#TAFAKARI YA LEO; WATU WA KUWAEPUKA KAMA UKOMA…

By | July 19, 2018

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya na bora sana kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Machaguo Mawili…

By | July 18, 2018

Kikwazo namba moja kwenye mauzo katika biashara nyingi ni mteja kukosa machaguo zaidi wakati ananunua. Mteja anaweza kuja kwenye biashara yako, akiwa na shida au uhitaji fulani. Wewe kama mfanyabiashara ukamweleza na kumpa kile ambacho unaona kinamfaa. Sasa utafanya kosa kubwa sana, kama utampa kitu kimoja tu. Maana wakati wote (more…)

UKURASA WA 1295; Usipowaambia Hawatajua Na Wasipojua Hawatafanya Vizuri…

By | July 18, 2018

Ili ufanikiwe, unahitaji kushirikiana na wengine, unahitaji msaada na mchango wa watu wengine. Kwa sababu hakuna tunachoweza kupata sisi wenyewe, chochote tunachotaka kinatoka kwa wengine. Hivyo hitaji muhimu sana kwenye mafanikio yetu ni uwezo mzuri wa kuwasiliana na wengine. Watu wengi wamekuwa wanakosa kile wanachotaka kwa sababu watu wengine hawajafanya (more…)

BIASHARA LEO; Kupunguza Bei Ni Uvivu Kibiashara…

By | July 17, 2018

Kama unapunguza bei kwa sababu gharama zako za uzalishaji au za kuendesha biashara zimepungua na unajali wateja wako wapate kilicho bora, hongera sana. Lakini kama unapunguza bei kwa sababu unataka wateja wengi zaidi waje kwako badala ya kwenda kwa washindani wako kibiashara, nina habari mbaya kwako, huo ni uvivu wa (more…)

UKURASA WA 1294; Kitu Pekee Utakachojutia Sana Kwenye Maisha Yako…

By | July 17, 2018

Ni kutokuishi kwa kiwango cha uwezo mkubwa uliopo ndani yako. Hichi ni kitu ambacho utakijutia sana, na hutajisamehe kwa kosa hilo. Ukiwa bado mdogo, bado kijana, bado mtu mzima unaweza kujidanganya kwamba muda bado unao. Ni pale unapokuwa mzee, pale unapokuwa huna tena muda mrefu wala nguvu za kupambana, ndiyo (more…)

BIASHARA LEO; Kwenye Biashara Ndogo, Mafanikio Yanategemea Kitu Hichi Kimoja…

By | July 16, 2018

Biashara ndogo ni biashara ngumu sana kufanya, kwa sababu wewe mfanyabiashara ndiyo unakuwa kila kitu kwenye biashara yako. Maamuzi yote kwenye biashara yako yanakutegemea wewe, na kwa wingi wa majukumu yako, ni rahisi kushindwa kuweka mkazo kwenye maeneo muhimu ya ukuaji wa biashara yako. Unapokuwa kwenye biashara ndogo, kila siku (more…)

UKURASA WA 1293; Ukichelewa Ni Bora Hata Usifike Kabisa…

By | July 16, 2018

Wahenga walituambia ni bora kuchelewa kuliko kutofika kabisa. Na hata kwenye jamii zetu, imekuwa ni kawaida kuchelewa sehemu fulani, kuliko kutokufika kabisa. Hilo linaweza kuwa sahihi kwenye maisha ya kawaida, kwenye mahusiano na ahadi mbalimbali. Lakini inapokuja kwenye swala la mafanikio, inapokuja kwenye hatua z akuchukua ili kufanikiwa, muda ndiyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA ANAYEIANZA SIKU KWA KUTAKA MABAYA, LAKINI YANATOKEA….

By | July 16, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku (more…)