Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

💥 #GHAHAWA☕☕; USIPOKEE ZAWADI ZA BURE…

By | May 22, 2017

Habari za jioni rafiki? Hongera kwa siku hii njema uliyokuwa nayo leo? Je ni ushindi gani umepeta leo? Yapi umejifunza leo? Haya ni maswali mawili ya kujibu ili kuimaliza leo vizuri. Karibu kwenye #GHAHAWA yetu jioni ya leo, tushirikishane yale machache muhimu ya kutuwezesha kufikiri kwa makini, na kutoruhusu hisia (more…)

Mambo Matano (05) Muhimu Ya Kuzingatia Wakati Wa Kupanga Bei Ya Huduma Au Bidhaa Kwenye Biashara Yako.

By | May 22, 2017

Kama unazalisha bidhaa zako mwenyewe, au unaandaa huduma zako mwenyewe, kupanga bei ni eneo muhimu sana. Tofauti na wale wanaochuuza, yaani kununua kwa jumla na kuuza kwa reja reja, wao wanakuwa na wigo wa bei tayari umeandaliwa. Lakini wewe unayeandaa mwenyewe, unahitaji kuwa makini wakati unapanga bei. Unaweza kuweka bei (more…)

UKURASA WA 873; Maamuzi Yoyote Ni Bora…

By | May 22, 2017

Kuna hatua huwa tunafikia kwenye maisha yetu, ambapo kufanya maamuzi yoyote ni bora kuliko kutokufanya maamuzi kabisa. Wakati huo tunakuwa tumekwama na hatujui kipi tufanye ili kupiga hatua. Hatuna uhakika wa chochote tunachotaka, lakini pia kwa kutokufanya chochote tunazidi kubaki nyuma. Wakati kama huu ni bora kufanya maamuzi yoyote, hata (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mambo Gani Ambayo Unasimamia Kwenye Maisha Yako?

By | May 21, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo tunajenga misingi imara ya maisha yetu, ili yawe bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Kama nikikuuliza falsafa ni nini utanijibu ni nini? Unaweza kujibu uwezavyo, kwa maana za kitaaluma au kihistoria. Lakini naomba (more…)

UKURASA WA 872; Mshumaa Usioisha…

By | May 21, 2017

Kila kitu kinachotuzunguka, hasa mazingira asili, yana kitu cha kutufundisha kuhusu maisha. Namna maisha yanavyopaswa kwenda ni kwa sheria za asili, ambazo zinasimamia kila kiumbe hai hapa duniani. Hakuna awezaye kuzipindisha sheria hizi na akafanikiwa kwa muda mrefu. Dunia inamshikisha adabu yeyote anayekiuka sheria za asili. Mshumaa unawaka na kutoa (more…)

Uongo Huu Unaojiambia Kila Siku, Ni Adui Mkubwa Wa Mafanikio Yako.

By | May 20, 2017

Huwa najifunza mambo mengi sana kupitia watu ambao wanakuja kwangu wakiomba ushauri juu ya changamoto mbalimbali ambazo wanapitia kwenye kazi zao, biashara zao na maisha kwa ujumla. Na ili kuweza kuwashauri vizuri hatua zipi wachukue, huwa napenda kujua ni hatua gani wameshachukua mpaka pale walipofikia sasa. Kwa sababu kukimbilia tu (more…)

UKURASA WA 871; Kuajiriwa Kula Biskuti…

By | May 20, 2017

Nafikiri kula biskuti ni moja ya vitu rahisi sana hapa duniani. Kwa sababu hata kama huwezi kutafuna, ukiweka mdomoni kwa muda tu italainishwa na mate na unachofanya ni kumeza tu. Hapo bado hujazungumzia utamu wake mdomoni ambao hauchoshi. Leo nilikuwa nafikiri kama yupo mtu ambaye analipwa kwa kula biskuti. Yaani (more…)

UKURASA WA 870; Kazi Itakayojimaliza Yenyewe…

By | May 19, 2017

Leo rafiki nataka nikuulize kitu kimoja, kuhusu kazi ambayo kila siku umesema utaifanya, ila unaendelea kuahirisha. Hivi unapokuwa unaahirisha unakuwa unafikiria nini? Kwamba hiyo kazi kwa muujiza fulani itakuja ijimalize yenyewe? Au kwa muujiza kesho utaamka ukiwa vizuri kuliko leo na kuweza kuanza au kuendelea kufanya? Tabia ya kuahirisha mambo, (more…)

💥 #GHAHAWA ☕; SAHAU GHARAMA AMBAZO UMESHAINGIA…

By | May 18, 2017

Hongera rafiki kwa siku hii nzuri ya leo. Nina imani umeimaliza siku yako ya leo vizuri, ukiwa na mengi ambayo umekamilisha na kujifunza pia. Nikupe hongera kwa hilo. Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye #GHAHAWA ya leo ambapo tunaendelea kuangalia namna tunavyofanya makosa kwenye kufikiri kwetu. Makosa haya ya kufikiri yanatufanya (more…)

Maajabu Ya RIBA MKUSANYIKO (COMPOUND INTEREST) Katika Kujijengea Utajiri.

By | May 18, 2017

Mwanasayansi Albert Einstein amewahi kunukuliwa akisema kwamba; riba mkusanyiko ni ajabu la nane la dunia, anayeielewa ananufaika, asiyeielewa analipa gharama. Kauli hii pekee inatosheleza kukushawishi kwa nini ni muhimu sana kujua na kutumia nguvu ya RIBA MKUSANYIKO au kama inavyofahamika kwa kiingereza COMPOUND INTEREST. Leo tutakwenda kujifunza kwa kina kuhusu (more…)