BIASHARA LEO; Mteja Hatakumbuka Zaidi Bei, Bali Hichi Muhimu…

By | July 15, 2018

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifikiri kwamba kikwazo cha wateja kununua kwao ni bei. Wengi wanashawishika kwamba wakishusha bei basi watapata wateja wengi. Na wakijaribu kufanya hivyo mwanzoni wanaweza kuona ongezeko la wateja, lakini mwisho wa siku hilo haliwasaidii kwenye ukuaji wa biashara zao. Hii ni kwa sababu moja, wateja makini wa (more…)

UKURASA WA 1292; Haraka Zimekunyima Mengi Kwenye Maisha Yako…

By | July 15, 2018

Kitu chochote kikubwa unachotaka kwenye maisha yako, kitahitaji muda mpaka kukipata kweli. Kadiri kile unachotaka kinavyokuwa kikubwa, ndivyo muda wa kukipata unakuwa mkubwa pia. Lakini wengi wamekuwa wanakosa kila wanachotaka, kwa sababu ya haraka. Wengi wamekuwa hawa subira wala uvumilivu, wamekuwa wanataka kitu na wanakitaka sasa. Hata wahenga walisema, haraka (more…)

UKURASA WA 1291; Watu Wapo Tayari Kugharamia Nini Kwako?

By | July 14, 2018

Lipo kosa moja kubwa ambalo watu wengi wanafanya na linawazuia sana kupata kile wanachotaka na hata mafanikio kwa ujumla. Kosa hilo ni kujirahisisha na kutokujithamini kwa namna wanavyopaswa kufanya. Watu wengi wamekuwa hawajiamini kama kweli wana thamani kubwa, na hivyo wamekuwa wakiogopa kuwataka watu walipe ile thamani ambayo wanaitaka hasa. (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Yako Inapaswa Kumpatia Mteja Fedha Zaidi…

By | July 14, 2018

Mtazamo ambao unao kwenye biashara unayofanya, ni moja ya vitu ambavyo vitaifanya biashara hiyo ifanikiwe sana au ishindwe kabisa. Hata kama utafanya kila kinachopaswa kufanya, kama mtazamo siyo sahihi, bado biashara haitapata matokeo makubwa. Mtazamo ambao mfanyabiashara anao huwa unakuwa kikwazo au kichocheo kikubwa kwa mafanikio ya biashara hiyo. Kuna (more…)

BIASHARA LEO; Wakati Sahihi Wa Kupunguza Gharama Kwenye Biashara Yako Ni Huu…

By | July 13, 2018

Faida ndiyo kitu kinachofanya biashara iendelee kuwepo. Kama biashara haitengenezi faida, haitachukua muda mrefu, itakupa. Pamoja na kuweka juhudi kubwa kwenye kuongeza mauzo na mapato, sehemu kubwa inayopunguza faida ya biashara ni gharama za kuendesha biashara hiyo. Gharama za kuendesha biashara zinapokuwa kubwa, faida inakuwa ndogo au hakuna kabisa. Hivyo (more…)

UKURASA WA 1290; Kwa Nini Kujua Pekee Hakukusaidii…

By | July 13, 2018

Karibu kila mtu anajua kitu gani sahihi kinapaswa kufanyika ili wapate kila wanachotaka. Ukitaka kudhibitisha hilo, jaribu kuomba ushauri kwa mtu yeyote unayekutana naye, au hata kwenye mitandao ya kijamii, fanya kama vile hujui au umekwama na unahitaji ushauri wa wengine. Utapata ushauri wa kila aina, kutoka kwa kila mtu. (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Unachofanya Mara Moja Kikawa Na Manufaa Kwenye Biashara Yako…

By | July 12, 2018

Hakuna kitu chochote ambacho ukifanya mara moja kitakuwa na manufaa makubwa kwenye biashara yako, hakuna kabisa. Mteja akinunua mara moja kwenye biashara yako na asinunue tena ni hasara kwako, hakuna faida yoyote unayotengeneza kwa mteja kununua mara moja. Mteja akija kwako na akanunua kitu kimoja huwezi kutengeneza faida nzuri kwenye (more…)

UKURASA WA 1289; Je Umetumia Vizuri Kila Nafasi Iliyopo?

By | July 12, 2018

Popote ulipo na chochote unachofanya, zipo nafasi nyingi sana za kufanya kuliko ambavyo unaweza kuzitumia. Nafasi za kufanya kwa ubora zaidi ni nyingi, lakini wengi wamekuwa wanatuma nafasi na njia chache, zile walizozoea, zile ambazo wamekuwa wanaona wengine wakitumia. Ndiyo maana mtu anaponiambia ameshafanya kila kitu lakini hapati anachotaka huwa (more…)