UKURASA WA 1176; Jikumbushe Maisha Yalikuwaje Kabla Ya Ulichozoea…

By | March 21, 2018

Mazoea ni sumu mbaya ambayo imekuwa inawasahaulisha watu kule walipotoka na kujikuta wanafanya makosa ambayo yanawarudisha kule walikotoka. Chukulia mfano wa mtu ambaye hana kazi, na maisha ni magumu, anaomba sana apate kazi, hata kama ni kazi yoyote na ataifanya kwa moyo kwa malipo yoyote. Kwa kuwa mawazo hujenga, basi (more…)

UKURASA WA 1175; Wakati Mwingine Siyo Makosa Yako…

By | March 20, 2018

Kuna wakati tunafanya kila tunachopaswa kufanya, tunajitahidi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, na tunategemea kupata matokeo bora kwa hatua tulizochukua. Lakini kinachotokea ni tunapata matokeo ya tofauti kabisa, matokeo yanakuwa mabaya kama vile hatujafanya kitu kabisa. Hapa ni rahisi kuanza kujilaumu na kuona kwamba tuna matatizo fulani. Tunaweza kuona tuna (more…)

UKURASA WA 1174; Usipange Kutokufanya Kitu Fulani, Ni Njia Ya Kushindwa….

By | March 19, 2018

Katika mipango yetu ya maisha, kuna vitu ambavyo tumekuwa tunafanya ambavyo vinaturudisha nyuma au vinatuzuia kufika kule ambapo tunataka kufika. Na hivyo katika kuhakikisha tunaondokana na mambo hayo, tunapanga kutokufanya vitu fulani. Lakini kinachotokea ni kwamba, tunajikuta bado tunafanya, na hivyo kuona kama tumeshindwa kuondokana na mambo hayo yanayoturudisha nyuma. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VITU HIVI VIWILI VISIKUSUMBUE…

By | March 19, 2018

“There are two things a person should never be angry at, what they can help, and what they cannot.” -Plato Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo, fursa ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

UKURASA WA 1173; Jinsi Ya Kupata Muda Wa Kufanya Kila Kitu…

By | March 18, 2018

Hakuna kitu kinawapa watu msongo wa mawazo kwa sasa kama kupata muda wa kufanya kila kitu. Kila mtu ana mambo mengi ya kufanya kuliko muda alionao. Na hivyo kwa kuwa ya kufanya ni mengi kuliko muda, kinachofuata ni msongo. Kama hiyo haitoshi, bado mambo ya kufanya yanaongezeka, wakati muda haujawahi (more…)

UKURASA WA 1172; Vitu Viwili Unavyopaswa Kufa Navyo…

By | March 17, 2018

Kuna watu wengi wanaanzia chini kabisa, wanakuwa na hamasa kubwa, wanaweka juhudi kubwa, na juhudi hizo zinazaa matunda, wanaanza kufanikiwa. Lakini haichukui muda wanaanguka. Watu hawa wanakuwa wamefanya kosa moja kubwa, wanakuwa wameshiba, wanakuwa wamezoa kile ambacho wamekuwa nacho kiasi cha kusahau walipotoka na kilichowafikisha pale walipo. Watu pia, wanapoanzia (more…)

UKURASA WA 1171; Kama Hukufa Utotoni, Basi Jua Uwezo Wako Ni Mkubwa Kuliko Unavyofikiri.

By | March 16, 2018

Kitu ambacho nimejifunza kwenye maisha ni kwamba, binadamu huwa tunazaliwa tukiwa na maandalizi ya kutosha kupambana na changamoto za dunia. Mtoto mchanga aliyezaliwa leo, akisikia sauti kali atashtuka, akiona kitu kinakuja mdomoni kwake ataanza kunyonya, akiona kama anaanguka anajishika kwenye kitu. Kumbuka huyu ni mtoto wa siku moja, ambaye hajafundishwa (more…)

UKURASA WA 1170; Maisha Yakiwa Mteremko Sana Unasahau Maono Yako…

By | March 15, 2018

Watu wa kawaida, wanapowaangalia watu waliofanikiwa huwa wanaona kama watu hao wanajitesa. Huwa wanaona watu hao licha ya kuwa na fedha nyingi, maisha yao ni ya kawaida sana na wanaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kazi zao kama vile ndiyo wanaanza. Watu wa kawaida hujiambia kama wakiwa na fedha kama walizonazo (more…)