Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

ONGEA NA COACH; Kitu Kimoja Muhimu Ninachotaka Wewe Ukijue Kila Siku.

By | October 11, 2016

Habari za leo rafiki yangu, Karibu tena kwenye mazungumzo yetu ya leo ambapo mimi na wewe rafiki yangu tunashirikishana yale muhimu kwa maisha yetu ya mafanikio. Leo nina mengi ya kukushirikisha lakini tutaanza na moja muhimu sana ninalotaka ulijue na kulisimamia kila siku kwenye maisha yako. Kwa kujua hiki na (more…)

UKURASA WA 649; Ufunguo Wa Mlango Wa Kipato Kikubwa….

By | October 10, 2016

Umewahi kuona mtu anakazana na kazi au biashara kwa muda mrefu, kipato chake kinakuwa kidogo lakini baadaye ghafla kipato chake kinaanza kukua kwa kasi sana? Au huenda imewahi kutokea kwako mwenyewe, unaanza kazi au biashara na unakuwa na kipato kidogo, lakini baada ya muda kipato chako kinakua. Kwenye kazi au (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kitu Kimoja Kibaya Ambacho Hatuwezi Kukikwepa, Na Jinsi Ya Kuishi Nacho Kwa Furaha.

By | October 9, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni matumaini yangu kwamba uko vizuri na unaendelea kuboresha maisha yako kupitia falsafa ambayo umekuwa unajijengea kila siku. Endelea kuyafanya maisha yako kuwa bora kila siku maana kadiri siku zinakwenda, tunapaswa kuwa bora zaidi. Leo tunakwenda kuangalia jambo moja muhimu sana kwenye maisha yetu, siyo (more…)

UKURASA WA 648; Kitu Kimoja Kinachoua Furaha Yako…

By | October 9, 2016

Kuna baadhi ya mambo huwa tunayasubiria sana kwenye maisha, tukiamini kwamba tukishayapata basi tutakuwa na maisha ya furaha. Inawezekana ni kumaliza masomo, au kupata kazi au kuanzisha biashara. Tunakuwa tunasubiri kwa shauku kubwa sana, na kuamini baada ya hapo tutakuwa na furaha. Tunapata hicho tulichokuwa tunasubiri, lakini cha kushangaza furaha (more…)

UKURASA WA 647; Hiki Ndiyo Kinachoua Ubunifu Na Ushirikiano…

By | October 8, 2016

Kuna vitu viwili muhimu mno kwa mafanikio kwenye zama hizi tunazoishi. Cha kwanza ni ubunifu, bila ya ubunifu huwezi kupiga hatua. Hii ni kwa sababu kila mtu anafanya kile ambacho unafanya. Na hata ukianza kitu kipya kabisa, bado watu watakuiga kama kitaonesha mafanikio. Hivyo silaha pekee unayoweza kutumia ni kuwa (more…)

UKURASA WA 646; Ufahari Kwenye Kazi Yako…

By | October 7, 2016

Moja ya vitu ambavyo tukiviangalia tunaweza kujua kama kazi au biashara unayofanya itakuletea mafanikio au la, ni ule ufahari ulionao kwenye kazi au biashara hiyo. Je unajisikia ufahari kwa kile unachofanya? Je upo tayari kusimama kifua mbele, mbele ya watu kuwaeleza kwamba hii ni kazi ambayo nimefanya mimi? Je upo (more…)

UKURASA WA 645; Gharama Iliyofichwa…

By | October 6, 2016

Kila kitu kina gharama, namaanisha kila kitu. Hakuna na wala hakujawahi kutokea kitu cha bure, kila kitu kina gharama, tofauti ni kwamba kuna gharama ziko wazi na kuna gharama ambazo zimefichwa. Kila kitu kina gharama kwa sababu hakuna kitu kinachotokea chenyewe. Lazima watu waweke juhudi, wakati mwingine waumie ili kuweza (more…)

UKURASA WA 644; Huhitaji Kutumia Nguvu Kwa Watu Kama Hawa…

By | October 5, 2016

Kitu ambacho najifunza kila siku ni aina tofauti za watu ambao tunahitaji kuchanganyika nao kila siku kwenye shughuli zetu. Katika aina hizi za tofauti, watu wana tabia za tofauti, na mitazamo ya tofauti. Kuna watu ambao wana mtizamo wa kukataa kila kitu ambacho wao hawawezi au hawajui. Yaani watu hawa (more…)

UKURASA WA 643; Zawadi Kubwa Kabisa Unayoweza Kumpa Mteja Wako.

By | October 4, 2016

Umewahi kwenda kwenye biashara fulani kupata mahitaji yako lakini ukatoka pale ukiwa unajisikia vibaya na hutamani kurudi tena pale? Vipi kwa upande wa pili, ulishawahi kwenda kwenye biashara fulani na ukajisikia vizuri sana, ukatamani kurudi tena na kila unayekutana naye unamweleza kuhusu biashara ile? Naamini umeshakutana na hali hii mara (more…)

UKURASA WA 642; Kuanzisha Biashara Siyo Kugumu, Ugumu Uko Hapa…

By | October 3, 2016

Kuanzisha biashara hakujawahi kuwa zoezi gumu, japo wengi huwa wanafikiria hivi. Huwa wanaona ni vigumu sana kuanzisha biashara kwa sababu wamekuwa anaangalia ni kipi wanakosa. Kwa kuangalia wanachokosa wanashindwa kutumia kile walichonacho kwa wakati huo. Mtu yeyote kwa kutumia mazingira na hali aliyonayo, anaweza kuanzisha biashara yake, kubwa au hata (more…)