KUJIAMINI; Madhara Ya Kujiamini Na Kutokujiamini.

By | November 18, 2014

Habari za leo mwana mafanikio? Karibu kwenye kipengele cha tabia za mafanikio na mwezi huu tunaendelea na kujijengea tabia ya kujiamini. Kama tulivyoona kwenye makala zilizopita, kujiamini ni muhimu sana ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Kama utakosa kujiamini utakuwa umejiwekea kikwazo kikubwa sana kuweza kufikia mafanikio. Leo tutajadili madhara ya (more…)

Mbinu tano za kufanikiwa kwenye ujasiriamali.

By | November 17, 2014

Kila mjasiriamali ana ndoto siku moja aweze kufikia mafanikio makubwa sana. Haijalishi ni kiwango gani cha mafanikio ulichofikia mpaka sasa, bado unahitaji kukua zaidi na kufikia mafanikio zaidi. Ndio maana hata wajasiriamali waliofanikiwa sana bado wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa kila siku ili waendelee kufanikiwa zaidi. Kama umejikuta tu (more…)

Hivi ndivyo unavyoweza kuianza wiki yenye mafanikio.

By | November 17, 2014

Habari za asubuhi rafiki?Ni siku nyingine mpya na mwanzo wa wiki mpya.Naamini umeipangilia wiki yako vizuri kwa ajili ya kufikia mafanikio makubwa.Wiki hii fanya kitu hiki kimoja;Dhibiti kiwango cha taarifa unazopata, hasa kupitia vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu taarifa nyingi ni;i. Zinakula muda wako mwingiii. Ni hasiiii. Hazina (more…)

THE RICHEST MAN; Mkopeshaji Fedha Wa Babeli – 2.

By | November 15, 2014

Baada ya kumaliza mfano ule wa maksai na farasi, Mathon alimuuliza Rodan amejifunza nini kwenye mfano ule? Rodan alijibu ni hadithi nzuri ila hajajifunza chochote. Mathon alimwambia somo la kujifunza hapo ni rahisi sana; kama unataka kumsaidia rafiki yako msaidie kwa njia ambayo haitaleta matatizo yake kwako. Mathon alimwambia kabla (more…)

THE RICHEST MAN; Mkopeshaji Fedha Wa Babeli.

By | November 13, 2014

Rodan aliyekuwa mtengeneza spea wa babeli alikuwa na vipande hamsini vya dhahabu. Alitembea njiani kwa maringo huku dhahabu ikitikisika kwenye mifuko yake. Haijawahi kutokea kwenye maisha yake akawa na kiasi kikubwa vile cha dhahabu. Kiasi hiko cha dhahabu kingemwezesha kununua chochote alichokuwa anataka iwe ni ardhi, nyumba, farasi na kadhalika. (more…)