KUJIAMINI; Uhusiano Kati Ya Kujiamini Na Mafanikio Mkubwa.

By | November 11, 2014

Tafiti nyingi zinaonesha kwamba kujiamini ni kiungo muhimu sana cha mtu kuweza kufikia mafanikio makubwa. Ukiangalia, watu wengi waliofanikiwa wanajiamini kwa kiasi kikubwa. Japokuwa kuna watu ambao wanajiamini ila hawana mafanikio na pia kuna watu ambao wana mafanikio makubwa ila hawajiamini kabisa. Pamoja na hayo, kujiamini kunakuongezea nafasi ya kufikia (more…)

Njia tano za kuongeza mauzo kwenye biashara yako.

By | November 10, 2014

Katika ujasiriamali na biashara kila mfanya biashara anajua kwamba fedha ndio damu ya biashara. Kama hakutakuwa na mzunguko wa fedha wa kutosha kwenye biashara ni sawa na mtu ambaye hana damu ya kutosha na hivyo itapelekea kufa kwa biashara. Na njia kubwa ya kuongeza mzunguko wa fedha kwenye biashara yoyote (more…)

Mambo 21 muhimu ya kiufanya kila siku ili kuwa na maisha yenye mafanikio.

By | November 9, 2014

HABARI ZA LEO RAFIKI?Naomba nikushirikishe Vitu 21 rahisi vya kufanya kila siku ili kuwa na maisha yenye furaha na mafanikio.i. Lala masaa nane kwa siku.ii. Kula milo miwili kwa siku.iii. Usiangalie TViv. Usile vyakula vya harakav. Usilaumu wala kulalamikavi. Usisengenye, usishiriki majungu na umbea.vii. Onesha shukrani kwa marafiki.viii. Andika orodha (more…)

Nguzo Kuu Ya Uongozi; Tekeleza Kile Unachoahidi.

By | November 9, 2014

Katika kujijenga kuwa kiongozi bora na imara kuna misingi mingi ya uongozi ambayo unatakiwa kuifuata. Kushindwa kufuata misingi hii kutapelekea uongozi wako kushindwa na hata kudharaulika sana. Moja ya nguzo muhimu za uongozi ni kutekeleza kile unachoahidi. Kuongea ni rahisi sana na hivyo watu wengi hujikuta wakiongea mambo ambayo hawana (more…)

NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Msamaha

By | November 7, 2014

Forgiveness is all about me giving up my right to hurt you for hurting me. Msamaha ni pale ambapo mimi naamua kupoteza haki yangu ya kukuumiza wewe kwa kuniumiza mimi. Unaposamehe unaepuka kutengeneza maumivu zaidi. Amua leo kuwasamehe wote waliokuumiza, maana kuendelea kukaa na kinyongo unazidi kuumia wewe. Nakutakia siku (more…)

RICHEST MAN; Sheria Tano Za Fedha – 1

By | November 6, 2014

Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON. Ukipewa mfuko uliojaa fedha na kitabu chenye maneno ya busara utachagua nini? Hili ni swali ambalo liliulizwa na Kalabab kwa watu 27 waliokuwa kwenye mjadala. Watu wote walijibu watachukua mfuko wa fedha. Kalabab alishangaa na kuendelea kusema, sikia mbwa mwitu (more…)