Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; NGUVU INAYOKUVUTA CHINI….

By | September 21, 2018

“We must all wage an intense, lifelong battle against the constant downward pull. If we relax, the bugs and weeds of negativity will move into the garden and take away everything of value.” —Jim Rohn AMKA Mwanamafanikio, AMKA kwenye siku hii nyingine nzuri sana ya leo, Siku ambayo tumepata nafasi (more…)

BIASHARA LEO; Kuuza Vitu Vya Kawaida Kwa Watu Wa Kawaida…

By | September 20, 2018

Kwenye maisha, kitu ambacho ni rahisi kufanya, pia ni rahisi kutokufanya. Pia kitu ambacho ni rahisi kufanya, huwa hakina thamani kubwa, huwa hakilipi kama mtu anavyoweza kuwa anataka. Hivyo kwa kifupi, tunaweza kusema kuchagua kufanya vitu rahisi, ni kujiweka kwenye mstari wa kushindwa. Njia rahisi ya kuingia kwenye biashara ni (more…)

UKURASA WA 1359; Ni Jukumu Lako, Lipokee Na Songa Mbele…

By | September 20, 2018

Kama huna furaha kwenye maisha yako, kama hufurahii jinsi maisha yako yanavyokwenda, hilo ni jukumu lako, pokea jukumu hilo, chukua hatua na songa mbele. Kama kuna matokeo ya tofauti uliyoyapata kwenye maisha yako, matokeo ambayo siyo uliyotegemea, hilo ni jukumu lako, pokea matokeo hayo, chukua hatua sahihi na songa mbele. (more…)

BIASHARA LEO; Kujenga Imani Ya Wateja Kwenye Bei…

By | September 19, 2018

Wafanyabiashara ndiyo tunaoharibu biashara zetu wenyewe, kwa sababu tunashindwa kutengeneza uaminifu kwenye biashara zetu. Mtu akija kwenye biashara yako, atauliza punguzo la bei, kwa sababu anajua na wewe utakuwa umeweka bei ya juu ili ukiulizwa punguzo uuze kwa bei unayotaka kuuza. Sasa hii ni njia ya hovyo sana ya kuendesha (more…)

UKURASA WA 1358; Kuwasiliana Na Kupiga Kelele…

By | September 19, 2018

Tunaishi kwenye zama za taarifa, zama ambazo taarifa ndiyo nguzo kuu ya mafanikio. Wale wenye taarifa sahihi ndiyo wanaoweza kufanya maamuzi sahihi na kufanikiwa sana. Lakini pia zama hizi zimekuwa na changamoto zake, zimekuwa zama ambazo tunaweza kusema ni zama za kelele. Kwa sababu kila mtu ana nafasi ya kutoa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MFULULIZO WA MAJARIBU…

By | September 19, 2018

AMKA Mwanamafanikio, Amka kwenye siku hii nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kujitengenezea Upendeleo Kwenye Biashara Yako…

By | September 18, 2018

Umewahi kwenda kwenye biashara mbili ambazo zinafanana, ukakuta kwenye biashara moja watu wamejipanga mstari kusubiri huduma, wakati biashara nyingine haina mteja kabisa? Yaani watu wapo radhi kusubiri wapate huduma kwenye biashara wanayotaka, kuliko kwenda kupata huduma pengine ambapo wangeokoa muda zaidi. Waswahili watakuambia anayejaza wateja anatumia dawa, au ushirikina, au (more…)

UKURASA WA 1357; Nje Pakitibuka, Ndani Panapaswa Kutulia…

By | September 18, 2018

Wapo watu ambao huwa wanasumbuliwa sana na shambulio la mshtuko, kitu fulani kinatokea na kuwashtua sana kiasi kwamba wanaogopa au kuhofia kabisa kufanya kitu hicho au hata kingine. Mara nyingi watu huwa wanakuwa na mipango mizuri wanapoanza kitu chochote, lakini wanapoendelea kufanya, wanakutana na changamoto, ambayo inavuruga mipango yao, na (more…)