Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maisha Siyo Mabaya Kama Unavyoaminishwa Kila Siku.

By | October 2, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye makala yetu ya leo ya falsafa mpya ya maisha, ambapo tunapena maarifa sahihi ya jinsi ya kuishi maisha yetu, kwa ubora na furaha. Unaishi hivyo unavyoishi kutokana na falsafa ya maisha ambayo umeibeba. Tatizo la jamii zetu ni kwamba hatuchagui wenyewe falsafa ya (more…)

UKURASA WA 641; Miliki Maisha Yako…

By | October 2, 2016

Unaweza kuchagua uvae viatu vya aina gani, kwa sababu unaweza kuwa na aina tofauti za viatu. Unaweza kuchagua ni chakula cha aina gani ule, kwa sababu kuna vyakula vingi unavyoweza kuchagua. Lakini inapokuja kwenye maisha yetu, huwezi kuchagua maisha mengine zaidi ya hayo uliyonayo sasa. Huwezi kusema unabadili maisha na (more…)

UKURASA WA 640; Hichi Ndiyo Unapata Kwenye Maisha Yako…

By | October 1, 2016

Mara kwa mara nimekuwa nasema tunachopata kwenye maisha ni kile ambacho tunakitafuta, kile ambacho tunafanyia kazi. Na hii ndiyo maana wale wanaofanya kazi za kawaida wanapata matokeo ya kawaida. Wale wanaofanya kazi za tofauti wanapata matokeo ya tofauti. Pia kadiri mtu anaweka juhudi ndivyo matokeo yake yanakuwa bora. Lakini swali (more…)

UKURASA WA 639; Maana Halisi Ya Wivu Na Kuiga…

By | September 30, 2016

Mwandishi na mwanafalsafa Ralph Waldo Emerson aliwahi kusema kila mtu atafikia hatua kwenye elimu yake ambapo atagundua WIVU NI UJINGA na KUIGA NI KUJIUA MWENYEWE. Na sina neno la ziada zaidi ya hayo maana ndiyo ukweli wa maisha. WIVU NI UJINGA. Ndiyo, hakuna namna nyingine tunayoweza kuusemea wivu zaidi ya (more…)

UKURASA WA 638; Sababu Kubwa Kwa Nini Unarudia Makosa Yale Yale…

By | September 29, 2016

Moja ya hitaji kubwa sana la kuweza kuishi maisha bora na ya mafanikio, ni kupenda ukweli na kuishi ukweli. Tunapozungumza ukweli mara nyingi tunafikiria kutokusema uongo na vitu kama hivyo. Lakini huwa tunasahau kuhusu tabia zetu wenyewe. Tumekuwa tunajidanganya sana kuhusu tabia zetu wenyewe. Kila mtu anapenda kutetea tabia yake (more…)

UKURASA WA 637; Upo Mahali Sahihi Na Huu Ni Wakati Sahihi…

By | September 28, 2016

Ili ufanikiwe, unahitaji kuwa mahali sahihi na kwa wakati sahihi, hii ni kauli ambayo tumekuwa tunaisikia kila siku. ni kauli yenye maana kubwa, lakini watu hawaichukulii kwa uzito wake. Watu huichukulia juu juu kwamba wanatakiwa kuwa sehemu sahihi na kwa wakati sahihi. Hivyo kama sasa hawafanikiwi, moja kwa moja wanachukulia (more…)

UKURASA WA 636; Ishi Maneno Yako…

By | September 27, 2016

Mara zote matendo yanaongea kwa sauti kuliko maneno. Kuna usemi wa wanafalsafa kwamba matendo yako yanaongea kwa sauti sana kiasi kwamba mtu hasikii kile unachoongea. Ukweli ni kwama unaweza kupiga kelele utakavyo, unaweza kusema chochote unachotaka kusema, lakini mwisho wa siku watu wataangalia matendo yako. Je unaishi maneno yako? Je (more…)

UKURASA WA 635; Hofu Ya Kuambukizwa…

By | September 26, 2016

Binadamu ni viumbe wa kijamii, tunajisikia salama pale ambapo tunakuwa kwenye jamii ambayo inafanya kile ambacho sisi pia tunafanya. Ndiyo maana unakuta kuna watu wanakunywa pombe siyo kwa sababu wanapenda, ila kwa sababu marafiki zao wanakunywa. Sasa hii inakwenda mpaka kwenye hofu, hakuna mtu ambaye anapenda kuwa na hofu na (more…)

UKURASA WA 634; Haijalishi Uko Wapi, Inajalisha Nini Kipo Ndani Yako.

By | September 25, 2016

Nimewahi kutoa mfano huu kwenye makala za nyuma, lakini leo nitaurudia tena ili tuweze kujifunza. Kijana mmoja alikuwa na babu yake wamekaa nje barazani wakipiga hadithi, sehemu waliyokaa ni pembezoni mwa barabara ambapo watu wanapita. Wakati wanaendelea na hadithi zao, wakapita watu na mizigo, wakasimama na kuwauliza, sisi tumetoka eneo (more…)

UKURASA WA 633; Aina Mbili Za Kushindwa…

By | September 24, 2016

Kwenye maisha, kazi na hata biashara, zipo aina mbili za kushindwa. Lakini kabla hatujaangalia aina hizi, kwanza tuangalie kushindwa. Kushindwa ndiyo kitu ambacho kimekuwa kinawapa wengi hofu pale wanapotaka kufanya mambo makubwa kwenye maisha yao. Lakini hofu hii imekuwa haiwasaidii chochote, badala yake imekuwa inawazuia kufanya yale makubwa kwenye maisha (more…)