Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 761; Ukweli Haulazimishwi…

By | January 30, 2017

Ukweli huwa unabaki kiwa ukweli, haulazimishwi wala haubembelezwi, bali unakuwa wazi na kila mtu anajionea mwenyewe. Ukiona mtu analazimisha ukweli, jua kuna kitu kinafichwa ndani yake. Ukiona wewe mwenyewe unalazimisha ukweli ili watu waamini kwenye kile unachotaka waamini, basi jua kuna shida mahali. Na shida kubwa ni kwamba siyo ukweli, (more…)

UKURASA WA 760; Siyo Mara Moja, Ni Kila Mara…

By | January 29, 2017

Tangu umezaliwa mpaka hapo ulipo sasa, kila siku unakula, jana ulikula, leo umekula na kesho utakula, hatuna shaka juu ya hilo. Siku zote za maisha yako umekuwa unaufanyia usafi mwili wako, na kila siku utaendelea kufanya hivyo, utaoga na kusafisha nguzo zako, ni maisha ya kila siku, siyo kitu cha (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; USITOROKE…

By | January 28, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu ambapo tunakwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupata matokeo bora zaidi. Tutumie nafasi hii ya leo vizuri rafiki ili tuweze kufanya makubwa. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTOROKA…. Mara (more…)

UKURASA WA 759; Kila Kitu Kinaweza Kuwa Bora Zaidi…

By | January 28, 2017

Wanasema mafanikio ni nguvu asilimia 10 na mtazamo asilimia 90, na hii ni kweli kabisa. Kwa sababu hakuna kitu kinachowarudisha watu nyuma kama mtazamo. Kile kitu ambacho watu wanakiamini na kukiishi kwenye maisha yao ya kila siku, ndiyo kikwazo namba moja kwa mafanikio yao. Tafiti nyingi mno zimefanywa juu ya (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; THAMANI YAKO NA MAWAZO YA WENGINE.

By | January 27, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufika popote tunapotaka kufika. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu THAMANI YAKO NA MAWAZO YA WENGINE. Moja ya (more…)

UKURASA WA 758; Ushindi Wa Wengine Ni Muhimu Kwetu…

By | January 27, 2017

Duniani tunategemeana, inaweza kuwa moja kwa moja au isiwe moja kwa moja. Kikubwa ni kwamba huwezi kuishi kwenye dunia yako peke yako. Na kwenye dunia unayoishi, pale kila mtu anaposhinda, ndivyo maisha yanavyokuwa bora, na ndivyo na wewe unashinda pia.   Hata wale ambao ni washindani wako wa moja kwa (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MATOKEO BORA….

By | January 26, 2017

Habari za asubuhi rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Leo hii tunakwenda KUTHUBUTU, KUSHINDA NA KUSHUKURU. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu matokeo bora. Kila mtu anapenda matokeo bora, Kila mtu (more…)

UKURASA WA 757; Nenda Kinyume Na Sababu Ulizonazo, Leo Tu…

By | January 26, 2017

Hakuna mtu ambaye hana ndoto kubwa, au hata kama siyo kubwa, basi angalau kila mtu ana taswira ya maisha yake mazuri, anajiona siku zijazo akiwa pazuri kuliko alipo sasa. Hakuna mtu ambaye hapendi mafanikio, kila mtu anapenda kuwa bora zaidi leo kuliko alivyokuwa jana. Lakini kama ulivyo uhalisia wa maisha, (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MAISHA KAMA MCHEZO…

By | January 25, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu, ambapo tuna jukumu kubwa la kwenda kuweka juhudi kubwa, kwa KUTHUBUTU, USHINDI NA SHUKRANI. Asubuhi ya leo tutafakari maisha kama mchezo, Na kama ambavyo tunajua, kwenye kila mchezo kuna watu (more…)

UKURASA WA 756; Una Nini Hapo Ulipo Sasa?

By | January 25, 2017

Watu wengi wana ndoto kubwa za maisha yao, lakini wachache ndiyo wanaoweza kuzifikia ndoto hizo. Kuna usemi kwamba wapo wanaoota ndoto halafu wanarudi kulala, na wapo wanaoota ndoto halafu wanaamka mapema na kwenda kuzifanyia kazi. Zipo sababu nyingi zinazowatofautisha wale wanaofikia ndoto zao na wanaoshindwa, ila moja kubwa ni namna (more…)