama kuna kitu kilipaswa kuwa rahisi kwenye maisha yetu, ni mtu kuwa wewe, kuwa kile ambacho umezaliwa na kuletwa hapa duniani kuwa. Kama ambavyo ukichukua yai la kuku na ukatamishia kwenye kanga, bado atatoka kuku, na hata kifaranga wa kuku atalelewa pamoja na vifaranga wa kanga, bado atabaki kuwa kuku. (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujawauzia Wengine Bidhaa Au Huduma Yako, Wauzie Hichi Muhimu…

By | August 6, 2018

Umewahi kukutana na mtu ambaye anaweza kuuza kitu chochote kwa mtu yeyote. Yaani unaenda mahali, unajiambia kabisa kwamba hutanunua, lakini unakutana na mtu, na kwa jinsi anavyokupokea, kwa jinsi anavyokusikiliza, jinsi anavyokuelezea unachouliza, unajisikia vibaya kutokununua? Kama umewahi kuwa kwenye hali kama hiyo, basi unajua kwamba ulinunua kitu siyo kwa (more…)

UKURASA WA 1314; Unaponasa Kwenye Yale Yasiyo Muhimu…

By | August 6, 2018

Moja ya sababu kubwa kwa nini kila mmoja wetu anapaswa kuwa na orodha ya vitu atakavyofanyia kazi kwenye siku yake ni kwamba siku inavyoharibika huwa siyo rahisi kuonekana. Unachoshangaa ni siku yako imeisha, umechoka, lakini ukiangalia, hakuna kikubwa umefanya, hakuna matokeo mazuri uliyozalisha. Tunazungukwa na kila aina ya usumbufu, na (more…)

BIASHARA LEO; Dawa Inayofanya Kazi Ni Inayouma…

By | August 5, 2018

Kuna tukio la kisaikolojia linatokea pale mteja anapotoa fedha yake aliyoipata kwa shida kukulipa kwa kile unachouza. Kwa sababu kwanza akishakupa fedha hiyo maana yake hawezi kuitumia kwa mambo mengine ambayo yanaweza kuwa muhimu kwake. Na pili, mteja anahitaji kupata uhakika kwamba anacholipia ni sahihi na moja ya kipimo anachotumia (more…)

UKURASA WA 1313; Siyo Mwonekano, Bali Matokeo…

By | August 5, 2018

Tunaishi kwenye dunia ambayo watu wanajali zaidi mwonekano wa nje kuliko matokeo ambayo wanatoa. Watu wanapenda kuonekana wamefanikiwa wakati matokeo wanayopata siyo ya mafanikio. Watu wanapenda kuonekana wanajua wakati wanachojua hakiwasaidii kuwa bora. Watu wanapenda kuonekana wana furaha muda wote wakati maisha yao hayaakisi aina hiyo ya furaha. Nilichojifunza kupitia (more…)

BIASHARA LEO; Miliki Matatizo Ya Wateja Wako…

By | August 4, 2018

Kabla hujakimbilia kupunguza bei kwenye biashara yako kwa sababu wengine wanapunguza bei, kuna hatua nyingi unazoweza kuchukua na zikaongeza thamani sana kiasi kwamba bei yako inaonekana si kitu kulingana na mteja anachopata. Moja ya vitu unavyoweza kufanya ni kuyamiliki matatizo ya wateja wako. Yale matatizo ambayo biashara yako inatatua. Mfanye (more…)

UKURASA WA 1312; Usifuate Sheria Ya Dhahabu, Fuata Sheria Ya Almasi…

By | August 4, 2018

Mahusiano yetu na wengine ni eneo muhimu sana la mafanikio yetu. Na kama Zig Zigler alivyowahi kusema, unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka. Sheria ya dhahabu imekuwa inachukuliwa kama sheria muhimu sana kwenye mahusiano baina ya watu. Sheria hii inasema watendee wengine kama ambavyo ungependa (more…)