Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 869; Kama Haiumizi, Haina Thamani…

By | May 18, 2017

Swali; ni mchezo gani ambao unapenda kuufuatilia sana? Mchezo ambao ukiwa unachezwa basi lazima utafuatilia hata kujua matokeo tu, kama huna muda wa kuangalia mchezo wote? Kwa watu wengi, upo mchezo ambao wanapenda kuufuatilia, inawezekana ni mpira wa miguu, ambao wengi wanafuatilia, mchezo wa ngumi, riadha, mpira wa kikapu, mieleka (more…)

UKURASA WA 868; Una Uhakika Hawapo Kazini?

By | May 17, 2017

Kuna wakati unaweza kuwa unashangaa sana kwa nini watu wanafanya kile ambacho wanafanya, kumbe ukawa hujui ya kwamba watu hao wapo kazini. Yaani unachoshangaa wao kufanya, ndiyo kazi yao, na ndiyo wanalipwa kwa kufanya kile unachowashangaa wao kufanya. Au wakati mwingine unawashauri watu kitu lakini hawafuati ushauri wako, au unawaambia (more…)

Tabia Moja Itakayokuwezesha Kudhibiti Matumizi Ya Fedha Zako.

By | May 16, 2017

Umewahi kununua kitu, halafu baadaye ukajikuta unajutia kununua kitu kile? Wakati unanunua ulijishawishi kabisa ya kwamba unakihitaji na umepata kwa unafuu, lakini baada ya kukinunua wala hujawahi kukitumia! Au umekitumia mara chache mno? Hali hii ipo sana kwenye vitu vidogo vidogo kama mavazi, pia tabia hii inawaathiri zaidi wanawake. Swali (more…)

UKURASA WA 867; Kabla Fedha Haijaanza Kukufanyia Kazi….

By | May 16, 2017

Nimekuwa nasema, maana rahisi kabisa ya utajiri na umasikini ni kwenye fedha na kazi. Pale ambapo wewe unaifanyia kazi fedha, yaani bila kufanya kazi huwezi kupata fedha ya kuendesha maisha, basi huo ni umasikini. Na pale ambapo fedha inakufanyia kazi wewe, yaani hata kama hufanyi kazi moja kwa moja bado (more…)

💥 #GHAHAWA; KAMA WATU MILIONI 50 WATASEMA KITU CHA KIJINGA, BADO NI CHA KIJINGA.

By | May 15, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Nina imani kubwa yapo makubwa uliyofanya leo, na pia yapo mengi uliyojifunza. Nikukumbushe kutosahau chochote ulichojifunza. Kwenye #GHAHAWA yetu ya leo tunakwenda kuangalia namna tunavyoponzwa na kundi kubwa, kufanya kitu ambacho siyo sahihi. Kwa mfano umetoka nyumbani na unakwenda kwenye (more…)

Njia Tano (05) Za Kuongeza Mauzo Kwenye Biashara Yako Unazoweza Kuanza Kuzitumia Mara Moja Na Kufaidika.

By | May 15, 2017

Mauzo ndiyo moyo wa biashara yoyote ile, kwa kuwa mzunguko wa fedha ni damu ya biashara, hivyo kinachosukuma mzunguko wa fedha ni mauzo, kama moyo unavyosukuma damu. Hii ina maana kwamba, kama biashara haiuzi, basi biashara hiyo inaelekea kufa, na hakuna namna ya kuiokoa bila ya kuongeza mauzo. Leo tutakwenda (more…)

UKURASA WA 866; Kinachokuzuia Kuona Mbele… … ni kuangalia nyuma.

By | May 15, 2017

Kuangalia umetoka wapi na ulipotoka watu kama wewe wanaweza au hawawezi kufanya nini. Kuangalia ulipokosea huko siku za nyuma na kujutia kwa nini ulifanya jambo la hovyo kiasi hicho. Kuangalia ulipojaribu siku za nyuma ukashindwa, na kujikumbusha kwamba huwezi, hata ukijaribu tena sasa utaishia kushindwa tu. Yote haya yamekuwa yanakusonga (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Ukweli Siyo Kipaumbele Cha Wengi, Na Kwa Nini Ni Muhimu Zaidi Kwako.

By | May 14, 2017

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu, Karibu kwenye makala ya leo ya falsafa mpya ya maisha, ambapo tunakwenda kujenga falsafa mpya ya maisha ambayo inatuwezesha kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Na kwa kuwa maisha ni kile mtu unachochagua, kupitia falsafa hii mpya tunaweza kuchagua kile kilicho bora (more…)

UKURASA WA 865; Vitu Ambavyo Hatujui Kama Hatujui…

By | May 14, 2017

Kuna vitu ambavyo tunavijua, na vipo vitu ambavyo hatuvijui. Hii ni kwenye maeneo yote ya maisha yetu, kuanzia kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla. Katika vile ambavyo hatujui, yapo makundi mawili pia. Kundi la kwanza ni vile vitu ambavyo tunajua hatujui. Yaani hatujui, lakini tunajua ni kipi hicho hatujui. (more…)

Njia Nzuri Ya Kusema HAPANA Kistaarabu, Kwa Wale Ambao Hawawezi Kusema Hapana.

By | May 13, 2017

Moja ya tabia zinazotuzuia kufanikiwa, ni tabia yetu ya kusema ndiyo kwenye kila kitu ambacho tunaombwa na wengine. Katika makala ya mambo manne yanayokuzuia kufanikiwa (unaweza kuisoma kwa kubonyeza maandishi haya) nilieleza kwamba hujawa na roho mbaya vya kutosha. Nikikueleza umuhimu wa kusema hapana kwa yale mambo ambayo wengine wanakutaka (more…)