Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1464; Kucheka Makosa Ya Wengine…

By | January 3, 2019

Ni rahisi sana kwetu kuyaona makosa ya wengine, Ni rahisi kuyaonesha na hata kuyaelezea, Ni rahisi pia kuyacheka na kukejeli makosa ya wengine, Kwa sababu tunafikiri sisi hatuwezi kufanya makosa kama hayo, hatuwezi kuwa wajinga kiasi hicho. Lakini huku kote ni kujidanganya. Kosa lolote analoweza kufanya mwingine, wewe pia unaweza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIWE NA HURUMA KWW VITU VISIVYOKUWA NA UMUHIMU…

By | January 3, 2019

“How many have laid waste to your life when you weren’t aware of what you were losing, how much was wasted in pointless grief, foolish joy, greedy desire, and social amusements—how little of your own was left to you. You will realize you are dying before your time!” —SENECA, ON (more…)

1463; Changamoto Zinakuwezesha Kukua Na Kukuletea Fursa Zaidi…

By | January 2, 2019

Huwa tunatamani sana kuwa na maisha ambayo hayana changamoto yoyote. Maisha ambayo tunapata kila tunachotaka kwa namna tunavyotaka na wakati tunaotaka. Maisha ambayo hayana misukosuko, kila kitu kinakwenda vizuri kabisa. Japo hii ni ndoto nzuri, lakini ikiwa kwenye uhalisia ni hatari sana. Hakuna maisha hatari na mabovu kama ambayo mtu (more…)

1462; Machaguo Makuu Matatu Kwenye Maisha…

By | January 1, 2019

Kwenye maisha yetu tuna machaguo makuu matatu; ZAIDI, KIDOGO, NA SAWASAWA. ZAIDI. Kwenye maisha yako kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifanya zaidi, hivi ni vile vitu vizuri vinavyokupeleka kwenye mafanikio makubwa. Kadiri unavyofanya zaidi vitu vizuri, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kufanikiwa zaidi. KIDOGO. Kwenye maisha yako kuna vitu ambavyo unapaswa (more…)

1460; Kitu Kimoja Pekee Kitakachobadili Kabisa Maisha Yako…

By | December 30, 2018

Watu wengi wamekuwa wakitafuta kitu kimoja pekee ambacho kitayabadili sana maisha yao. Wanaamini kuna kitu kimejificha mahali, ambapo wakikijua au kukipata basi wataweza kupata kila wanachotaka. Wengi itafuta kitabu kimoja pekee ambacho wakikisoma kitabadili sana maisha yao. Wengine wanatafuta wazo moja pekee la biashara ambalo wakilitekeleza maisha yao yatakuwa bora. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; AMINI LAKINI THIBITISHA…

By | December 30, 2018

Hongera sana rafiki yangu mpendwa kwa siku hii mpya kabisa ya leo. Ni ukurasa mwingine mpya kwenye kitabu cha maisha yetu ambapo tumepata nafasi nyingine ya kukiandika kitabu hiki kwa vile tunavyotaka sisi wenyewe. Kwa kuitumia siku hii ya leo vizuri, kwa kuweka juhudi kubwa na kusimamia vizuri muda wetu, (more…)