Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#KURASA_KUMI; Matatizo ya dunia yataisha iwapo itatawaliwa na wanafalsafa.

By | September 28, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa; 177 – 186.. Mwanafalsafa Plato, kupotia kitabu chake cha The Republic, aliandika kwamba dunia itatulia na kuwa sehemu salama, iwapo wanafalsafa wataitawala dunia. Aliamini changamoto ambazo dunia inipitia, zinaweza kutatuliwa na wanafalsafa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KISICHOWEZA KUSUBIRI NUSU SAA…

By | September 28, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi ya leo (more…)

UWEKEZAJI LEO; Dalali Wa Soko La Hisa Ni Mtu Wa Aina Gani Na Jinsi Ya Kuchagua Dalali Mzuri.

By | September 28, 2017

Wengi wetu tunaposikia neno dalali tunajua ni mtu ambaye anafanya biashara ya kuuza vitu vya wengine, kwa kuongeza bei ili apate fedha. Kwa fikra hizi tuna mtazamo mbaya kuhusu madalali na kuona ni watu wanaolangua wengine. Hivyo tunaposikia tena kwenye soko la hisa kuna madalali, tunastuka na kukosa amani. Tunajiuliza (more…)

UKURASA WA 1002; Kujua Kila Kitu Na Kujifunza Kila Kitu…

By | September 28, 2017

Nimekuwa natumia muda mwingi kusoma na kujifunza falsafa mbalimbali ambazo zimekuwepo duniani. Na kitu kimoja ambacho najifunza ni kwamba, karibu kila falsafa tunayoijua ina msingi wake kwenye mafundisho ya mwanafalsafa Socrates. Kila msingi wa falsafa, una ufanano na misingi ya kifalsafa iliyoasisiwa na Socrates. Na hata misingi mingi ya kidini, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KINACHOTOKEA SASA…

By | September 27, 2017

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi ya (more…)

#KURASA_KUMI; Jinsi ya kutawala fikra zako na kudhibiti maisha yako.

By | September 27, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 167 – 176. Miaka mingi iloyopita, mwanafalsafa Plato alisema kwamba sisi binadamu tuna nafsi zaidi ya moja. Na kinachofanya maisha yetu kuwa magumu, niale tunaposhindwa kudhibiti kila nafsi na kujikuta tunataka kuirishisha (more…)

BIASHARA LEO; Weka Roho Yako Kwenye Biashara Yako.

By | September 27, 2017

Najua unajua kwamba utandawazi umeifanya dunia kuwa kijiji. Kila siku dunia inazidi kuwa ndogo zaidi na zaidi. Na hili limekuwa na madhara makubwa sana kwenye biashara. Kwa mfano, siku za nyuma watu walifikiri ukishakuwa na biashara yako eneo fulani na ukaweza kuikuza pale, basi hakuna kinachoweza kukuhatarisha kama utakuwa mwangalifu (more…)

UKURASA WA 1001; Utakutana Na Bahati…

By | September 27, 2017

Kwenye maisha huenda umewahi kuona mambo yametokea kwa watu na kusema watu hao wana bahati kweli. Labda wanakuwa wamekutana na kitu ambacho kimerahisisha zaidi safari yao ya mafanikio. Wakati mwingine ni wewe unakuwa umekutana na hali fulani na kujiona mwenye bahati, au wengine wakasema una bahati sana. Swali ni je (more…)

#KURASA_KUMI; Ubepari unastawi kwa kutengeneza mateso kwa wengi.

By | September 26, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 153 – 166 Wanafalsafa ambao wanapingana na mifumo ya kijamii iliyopo, CYNICS wanatuonesha ni kwa namna gani ustaarabu na kutaka kuonekana vizuri kwa wengine kulivyo mateso kwetu. Kupenda kwetu kufanya kile ambacho (more…)