UKURASA WA 859; Ujasiri Unahitajika Pia…

By | May 8, 2017

Hakuna kitu utakachofanya, wakosekane watu wa kukukosoa au kukupinga. Pamoja na juhudi kubwa unazoweka, wapo ambao watasema unachofanya siyo sahihi, wengine watasema unapoteza muda, na wapo watakaokushauri kipi hasa ufanye. Hivyo, kitu kikubwa sana unachohitaji, ni ujasiri, kwenye jambo lolote lile ambalo utaamua kufanya. Kwa sababu bila ujasiri, hutaweza kwa (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maana Halisi Ya Kuwa Mtu.

By | May 7, 2017

Karibu mwanafalsafa kwenye makala zetu za falsafa mpya ya maisha, ambapo tunashirikisha na kujenga falsafa mpya ya maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Maisha yetu ni kile tunachotengeneza wenyewe, iwe tunajua au hatujui. Upo hapo ulipo sasa, kutokana na falsafa ambayo umechagua kuiishi, iwe ulichagua kwa kujua au kutokujua. (more…)

UKURASA WA 858; Kuona Unachotaka Kuona…

By | May 7, 2017

Ukiacha kudanganywa na wengine, au kuwadanganya wengine, sisi binadamu tupo vizuri sana kwenye kujidanganya wenyewe. Kwa makusudi kabisa, tunaamua kuacha kuuangalia ukweli na kuangalia kile ambacho tunataka sisi, kile ambacho tunataka kuona. Changamoto kubwa kwenye hili ni kwamba unaweza hata usijue kama unajidanganya. Wewe unaona mambo yanakwenda vizuri tu, kumbe (more…)

Jinsi Unavyoweza Kuwa Mwaminifu Kwenye Ulimwengu Wa Sasa Uliojaa Kila Aina Ya Hila.

By | May 6, 2017

Msingi wetu mkuu tunaouishi kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA. Hizi ni nguzo tatu muhimu sana kwenye mafanikio ya maisha yetu, kuanzia kwenye kazi, biashara, mahusiano, afya na kila eneo la maisha yetu. Uadilifu unaendana sana na uaminifu, japo siyo kitu kimoja. Uaminifu ni kile unachosema na (more…)

UKURASA WA 857; Hakuna Anayejali Zaidi Yako….

By | May 6, 2017

Kuna makosa makubwa sana huwa tunayafanya kwenye kujali, tunafikiri wapo watu wanajali sana kuhusu sisi na maisha yetu kuliko hata tunavyojijali sisi wenyewe. Hili ni kosa tunalorudia mara kwa mara na linazalisha matatizo makubwa kwetu, au kutuzuia kupata kile ambacho tunakitaka. Kwanza tunashindwa kufanya yale ambayo tunataka kufanya, kwa kuona (more…)

FURSA NDANI YA TATIZO; Mambo Matano(05) Ya Kufanya Pale Unapokuwa Umekwama.

By | May 5, 2017

Waswahili wanasema, mipango siyo matumizi. Wakiwa na maana kwamba unaweza kupanga sana, lakini inapofika kwenye utekeleaji, mambo yanaweza kwenda tofauti na ulivyotegemea. Na kwa uzoefu wangu na wengine ambao nimekuwa nawaangalia, mara nyingi sana mambo huenda tofauti kabisa na mategemeo ambayo watu wanakuwa nayo. Inapofika hali kama hii, wengi hukata (more…)

Angusha Na Tawala Watu Hawa Wawili Ili Uweze Kuwa Na Mafanikio Makubwa.

By | May 4, 2017

Kuna watu wawili ambao wamesimama kati yako hapo ulipo wewe na pale ambapo unataka kufika, yaani mafanikio yako kimaisha. Hii ina maana kwamba, ukiweza kuwavuka watu hao wawili, hakuna cha kukuzuia wewe kufika pale unapotaka kufika. Lakini kama ilivyo, shida kubwa ya kutatua tatizo siyo tatizo lenyewe, bali kulijua tatizo. (more…)

UKURASA WA 855; Inayochukua Muda Ni Hatari Zaidi…

By | May 4, 2017

Mtu akiamka asubuhi, na ghafla akagundua anaharisha damu, atakimbilia hospitali mara moja. Kuharisha damu ni tatizo linaloonekana haraka. Lakini iwapo mtu huyu ataamka tu na tumbo likawa linauma na kuacha, hatakuwa na haraka, au kapata choo kimoja chenye rangi isiyoeleweka, ataendelea kusubiri. Inaweza kwenda hivyo kidogo kidogo, mpaka siku anakuja (more…)

Jinsi Ya Kuchagua Uwekezaji Unaokufaa Wewe Kulingana Na Mahitaji Yako.

By | May 3, 2017

Kila mtu ambaye yupo makini na fedha, anataka kufikia uhuru wa kifedha na utajiri, basi uwekezaji ni kitu cha lazima kufanya. Siyo kitu cha kujaribu na wala siyo kitu cha kuangalia kama unaweza, bali ni kitu ambacho unapaswa kujifunza, kukijua kiundani na kuwekeza. Hii ni kwa sababu kadiri umri wetu (more…)