KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

By | February 3, 2017

Habari za leo rafiki yangu? Moja ya changamoto kubwa ambayo watu wengi wamekuwa wanasema inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni muda. Watu wana mipango mikubwa na mizuri sana, lakini wanakosa muda wa kutekeleza mipango yao hiyo mizuri. Watu wanapanga kuanza biashara zao ili kuweza kujitengenezea uhuru wa kifedha, (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; FANYA KILA SIKU…

By | February 2, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Hii ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ili tuweze kupata matokeo bora kabisa. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUFANYA KILA SIKU…. Kama kuna kitu muhimu sana kwenye maisha yako, Kama kuna (more…)

UKURASA WA 764; Samaki Huanza Kuozea Kichwani…

By | February 2, 2017

Popote tunapokutana na changamoto, huwa tunaanza kuangalia nani wa kumlaumu. Na tukishaanza kutafuta wa kulaumu, huwa hatumkosi, kwa sababu ni rahisi kupata watu wa kuwalaumu. Lakini mara nyingi, chanzo cha changamoto kipo wazi. Kama changamoto ni kwenye maisha yako binafsi, basi wewe ndiye unayezisababisha, na siyo mtu mwingine yeyote. Wewe (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; WAO WAMEFANYA NINI?

By | February 1, 2017

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nzuri sana ya leo. Hii ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Nguzo zetu kuu zikiwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu wao wamefanya nini? Kila tunapopanga kufanya mambo makubwa, wapo watu wanaojitolea kutushauri (more…)

UKURASA WA 763; Hakikisha Watu Wanafanya Kile Wanachopaswa Kufanya….

By | February 1, 2017

Kama wapo watu wanaofanya kazi chini yako, labda kwenye ajira una watu ambao wewe unawasimamia, au kwenye kazi shughuli zako umeajiri watu ambao wanakusaidia, basi moja ya majukumu yako ni kuhakikisha watu wanafanya kile wanachopaswa kufanya. Unahitaji kujua kwa karibu na hata kuwakumbusha kuhusu majukumu yao, kuona maendeleo yao na (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; USIWE TAKWIMU….

By | January 31, 2017

Asubuhi njema rafiki, Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo ambapo tunapata nafasi nyingine ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tunafanya. Tutumie nafasi ya leo vizuri ili tuweze kufanya makubwa. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu takwimu. Zipo takwimu nyingi mno kwenye maisha ya kawaida. Mfano wa (more…)

UKURASA WA 762; Hadithi, Mchezo, Ushindi…

By | January 31, 2017

Maneno matatu yanayoweza kubeba mafanikio yako yote kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla. Unaanza na hadithi, hii ni ile ndoto yako kubwa ya maisha, ni yale maono unayoyapata ya namna unataka maisha yako yawe. Nimewahi kukuambia tena ya kwamba maisha ni hadithi, hivyo ni uamuzi wako unataka kuishi hadithi (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; BADILI KITU LEO…

By | January 30, 2017

Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA kwenye kila tunachofanya kwenye maisha yetu, ili kuweza kupata matokeo bora. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kufanya mabadiliko madogo leo. Kama ambavyo tunajua, mafanikio kwenye maisha hayatokei kama ajali, kwamba (more…)

UKURASA WA 761; Ukweli Haulazimishwi…

By | January 30, 2017

Ukweli huwa unabaki kiwa ukweli, haulazimishwi wala haubembelezwi, bali unakuwa wazi na kila mtu anajionea mwenyewe. Ukiona mtu analazimisha ukweli, jua kuna kitu kinafichwa ndani yake. Ukiona wewe mwenyewe unalazimisha ukweli ili watu waamini kwenye kile unachotaka waamini, basi jua kuna shida mahali. Na shida kubwa ni kwamba siyo ukweli, (more…)

UKURASA WA 760; Siyo Mara Moja, Ni Kila Mara…

By | January 29, 2017

Tangu umezaliwa mpaka hapo ulipo sasa, kila siku unakula, jana ulikula, leo umekula na kesho utakula, hatuna shaka juu ya hilo. Siku zote za maisha yako umekuwa unaufanyia usafi mwili wako, na kila siku utaendelea kufanya hivyo, utaoga na kusafisha nguzo zako, ni maisha ya kila siku, siyo kitu cha (more…)