Tag Archives: SIRI 50 ZA MAFANIKIO

SIRI YA 20 YA MAFANIKIO; Iendee Dhahabu…

By | February 17, 2015

Watu waliofanikiwa sana sio watu wanaokubali kuwa kawaida. Hawakubali kuwa bora wa piku. Hawaridhishwi na kufanya vitu kama kila mtu anavyofanya. Washindi siku zote wanaongeza kiwango chao. Wanataka kufanikiwa zaidi na wanataka kila wanachofanya kuwa cha daraja la kwanza. Wanakwenda hatua ya ziada. Wanaweka jitihada zisizo za kawaida kwenye kile (more…)

SIRI YA 19 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kuongeza Kipato Chako Mara Mbili.

By | February 12, 2015

Chukua wastani wa kipato cha watu watano unaokaa nao muda mrefu na utapata kipato chako. Asilimia tisini ya mafanikio yako yanaamuliwa na watu unaokaa nao muda mrefu. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu watu wenye mafanikio wanafikiri tofauti na watu wasiofanikiwa na wewe unafikiri kama wale wanaokuzunguka wanavyofikiri. Kama unataka (more…)

SIRI YA 18 YA MAFANIKIO; Fanya Kitu Unachopenda…

By | February 12, 2015

Tafuta uwanja unaopendelea kufanyia kazi. Fanya kitu ambacho unakifurahia. Fanya kitu ambacho uko tayari kukifanya bure. Maisha ni mafupi sana kufanya kitu ambacho hukipendi. Kama utapenda kazi/biashara unayofanya, hakuna kitakachokuzuia kufikia mafanikio.    “I never did a day’s work in my life. It was all fun.”  – Thomas Edison (more…)

SIRI YA 17 YA MAFANIKIO; Una Hamu Kiasi Gani Ya Kufikia Ndoto Yako?

By | February 12, 2015

Hamu kubwa unayokuwa nayo kwenye kitu unachotaka ndio inapima kama utaweza kukipata. Kama una hamu kubwa sana ya kupata kitu, hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kukipata. Hata utapokutana na changamoto lazima utapata njia. Hamu kubwa ya kupata kitu inakupa nguvu ya kulipa gharama ya mafanikio. Unaweza kujitengenezea hamu, kuichochea hamu na (more…)

SIRI YA 16 YA MAFANIKIO; Jifunze Kutokana Na Makosa Yako Na Jipange Kufanikiwa.

By | February 11, 2015

Fursa zinakuja na kuondoka. Maisha yana nyakati ambazo zinakuja na kuondoka kama mawimbi ya bahari. Mwogeleaji anapokosa wimbi moja hakai chini na kujutia, bali hujifunza kutokana na makosa yao na kujiandaa vizuri kwa wimbi lijalo. Kuwa kama mwogeleaji kwa kuangalia fursa, jiweke kwenye nafasi ya kushinda. “Luck is the sense (more…)

SIRI YA 15 YA MAFANIKIO; Mafanikio ni Hatua Kwa Hatua.

By | February 11, 2015

Hakuna kitu kama mafanikio ya haraka. Ni lazima uweke misingi siku kwa siku na kwa muda mrefu sana. Ni lazima uweze kusinda mapambano madogo madogo mengi kabla ya kukutana na mapambano makubwa. Nyumba zinajengwa tofali moja baada ya jingine. Mashindano ya mpira yanasindwa kwa mechi moja baada ya nyingine Biashara (more…)

SIRI YA 14 YA MAFANIKIO; Tengeneza Ujasiri Wa Kufanikiwa.

By | February 8, 2015

Ujasiri unamaanisha kuwa mkubwa kuliko matatizo yako. Ujasiri sio kutokuwepo kwa woga. Ni kuweza kutenda licha ya kuwa na hofu. Kufanikiwa kwenye maisha unahitaji ujasiri wa aina mbili; 1. Ujasiri wa kuanza kuchukua hatua na kutenda. Ujasiri huu unatokana na kujiamini wewe mwenyewe. 2. Ujasiri wa kuendelea kutenda. Ujasiri huu (more…)

SIRI YA 13 YA MAFANIKIO; Fanya Kazi Na Wengine Ili Kila Mmoja Anufaike.

By | February 8, 2015

Kujenga mahusiano mazuri na watu ni jambo muhimu sana kufikia mafanikio yako. Hii ni kwa sababu mafanikio yako yanategemea sana mchango wa watu wengine. Unaweza kufanikisha mengi ukiwa na wengine kuliko unavyoweza ukiwa mwenyewe. Jua ni jinsi gani wengine wanaweza kunufaika na wewe na hii itawafanya waweze kushirikiana na wewe (more…)

SIRI YA 12 YA MAFANIKO; Shika Hatamu Ya Maisha Yako.

By | February 7, 2015

Wewe ndio msimamizi wa maamuzi yako. Pale unapompa mtu mwingine mamlaka haya unaacha kuwa kiongozi mkuu wa maisha yako. Pale unapochukua majukumu ya maisha yako unakuwa msimamizi mkuu wa maisha yako. Chukua hatima ya maisha yako, na utaamua maisha yako yaweje. “If you don’t run your own life, someone else (more…)

SIRI YA 11 YA MAFANIKIO; Yazike Mawazo Hasi

By | February 7, 2015

Changamoto kubwa kwenye njia ya mafanikio ni kuweza kuitawala nafsi yako. Haijalishi unafanya nini, kuna wakati utakuwa na wasiwasi kama unaweza au kuwa na mtafaruku ndani ya nafsi yako kama ufanye au usifanye kile kitakachokufikisha kwenye malengo yako. Mara zote jiulize ni kitu gani kikubwa naweza kufanya sasa na kikanisogeza (more…)