Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Tengeneza Sanaa Ya Maisha Yako.

By | October 20, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 161 – 170. Kama ilivyokuwa kwa Socrates, kila mmoja wetu ana kitu ndani yake, ambacho kinaweza kuinufaisha dunia. Kitu hichi kinatoka ndani yake na kwakukifanya mtu anapata furaha na kuridhika sana. Na (more…)

UKURASA WA 1024; Kuna Wewe Mmoja Tu Hapa Duniani, Mtumie Vizuri…

By | October 20, 2017

Kuna safari moja, kwenye njia moja ambayo kuna mtu mmoja pekee anayeweza kufanya safari hiyo. Mtu huyo ni wewe mwenyewe. Wewe, upo mmoja tu hapa duniani, hakuna kama wewe, hajawahi kutokea na wala hatakuja kutokea. Na hii ndiyo siri kubwa sana ya maisha yetu hapa duniani, ambaye hakuna aliyeweza kuing’amua. (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jiimarishe Kiroho.

By | October 19, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross UKURASA; 151 – 160. Licha ya kwamba Socrates hakuwa na umiliki wa mali yoyote ile, Licha ya kudhihakiwa na watu wengi, Na licha ya kuhukumiwa kifo na kuchagua kufa, Socrates alikuwa mtu mwenye (more…)

UWEKEZAJI LEO; Maana Ya Gawio Katika Uwekezaji Na Utolewaji Wake.

By | October 19, 2017

Kampuni au taasisi ambayo inauza hisa zake kwenye soko la hisa, inapaswa kutoa hesabu zake za mwaka kila mwaka. Katika hesabu hizi kampuni itaonesha mapato, matumizi, faida na hata hasara. Iwapo kampuni imepata faida mwisho wa mwaka wa fedha, faida ile inapaswa kurudi kwa wanahisa wa kampuni hiyo. Ile sehemu (more…)

UKURASA WA 1023; Tatizo Siyo Waliokuzunguka, Tatizo Ni Wewe…

By | October 19, 2017

Wapo watu wengi ambao wamekwama, wameshindwa kupiga hatua walizopanga kupiga. Ukiwauliza kwa nini wameshindwa, au pale wanapojiuliza wao wenyewe, wanasema wale waliowazunguka ni kikwazo kikubwa kwao kupiga hatua. Labda ni mwajiriwa ambaye mwajiri wake amekuwa kikwazo, au wafanyakazi wenzake wamekuwa changamoto kwake. Au ni mtu ambaye mwenza wake amekuwa kikwazo (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Ongea Ukweli Mara Zote.

By | October 18, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 141 – 150. Socrates alisifika kwa kuhoji kila jambo mpaka kujua ukweli wake. Alimhoji kila mtu kwa kila jambo. Hapakuwa na mtu au kitu ambacho Socrates hakuhoji au kuchimba zaidi. Jambo hili (more…)

BIASHARA LEO; Kila Msaidizi Wako Kwenye Biashara Anapaswa Kujibu Swali Hili Kwa Ufasaha…

By | October 18, 2017

Kumekuwa na changamoto kubwa kwenye kupata wasaidizi wa biashara wenye uwezo mzuri wa kufanya kazi kwenye biashara. Uaminifu na kujituma ni vitu ambavyo vinakosekana kwa wengi tunaowapata watusaidie kwenye biashara zetu. Pamoja na changamoto kuwa kwenye tabia za watu, lakini sisi wamiliki wa biashara pia tuna mchango katika hilo. Kuna (more…)