Mambo Muhimu Ya Kuzingati Wakati Wa Kujenga Nidhamu Binafsi.

By | September 23, 2014

Kujenga nidhamu binafsi sio kazi rahisi. Kuna changamoto nyingi sana ambazo utakutana nazo na kama hujajipanga vizuri unaweza kukata tamaa na kuacha kabisa. Wiki iliyopita tulijadili jinsi ya kujenga nidhamu binafsi. Baada ya kujua hayo leo tutajifunza mambo muhimu ya kuazingatia wakati wa kujenga nidhamu binafsi. Hapa kuna mambo matano (more…)

Sababu 5 Kwa Nini Ni Marufuku Wewe Kukata Tamaa.

By | September 23, 2014

Katika maisha kuna wakati ambapo mambo huwa magumu sana. Ni katika nyakati hizi ambapo watu wengi hukata tamaa na kuacha kile ambacho walikuwa wanafanya. Kwa kukata tamaa unashindwa kufikia mafanikio na pia unaona maisha yako kama hayana maana. Leo JIONGEZE na sababu hizi tano kwa nini ni marufuku wewe kukata (more…)

Mambo 5 Muhimu Ya Kufanya Kabla Hujalala Leo.

By | September 22, 2014

Siku ya leo ndio inaelekea kuisha na kwa siku nzima ya leo umepitia mambo mengi sana. Kuna mengi umefanikiwa kufanya leo na pia kuna ambayo umepata changamoto kubwa. Hata kama siku yako ilikuwa mbaya kiasi gani, kuna mambo mazuri uliyojifunza kwa siku hii. Hapa kuna mambo matano muhimu unayotakiwa kufanya (more…)

SIKU YA 22; Akili Yako Ya Ndani Inaweza Kukufikisha Kwenye Mafanikio Makubwa.

By | September 22, 2014

Ni kweli kwamba kuna nguvu kubwa sana ya uumbaji katika akili yako ya ndani(subconscious mind) ambayo inaweza kukuletea chochote unachotaka. Nguvu hii ni kubwa kama ile inayodhaniwa kuwa nguvu ya majini katika hadithi za Allannin, ambapo unasema kitu na kinatokea. Leo tutajifunza jinsi unavyoweza kutumia nguvu hii kufikia mafanikio makubwa. (more…)

Biashara 5 Unazoweza Kuanza Kufanya Bila Ya Kuwa Na Mtaji.

By | September 22, 2014

Kikwazo kikubwa cha watu wengi kuingia kwenye biashara kimekuwa ni mtaji. Japo sio kweli kwamba mtaji pekee ndio kikwazo, lakini wengi wanaamini mtaji tu ndio unawazuia. Lakini pia wakati huo ambao mtu hana mtaji hakuna juhudi kubwa anazofanya ili kuhakikisha anapata mtaji huo. Sasa kufupisha habari leo JIONGEZE na biashara (more…)

Njia tano unazoweza kutumia kuongeza kipato chako kwenye biashara.

By | September 22, 2014

Moja ya changamoto ambazo zinawakabili wajasiriamali wengi ni kipato kidogo kutoka kwenye ujasiriamali wao au biashara zao. Watu wengi wamekuwa kwenye ujasiriamali kwa muda mrefu ila hawaoni mabadiliko makubwa kwenye kipato chao. Hali hii imefanya biashara za watu wengi kudumaa na hatimaye kufa kabisa. Leo tutajadili njia tano unazoweza kutumia (more…)

NENO LA LEO; Kuhusu Zawadi Kubwa Uliyopewa.

By | September 22, 2014

Everyone is gifted – but some people never open their package!   Kila mtu amezawadiwa, lakini baadhi ya watu hawafungui maboksi yao. Kama unajiona wewe ni mtu ambaye huna bahati au huna kipaji chochote na kuna wengine ndio bora zaidi basi hujajijua vizuri. Kaa chini na utafakari kwa kina utaiona (more…)

Mambo Matano(5) Ya Kufanya Siku Ya Jumatatu Ili Kuwa na Wiki Yenye Mafanikio.

By | September 22, 2014

Jumatatu ndio siku inayochukiwa na watu wengi kuliko siku nyingine yoyote ya wiki. Siku hii imepewa majina mabaya sana likiwemo BLUE MONDAY. Jumatatu ni siku ambayo watu wanatoka kwenye mapumziko na kuanza tena kazi. Ni siku ambayo watu wanajua kuna siku tano za kazi mbele, na kama hupendi kazi yako (more…)