2364; Jifunze, Nufaika, Fundisha…

By | June 21, 2021

2364; Jifunze, Nufaika, Fundisha… Kusudi kuu la maisha ya viumbe wote hapa duniani ni kuzaliana. Na siyo tu kuzaliana, bali kuzaliana kwa namna ambayo ni bora kabisa. Hivi ndivyo mageuzi yamekuwa yanatokea duniani, viumbe hai wanayakabili mazingira, wanabadilika kulingana na mazingira hayo na kisha kuzaa viumbe hai walio bora zaidi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA WEWE YAMEKUSHINDA, UNADHANI WENGINE WATAWEZA?

By | June 21, 2021

Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe. Hilo ndiyo jukumu lako kubwa unalopaswa kulipa kipaumbele kikubwa. Kitu chochote ambacho unataka watu wakupe, lazima uanze kujipa wewe mwenyewe. Ukitaka wakupende, jipende. Ukitaka wakukubali, jikubali. Na ukitaka wakuheshimu, jiheshimu. Kama wewe mwenyewe unashindwa kujipa vitu hivyo, unadhani wengine watawezaje (more…)

2363; Hiyo siyo kazi yao…

By | June 20, 2021

2363; Hiyo siyo kazi yao… Unataka kila mtu akubaliane na wewe ndiyo ufanye kile unachotaka, unajichelewesha bure. Unataka kila mtu akupende ndiyo uone umekamilika, utasubiri sana. Unataka watu wakuheshimu ndiyo ujione una thamani, utazidi kujipoteza. Siyo kazi ya wengine kukupenda, kukukubali na kukuheshimu, hiyo ni kazi yako mwenyewe. Kinachowatofautisha wanaofanikiwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FURAHIA CHANGAMOTO…

By | June 20, 2021

Wakati wengine wanazichukoa na kuzikimbia changamoto, wewe unapaswa kuzifurahia na kuzikaribisha, kwa sababu ndani yake huwa zina fursa nzuri za ukuaji zaidi kwako. Hutaweza kuziona fursa hizo nzuri kama utaona changamoto ni mbaya. Hivyo anza na mtazamo kwamba changamoto ni nzuri kisha jiulize ni fursa zipi nzuri zilizo ndani ya (more…)

2362; Fursa zilizo ndani ya changamoto…

By | June 19, 2021

2362; Fursa zilizo ndani ya changamoto… Tunaposema kila changamoto ina fursa ndani yake, siyo ru kujifurahisha kwa kuwa chanya, bali ndiyo uhalisia. Hata kama linalokukabili ni kubwa na baya kiasi gani, bado kuna mazuri mengi ndani yake ambayo unaweza kuyafanyia kazi. Kama huzioni fursa zilizo kwenye changamoto, siyo kwa sababu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKIWA NACHO UTAJUA…

By | June 19, 2021

Ukiwa na furaha utajua, huhitaji kujiuliza mara mbilimbili kama una furaha au la. Ukifanikiwa utajua, huhitaji kujihoji kama umefanikiwa. Mambo yote muhimu kwenye maisha, unayajua wazi kama unayo au la na kama bado unajiuliza, basi jibu ni huna. Tafakari ni maswali gani umekuwa unajiuliza mara kwa mara, jua nini unakosa (more…)

2361; Kama Bado Unajiuliza, Jibu Ni Hapana…

By | June 18, 2021

2361; Kama Bado Unajiuliza, Jibu Ni Hapana… Kama bado unajiuliza kama una furaha au la, jibu liko wazi, huna furaha. Wenye furaha hawapotezi muda kujiuliza kama wana furaha au la, bali wanayafurahia maisha yao. Kama bado unajiuliza kama mtu anakupenda au la, jibu unalo, hakupendi. Upendo ukiwepo huwa uko wazi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIHARAKISHE PASIPO NA UMUHIMU…

By | June 18, 2021

Huwa tunafikiri tutayafurahia maisha baada ya kupata vitu fulani au kufika hatua fulani. Tunaharakisha kufika huko na hatuipati hiyo furaha. Furaha haipo kwenye matokeo, bali kwenye mchakato. Hivyo unapaswa kuweka umakini wako kwenye kile unachofanya, kiwe ndiyo muhimu kabisa na kukipa muda wa kutosha. Kila unapochagua kufanya kitu, kinapaswa kuwa (more…)