Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; JINSI UNAVYOFANYA KITU KIMOJA NDIVYO UNAVYOFANYA KILA KITU…

By | May 18, 2019

“Pay attention to what’s in front of you—the principle, the task, or what’s being portrayed.” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.22 Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi (more…)

1598; Wasiwasi, Kujitelekeza, Kujidharau Na Kiburi…

By | May 17, 2019

Hizi ni sumu nne kubwa za mafanikio makubwa. Ni mambo ambayo wengi wamekuwa wanafanya kwa mazoea, lakini ni kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio yao. Hupaswi kuwa na wasiwasi au mashaka juu yako. Unapojiwekea malengo na mipango yako, unapaswa kujiamini kwamba utayafikia. Usianze kujiwekea wasiwasi na mashaka, kwa sababu ukisharuhusu hali (more…)

1597; Iamini Dunia Na Hofu Zitapotea Zenyewe…

By | May 16, 2019

Chanzo kikuu cha hofu kwenye maisha yetu ni kukosa imani kwenye dunia na kwetu wenyewe. Kuna kitu tunakuwa tunataka, lakini tunapoangalia nafasi ya kuweza kukipata, na hatari iliyopo kwenye kukikosa tunapata hofu kubwa. Tunajiuliza vipi kama tukijaribu na tukashindwa, au vipi kama mambo yakienda tofauti na jinsi tulivyopanga? Huwa tunataka (more…)

1596; Utamu Upo Kwenye Safari Yenyewe Na Siyo Mwisho Wa Safari…

By | May 15, 2019

Tumekuwa tunachagua kuyapoteza maisha yetu wenyewe kwa kuweka mkazo kwenye maeneo ambayo siyo sahihi. Mara nyingi tumekuwa tunaangalia mwisho wa safari yetu, kisha kujiambia kama tukifika pale basi tutakuwa na furaha kubwa na maisha yetu yatakuwa mazuri sana. Tunakazana kweli kweli, tunaweka maisha mengine pembeni na kuhakikisha tunafika pale tulipopanga (more…)

1595; Kinachokukwamisha Ni Hujaamua Nini Hasa Unachotaka…

By | May 14, 2019

Kuna changamoto kubwa sana kwenye zama tunazoishi kwa sababu machaguo ni mengi mno. Watu walioishi kipindi cha nyuma, hawakuwa na machaguo mengi kama tuliyonayo sasa. Kazi au biashara zilikuwa ni chache na moja kwa moja watu walielekea kwenye kile wanachofanya na kuweka nguvu zao zote hapo. Lakini sasa hivi machaguo (more…)