💥 #GHAHAWA; AKILI INATENGENEZA KILE UNACHOWAZA….

By | May 11, 2017

Habari rafiki kwa kuimaliza siku hii nzuri ya leo. Nina hakika yapo mengi umeshinda leo, na pia yapo ambayo umejifunza, ambayo wengi wanasema wameshindwa. Ila wewe hujashindwa, umejifunza na kesho utafanya kwa ubora zaidi. Karibu kwenye #GHAHAWA jioni ya leo, ambapo tunakwenda kuangalia makosa ambayo tumekuwa tunafanya kwenye kufikiri. Akili (more…)

Mambo Haya Manne Yanakuzuia Wewe Kufikia Ukuu Kwenye Maisha Yako. Yajue Na Uyaepuke Ili Kufanikiwa.

By | May 11, 2017

Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa bora, kila mtu anapenda kufanya mambo makubwa, kuwasaidia wengi, kupata mafanikio na pia kukumbukwa na wengi kwa namna walivyofanya makubwa. Kila mtu ana ukuu ndani yake, ana uwezo mkubwa wa kufanya mambo ya kipekee hapa duniani, mambo ambayo hakuna mwingine awezaye kuyafanya, mambo ambayo dunia (more…)

UKURASA WA 862; Wanachosema Na Wanachofanya….

By | May 11, 2017

Ili kuboresha chochote unachofanya, hasa biashara basi unahitaji maoni ya watu wengine. Unahitaji maoni ya wateja wako, wale ambao wanategemea kile unachowauzia. Na pia unahitaji maoni ya wadau wengine wa karibu ili uweze kuboresha zaidi. Watu wamekuwa wakiomba maoni kwa watu hao muhimu, wanapata maoni na kuyafanyia kazi lakini cha (more…)

💥 #GHAHAWA; UNACHOONA SIYO KINACHOSABABISHA….

By | May 10, 2017

Hongera rafiki kwa mapambano ya siku ya leo. Nina hakika umeweka juhudi za kutosha kadiri ya uwezo wako. Na pale ambapo mambo hayakwenda sawa, kuna kesho, hakikisha unafanya kwa ubora zaidi. Jioni hii karibu kwenye #GHAHAWA ambapo tunashirikishana makosa tunayofanya kwenye kufikiri na namna ya kufikiri sawasawa. Najua kila mmoja (more…)

Sheria Tano Muhimu Za Kufuata Wakati Wa Kuchagua Hisa Za Kununua.

By | May 10, 2017

Hisa ni moja ya aina ya uwekezaji ambapo unaweka fedha yako kwenye makampuni ya umma, fedha inatumika kwenye kuendesha makampuni hayo na baadaye unanufaika kwa thamani ya hisa kuongezeka na/au kupata gawio kutoka kwenye kampuni pale inapotengeneza faida. Uwekezaji kwenye hisa ni moja ya maeneo muhimu ambayo kila mwekezaji anapaswa (more…)

UKURASA WA 861; Tunaona Kilichopo, Na Siyo Kisichokuwepo…

By | May 10, 2017

Leo sijaumwa mguu, Siyo kwamba ni kawaida yangu kuumwa mguu, lakini nimefikiria sijawahi kujiambia hivyo. Zipo siku nyingi ambazo siumwi mguu, lakini sijawahi kuchukua muda na kufikiria namna ambavyo siumwi mguu. Lakini inapotokea siku moja nimeumwa mguu, mawazo yangu yote yanahamia kwenye kuumwa mguu. Nitafikiria zaidi kuhusu kuumwa mguu, japo (more…)

Kubana Matumizi Siyo Mbinu Ya Kutajirika, Mbinu Hasa Ni Hii.

By | May 9, 2017

Linapokuja swala la fedha, kuna vitu vikuu viwili; Cha kwanza ni mapato, kile ambacho unapata kutoka kwenye kazi au biashara ambayo unaifanya. Kitu cha pili ni matumizi, namna ambavyo unatumia kile kipato chako. Changamoto kubwa sana kwenye fedha huwa inaanza pale matumizi yanapozidi mapato, hapo ndipo wengi hujikuta wanaingia kwenye (more…)

UKURASA WA 860; Kitu Kimoja Kilichosababisha Yote…

By | May 9, 2017

Jambo lolote linapotokea, ni kawaida kwa watu kutafuta kitu kimoja kilichosababisha yote. Yaani kile kimoja ambacho ndiyo kisababishi. Iwe ni jambo baya au zuri, mfano inapotokea ajali, kila mtu hutafuta kitu kimoja pekee kilichopelekea ajali ile, labda dereva alikuwa mwendo kasi, au barabara mbovu, au chombo cha usafiri kibovu na (more…)

💥 #GHAHAWA; WALIOPONA NDIYO WANAOANDIKA…

By | May 8, 2017

Hongera kwa siku ya leo rafiki yangu, Najua yapo mengi umejifunza na zipo changamoto umekutana nazo. Hakikisha kila ulichopitia leo, kinakuwa somo kwako hapo kesho, ili uwe bora zaidi. Karibu kwenye #GHAHAWA leo tuangalie namna tunavyokosea kufikiri na hatimaye kufanya maamuzi. Hadithi za watu waliofanikiwa zipo kila mahali, Hadithi za (more…)

Tabia Za Wajasiriamali Wakubwa Ambazo Huwezi Kuzikuta Kwa Watu Wengi.

By | May 8, 2017

Kama wapo watu tofauti, ambao wanafanya kitu kimoja, na kati yao wachache wakawa wanafanya vizuri kuliko wengine, ni dhahiri kuna tofauti kati yao katika utendaji. Hata kama wanaonekana wanafanya kwa usawa kabisa, ukichunguza kwa ndani, utaona zipo tofauti, hata kwa kuanzia kwenye tabia na mtazamo ambao watu hao wanao katika (more…)